Kufuatia tetesi za Manji kukodishwa timu, tunaomba majibu ya maswali haya

thats way i told u tafuta habari kami kwamba we mwenyewe wajua kwamba ni vigumu kukodisha
 
Wakati mnakula pesa zake mlishajiuliza maswali yote huyo?
 
Elimu ni tatizo kubwa sana kwa Watanzania, Sio elimu ya Darasani tu hata elimu ya kuchanganua Mambo..Mtu anashangilia kabisa Club ya kukodishwa. Mbaya zaid inakodishwa kwa Mwenyekiti wa Club..Me ni Mshabiki wa Yanga sema bado siielewi hii Kukodishwa Model ya Manji..
 
Acheni bla bla zenu hamjawahi kuichangia Yanga hata shilingi kumi..Maendeleo ya sasa hivi ya Yanga kutaifa na kimataifa yametokana na ufadhili wa Manji...Manji ameisaidia sana Yanga hata akiikodisha kwa miaka 100 ni sawa tu
Hujui majukumu yako
 
Hawa jamaa wameshangaza ulimwengu.. halafu sasa hivi wametepeta kiasi kwamba hata manji aseme nini wao ndiyo mzee.. ndio mzee
 
Mleta thread usitengemee kupata majibu hapa! na media zinazo report michezo washapewa mpunga kupumbaza hii ngoma Yanga wameingizwa cha kike!

Mzee Regnald Mengi sijui atakuwa kwenye hali gani hadi muda huu
 
Ukitoa Nyumba yako kwa mtu mmoja kwa hisa za 51%ni kwamba umehamisha umiliki kwa mtu huyo ila ukipangisha kwa mkataba wa hasara wa miaka kumi kuna mawili.
1.Nyumba bado ni yako.
2.uivumilie hasara kwa miaka kumi au uvunje mkataba umlipe.

Unapompa mtu kwa 51% napo kuna mawili.
1.Nyumba si mali yako tena.
2.ukitaka kuimiliki tena umwombe akuuzie hisa kwa bei anayotaka yeye (itategemea kama atataka kuuza)
 
Acheni bla bla zenu hamjawahi kuichangia Yanga hata shilingi kumi..Maendeleo ya sasa hivi ya Yanga kutaifa na kimataifa yametokana na ufadhili wa Manji...Manji ameisaidia sana Yanga hata akiikodisha kwa miaka 100 ni sawa tu
Kwanza hatupingi yy kukodishwa ila njia za kukodishwa hazijawa sawa, ilipaswa ajihudhuru kwanza halafu aje na mapendekezo kutoka kamati ya utendaji, kuhusu namna bora anayoona inafaa kuiendesha club,

Sasa hebu tazama kizingumkuti mkuu, mwenyekiti ni manji, mfadhiri manji, anaeomba kukodishiwa timu manji,

Sasa umeona mkuu, sasa heb rudi nyuma, nan anawazo hlo?ni manji, nan anamtaji manji, nan kauitisha mkutano manji, c ajabu hata wanachama wamelipwa posho na manji,

Mkuu yanga haiko dar, hvi nan anamiliki majengo ya yanga na aset zate? Kama ni wanachama, kwa mjib wa katba ya yanga nan anakuwa msemaji na mwenye mamlaka? Unaweza kukuta ni mwenyekiti..


Kinachotokea ni kuwa viongozi wote wa yanga wamekuwa kama nyumbu, hawana tena usemi, wapo kama hawapo....

Na wasipoangalia tim inakwenda kushuka daraja na hapo ndipo yanga watakapostuka, yanga wamekuwa kama wameolewa hawana usemi, hawahoji, hata swali dogo tu kuwa hyo aslimia 25, ni mtaji kiasi gani hawahoji, afadhari mo kasema kiwango kuwa ni b20 kwa 51%, je manji[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15]
 
Hatua zozote zinachokuliwa na MANJI ni MWIBA kwa MAKOMANDOO na wale wote walioiishi muda mrefu kwa Kuitegemea Yanga, ikumbukwe kuna WATU(Wanachama) wameelimisha Watoto (Shule) kwa mgongo wa Yanga,kuna baadhi wamejenga Nyumba kupitia Yanga,kuna watu Wanamiliki magari mazuri tu kwa jasho la Yanga,....Leo hii walio mstari wa mbele kuhoji hatua zozote ambazo Manji anafanya kwanza mchunguze,Je ni kweli ana wanachungu kweli na Yanga ? wanachangia kiasi gani maendeleo ya Yanga,? Lini alitengeneza Proposal yoyote juu ya namna gani Yanga ifanye iliisonge mbele? Jiulize hizi Page za Facebook,Twitter,au mawasiliano kwenye Instagram,Whattsapp,zinaweza kweli kufikisha mchango(mawazo) kwa Uongozi wa Yanga hasa mwenyekiti Yusuf Manji? au staili hii ni mbinu za kupayuka ili Mwenyekiti akuiite akuambie acha kupayuka na bahasha mkononi?, Hivi kuikodisha NEMBO ya Yanga na kubaki na Makomandoo wanaoitafufana klabu lipi lenye faida ?,.Kuendesha mpira zama hizi ni gharama, hiki siyo kile kipindi cha kusajili mchezaji kwa mapenzi ya klabu,ukifanya hivyo utaiishia kupata wachezaji wa kiwango cha chini na hatimaye timu inafanya vibaya na kushuka daraja,fahari itabaki Majengo kama walivyo PAN AFRICA.
 
Vitu vinavyoongoza kununuliwa Dar
Unga wa mahindi
Mchele
Matunda ya msimu e.g. machungwa kwa sasa
Vyangudoa
Nyanya mbovu (masalo)
Simba Sports Club
Etc
 
Mtoa mada ana hoja ya msingi. Ila haikupaswa kujibiwa sasa ilivyokuwa huo mkataba wa ukodishwaji haujafikiwa. Kama maelezo ya mkutanoni yameeleweka vizuri, kilichowasilishwa na Manji mkutanoni ni taarifa tu ya jambo hilo ili wanachama wajue. Hatua rasmi iliyofikiwa ni maombi hayo kupelekwa kwa Baraza la Wadhamini. Hao ndio wenye maamuzi. Wakikubaliana ndio hatua ya mkataba inafuata. Na hapo ndio hoja za mtoa mada zitapostahiki kuzingatiwa. Kwa maneno mengine, kauli ya wanachama kumkubalia Manji ni maoni yao tu hadi sasa, kama yalivyo ya wanachama wa Simba kumkubalia Mo kumiliki 51% ya hisa za Simba baada ya yeye kuingiza mafao yatokanayo na ununuzi wa Hati Fungani za Serikali za Shilingi 20bn. Kwa sasa, si Simba wala Yanga imeshafikia makubaliano na Mo ama Manji ingawa kuna dalili wote watakubaliwa.
 
Vitu vinavyoongoza kununuliwa Dar
Unga wa mahindi
Mchele
Matunda ya msimu e.g. machungwa kwa sasa
Vyangudoa
Nyanya mbovu (masalo)
Simba Sports Club
Etc
Kipi cha ajabu kununuliwa hapo sasa...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…