Kufuatia tetesi za Manji kukodishwa timu, tunaomba majibu ya maswali haya

Kufuatia tetesi za Manji kukodishwa timu, tunaomba majibu ya maswali haya

Sawa kabisa. Sasa niondolee shaka hii; wale wanachama watakaokataa kuridhia jambo hilo, watalindwa au watapigiwa kura ya kuvuliwa uanachama?
Itakuwa wengi wape basi. Hata huko Simba umesema vema kuna watu hawataki lakini imepita Kwa majority.
Waliovuliwa uanachama kuna mengi ndani yake. Si suala la kukodisha timu pekee. Wachezaji walishasema na iliandikwa kwenye magazeti kuhusu kuwarubuni wacheze chini ya kiwango.
 
Yanga kuna tatizo fulani nadhani. Walioonyesha hali ya kukosoa jambo hilo, uongozi wa klabu uliweka mezani hoja ya kuwavua uanachama, na kweli wakavuliwa. Anayeongoza kikao na kuweka hoja ya kuwavua uanachama wanaopinga hilo, ndio huyo huyo mkodishwaji. Kulikuwepo mgongano wa maslahi hapo
Hapa ndipo tulipokosea Yanga, uongozi unaokuja atawapendekeza yeye kulingana na hotuba yake.

uongozi huo utajadili hili suala chini ya uenyekiti wa manji, wakimaliza katibu atasaini kwa niaba ya mwenyekiti manji kumkosisha manji atakaye saini kama mkodishwaji.

aisee, haya mambo serikali wayaingilie bora tufungiwe na fifa
 
Na Je ikitokea yanga inashuka daraja mwaka huu nini hatima ya wanachama kwenye club hiyo, na Je Manji ataendelea na huo udhamini na vipi mkataba unasemaje kuhusiana na hicho kipengele?
 
Muhindi kawashika pabaya watani zangu......mimi nilijua tu zile zile heka heka za Manji kujifanya msamalia mwema hazikuwa za bure.......

Mimi nilifurahi pale niliposikia kuwa majengo yeye hana kazi nayo....na wanaYanga wanashangilia kama wamerukwa na akili......

Ukitumia akili yako kidogo tu utaona jinsi Manji anavyotaka kuwadhurumu klabu yao majirani zetu.....
 
Wabongo wengi ni ma slow learner,lakini bado wanajifanya wajuaji,yangu macho.
 
Kuna mashabiki wengi na wanachama wachache waaminifu wanaolipa ada,acheni timu apewe Mwenyekiti ameisaidia sana tu mpaka tulipo
 
Back
Top Bottom