FisadiKuu
JF-Expert Member
- Nov 19, 2015
- 8,169
- 13,455
Habarini za Asubuhi wakuu.. Kuna shida nimeipata na ningeomba kusaidiwa ushauri wa kitaalamu..
Mzee wangu alikuwa na kampuni iliyokuwa inajihusisha na biashara flani flani (ilikuwa na General Company) na ilifanya shughuli zake kuanzia mwaka 1990 mpaka kwenye 2006-08.. Kuanzia hapo ikawa dormant, haikuwa inafanya chochote. Mimi nilipomaliza chuo kikuu sikujishughulisha nayo na nikaenda kuajiriwa.. Lakini huku kwenye kufanya kazi za watu mambo ni magumu. Mshahara ni mzuri lakini sijisikii kuwa huru bali kutumikishwa. Sasa nikawa na wazo la kuacha ajira na nifufue kampuni ile ya mzee nifanye shughuli zangu huko. Nae nilipomfata akanikubalia sababu yeye ameshachoka sasa (he is in late 60's now).. Akanipatia document zote, sasa nikampigia rafiki yangu mmoja wa TRA aniangalizie record ya ulipaji kodi huko kabla ya mimi sijatia pesa yangu hapa nisije pata hasara. Jamaa akanirudishia majibu kwamba kampuni haionekani kwenye records zao kuanzia mwaka 2009 mpaka 2015. Hii kidogo ikaniogopesha..
Lakini mimi nilikuwa nimepanga kufanya yafuatayo.. Kuifanya kampuni iwe Limited company na kila mwanafamilia apate share yake, nimeshaandaa Articles and Memorandum of association, Je, hapa kwenda BRELA kushughulikia ni lazima nisafiri kwenda Dar au?? Na Je, hii itanichukua siku ngapi kukamilisha?? Pili, hili swala la TRA litamalizika? Wataamini kwamba kampuni ni kweli ilikuwa haifanyi kazi (hapa nimeangalia na huu upepo wa kisiasa sasahivi, wasije wakadhani kwamba tulikuwa tunakwepa kodi na baada ya Rais mpya kuingia ndio tunajifanya kampuni haikua hai). Tatu, Je kuiprocess hii kampuni mpaka iwe hai tena na kuanzisha nyingine lipi ni rahisi (mimi nilitaka kuifufua hii sababu ina reputation nzuri kwa wateja wake kuliko kuanza na mpya ambayo haijulikani)
Wakuu The Boss Ngongo na wengineo ningeomba ushauri wenu juu ya hili...

Last edited by a moderator: