Inategemea na aina ya silaha na risasi inayotumika kufanyia jaribio hilo.
Ila risasi karibu zote za rifle na pistol (siyo shot gun) zinafungua kufuli kutokana na kasi na uzito wa kishindo chake: na hapa naeleza kwa lugha rahisi.
Halafu risasi kukita sehemu halafu irudi nyuma jambo hilo haliwezekani hata ungelifyatua kwa umbali mfupi kiasi gani.
Kama object unayoipiga ni ngumu kuhimili mpenyo wa risasi, basi risasi hiyo huyeyuka na kusambaa, utakuta vipande vilivyoyeyuka vimesambaa hapo chini.
Hii hutokea hata ukipiga jiwe, risasi huyeyuka na huwa hairudi ilikotoka.
Madhara unayoweza kuyapata kwa kupiga umbali mfupi ni zile cheche za moto kama risasi hiyo itashindwa kupenya hata kwa upenyo mdogo.
Lakini kwa material yaliyotengenezea kufuli(shaba ya njano), ukipiga risasi, kishindo kile kitaiyeyusha kufuli hiyo na kusambaa yote kabisa.