Nilikua na washkaji wengi kabla ya kufunga ndoa na ndugu wengi nilikua nawachangia sana kwenye misiba na harusi lakini Mimi nilivotangaza ndoa wakaniunga mkono muda ulipofika nikipiga cm wana hawapokei wala kujibu text
Nikakausha nikakomaa likapita saivi wengine wanaishia kuview status WhatsApp tu na wengine tukionana wanajikanyaga tu
Nimeamua saivi nitachangia misiba tu Teena ila ya moja kwa moja cjui kipaimara harusi cjui nini mwisho na Nina list ya walionichangia ndo nataka tu kuwarudishia michango yao baasi
Sent from my TECNO RA7 using
JamiiForums mobile app
Habari za kuchangishana kwenye harusi na misiba ni habari za ujima.
Tutengeneze uchumi utakaowezesha watu kugharamia harusi na mazishi yao wenyewe.Ikibidi hata kwa bima maalum za maisha na mifuko maalum ya kuweka akiba za harusi.
Kama mtu anaamua kutoa iwe zawadi kwenye harusi au kusaidia familia vitu vikubwa kwenye misiba.
Naelewa hali ilivyo, na kwamba haya mambo labda yanahitajika kwa sasa, na kwamba yameonekana kama sehemu ya utamaduni, lakini, kimsingi, ni maishabfulani ya kijima yanayojiondoa katika kujitegemea.
Pia, kwenye harusi watubwengi wanaendekeza harusi kubwa zenye gharama sana wakati hawananuwezo wa kiuchumi kuzi support harusi hizo na kuishi maisha yaliyo sawa na harusi hizo. Na gharama hii inabebwa na michango.
Michqngo ya harusi inakuwa mingi kuliko michango ya shughuli za maendeleo.
Utasikia sana watu wanachangishana harusi, lakini husikii watu wakichangishana hivyo kwenye biashara au kusoma.
Hii ni dalili ya jamii inayoendekeza kubembea badala ya kufanya kazi.
Tufikie wakati iwe nibjambo la aibu mtu kuhitaji kuchangiwa ili kufanikisha harusi yake.
Ikibidi vijana, kama wanatakanharusi za kifahari, waanze kuweka akiba tangu wadogo.
Mbona nyumba watu wanajenga bila kuchangiwa na jamii?
Sasa hivi tunatengeneza mpaka uhasama kwa sababu ya michango ya harusi, urafiki unakwisha kwa sababu ya michango ya harusi.
Mbona zamani watu walifanya harusi simole sana na ndoa zilidumu vizuri tu?
Kwani ni lazima kufanya harusi zenye gharama kubwa sana?
Ni jambo la kuhuzunisha sana.