Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Tatizo linakuja tukianzia hapo kwenye mentality ya kudai michango.Pole sana mkuu,
Hii michango inaleta uhasama sana kimsingi tu naona bora nisichangishe maana kuidai hio michango ni shughuli kweli kweli
Tumefanya michango kama aina fulani ya social insurance.
Unamchangia mtu ukitegemea na yeye atakuchangia, kitu ambacho si lazima.
Mchango unatakiwa uwe kama zawadi, unachangia ukijua huyu anaweza kunichangia au anaweza asinichangie, after all, hatujui kesho yake itakuwaje. Hatujui hata kama atakuwa hai.
Unqtakiwa ujue kuwa mimi nahitaji kuwa na uwezo wa kufanikisha shughuli yangu either way.
Sasa, tatizo letu tumefanya michango kuwa ni uwekezaji, ukiwekeza unahitaji kurudishiwa, na usiporudishiwa inakuwa ugomvi.
Hapo ndipo naona imefika wakati tuachane na michango ya harusi. Kama mtu anataka kutoa zawadi, atie zawadi tu.
Michango inaleta pressure sana.
Imagine umeomba watu michango wakatoa watu wengi sana hela nyingi sana.
Hilo linamanisha nini?
Kwamba na wewe itakubidi utoe hela nyingi sana kuchangia harusi za watu wengi sana?
Kama huna?
Hatuoni hapo tunatengeneza tatizo?