KUFUNGIWA REDIO IMAAN NA NYINGINEZO: haki haijatendwa!

Tumo katika nchi inayofuata sheria. nchi yoyote ile lazima iongozwe kwa kufuata sheria. TCRA ni chombo kinacho simamia vyombo vya habari vya kielektroniki hasa redio na televisheni. kina mamlaka ya kuonya au hata kufungia chombo cha habari kinacho kiuka maadili ya utangazaji.

redio imaan ya morogoro na kwa neema fm ya mwanza zimefungiwa na kamati ya maudhui (content committee) iliyo chini ya TCRA. clouds fm ya dsm imeonywa na kutozwa faini ya 5,000,000/=. sababu iliyo tolewa ya kuifungia redio imaan ni kuhamasisha waislamu wasishiriki katika sensa ya mwezi agosti mwaka jana. kuhusu kwa neema fm imeelezwa kuwa imehamasiha kwa zaidi ya miezi 4 wakristo wasile nyama iliyochinjwa na waislamu hadi uhamasishaji wao ukasababisha watu kuuana!. clouds fm inasemekana walicheza clip ya askofu wa marekani aliekua akiunga mkono ushoga. watangazaji waliiunga mkono kauli yake na kusema kuwa mashoga waruhusiwe. ni haki yao.

lengo lango ni kuizungumzia redio imaan huku nikiakisi redio nyingine mbili. ni takriban miezi 7 tangu sensa ya watu ifanyike. kwa mujibu wa bbc jana jioni, mkurugenzi wa redio imaan alipohojiwa alisema kuwa redio yake ilikua ikiripoti maoni ya watu kuhusu kipengele cha dini kuwekwa kwenye dodosa za sensa. alisema kuwa japo kila mtu ana uhuru wa kuisikiliza redio imaan lkn imewalenga sana waislamu. waislamu ndiyo wenye redio na michango yao ndiyo inaifanya redio iwepo. alisema kuwa waislamu walijenga hoja kuwa wanabaguliwa katika mambo mengi hasa ajira serikalini kwa madai kuwa ni wachache. wao wanaamini ni wengi. walitaka kwenye dodosa kiwekwe kipengele cha dini ili ukweli ujulikane kama zifanyavyo nchi nyingine. alisema kuwa mada ilianzishwa na watu wakawa wanapiga simu kuchangia mada hiyo.

aliendelea kusema kuwa katika kipindi cha miezi 7 iliyopita, hajawahi kupokea barua kutoka TCRA ikimuonya kuhusu mada ya sensa! inakuaje afungiwe ghafla bila hata karipio!? alisema vipindi vya redio imaan vimekua vikiendeshwa kwa ueledi na kwa kuzingatia taaluma ya utangazaji. redio imaan haijawahi kuhamasisha mtafaruku, kuhatarisha amani na kusababisha vifo vya raia. imekua daima ikieleza na kuripoti ukweli kuhusu mambo mbalimbali yanayotukia hapa nchini.

MY TAKE:
ukiangalia kosa la kwa neema fm, utagundua kuwa uhamasishaji ulikua wa wazi na hadi ulikaidi amri ya serikali ya kuomba uchinjaji uendelee huku suluhu ikitafutwa. redio ilipuuzia agizo la serikali na kuendelea na uhamasishaji bila ya kuangalia madhara yake. matokeo yake watu wakauana! inakuaje clouds fm inayo shabikia ushoga ipewe karipio na kutozwa faini lakini redio imaan inafungiwa! watu kudai haki ya kutambuliwa katika dodosa za sensa na wanaohamasisha ushoga ni yupi anaekiuka maadili na katiba ya nchi?

kazi kwenu wadau kutoa majibu yenye hoja zilizo kwenda shule!

naomba kuwasilisha!
Si kila kosa linapitia karipio... Hata kwenye mpira wa miguu, kuna makosa mchezaji akiyafanya, ni red card moja kwa moja.. Kwa hiyo sikubaliani kwamba walitakiwa wapewe karipio. Kwanza wamechelewa kuwafungia, nadhani walikuwa wanasubiri wakubalansia mambo, na ndo wakampata kwa neema FM
 
suala hapa ni kulikua na kosa gani redio kurusha hewani maoni ya watu waliokua na madai ya msingi kuhusu sensa?.
Kigezo gani kilitumika kuyajudge madai ya waislamu kuhusu sensa kuwa ni yasiyofaa?.
Kwamaana nyingine serikali inawaambia waislamu kuwa wao hawana haki humu nchini.
Je,serikali itafuta vipi hisia hizi za kuwepo mfumo kristo kama badala ya kuclarify issue kama MOU ,WAO WANAKIMBILIA KUIFUNGIA redio kwa kuexpose MOU ,huku wakidaganya kuwa sababu ni sensa?
 
haya tumekuelewa sheikh ubwabwa na tumewazoea coz kila kitu mnaona nyie ndo mnahaki coz utetezi wako ni dhahiri kwa kituo cha redio cha WAHUNI CHA IMANI wewe kwa mtazamo wako mfupi wa kikaidi unaona eti wameonewa hao unaowatetea na kwamba waliofanya makosa ni KWA NEEMA NA CLOUDS tu...unajitia ujinga mwenyewe na upofu...tunasubiri maandamano ya wato waliovaa kofia vikarai na magauni meupe pamoja na makobaz kutaka serikali iifungulie redio iman na kuifungia clouds na kwa neema fm

Tumo katika nchi inayofuata sheria. nchi yoyote ile lazima iongozwe kwa kufuata sheria. TCRA ni chombo kinacho simamia vyombo vya habari vya kielektroniki hasa redio na televisheni. kina mamlaka ya kuonya au hata kufungia chombo cha habari kinacho kiuka maadili ya utangazaji.

redio imaan ya morogoro na kwa neema fm ya mwanza zimefungiwa na kamati ya maudhui (content committee) iliyo chini ya TCRA. clouds fm ya dsm imeonywa na kutozwa faini ya 5,000,000/=. sababu iliyo tolewa ya kuifungia redio imaan ni kuhamasisha waislamu wasishiriki katika sensa ya mwezi agosti mwaka jana. kuhusu kwa neema fm imeelezwa kuwa imehamasiha kwa zaidi ya miezi 4 wakristo wasile nyama iliyochinjwa na waislamu hadi uhamasishaji wao ukasababisha watu kuuana!. clouds fm inasemekana walicheza clip ya askofu wa marekani aliekua akiunga mkono ushoga. watangazaji waliiunga mkono kauli yake na kusema kuwa mashoga waruhusiwe. ni haki yao.

lengo lango ni kuizungumzia redio imaan huku nikiakisi redio nyingine mbili. ni takriban miezi 7 tangu sensa ya watu ifanyike. kwa mujibu wa bbc jana jioni, mkurugenzi wa redio imaan alipohojiwa alisema kuwa redio yake ilikua ikiripoti maoni ya watu kuhusu kipengele cha dini kuwekwa kwenye dodosa za sensa. alisema kuwa japo kila mtu ana uhuru wa kuisikiliza redio imaan lkn imewalenga sana waislamu. waislamu ndiyo wenye redio na michango yao ndiyo inaifanya redio iwepo. alisema kuwa waislamu walijenga hoja kuwa wanabaguliwa katika mambo mengi hasa ajira serikalini kwa madai kuwa ni wachache. wao wanaamini ni wengi. walitaka kwenye dodosa kiwekwe kipengele cha dini ili ukweli ujulikane kama zifanyavyo nchi nyingine. alisema kuwa mada ilianzishwa na watu wakawa wanapiga simu kuchangia mada hiyo.

aliendelea kusema kuwa katika kipindi cha miezi 7 iliyopita, hajawahi kupokea barua kutoka TCRA ikimuonya kuhusu mada ya sensa! inakuaje afungiwe ghafla bila hata karipio!? alisema vipindi vya redio imaan vimekua vikiendeshwa kwa ueledi na kwa kuzingatia taaluma ya utangazaji. redio imaan haijawahi kuhamasisha mtafaruku, kuhatarisha amani na kusababisha vifo vya raia. imekua daima ikieleza na kuripoti ukweli kuhusu mambo mbalimbali yanayotukia hapa nchini.

MY TAKE:
ukiangalia kosa la kwa neema fm, utagundua kuwa uhamasishaji ulikua wa wazi na hadi ulikaidi amri ya serikali ya kuomba uchinjaji uendelee huku suluhu ikitafutwa. redio ilipuuzia agizo la serikali na kuendelea na uhamasishaji bila ya kuangalia madhara yake. matokeo yake watu wakauana! inakuaje clouds fm inayo shabikia ushoga ipewe karipio na kutozwa faini lakini redio imaan inafungiwa! watu kudai haki ya kutambuliwa katika dodosa za sensa na wanaohamasisha ushoga ni yupi anaekiuka maadili na katiba ya nchi?

kazi kwenu wadau kutoa majibu yenye hoja zilizo kwenda shule!

naomba kuwasilisha!
 
Al shaabab mmeanza, yaani hamkosi pakuanzia. TUMEWACHOKA BHANA!

Hapo ndio mwisho wako wakufikiri kweli akili ni nywele kila mtu anazake

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
mdau mipaka gani unayomaanisha hapa?na ishu si kwamba kila muislam aiunge mkono,mfano mawaidha ya redio imaan yalikua yanakataza pombe,riba,zinaa,sasa muislam anayemiliki bar ataiunga mkono redio imaan?ukiandika kuwa si waislam wote wanaiunga mkono redio imaan,huenda ukawa ryt nami nakwambia si watz wote wanamkubali jk japo ni rais,maana si lazima.REDIO IMAAN IT WAZ OUR VOICE,NA INSHALLAH ITARUD HEWAN AFTA 6 MONTHS,KWA IDHIN YA ALLAH.

Acha kumkosea ALLAH!!

Redio si chombo cha Allah kuwakilisha mawazo ya walio waislamu dhidi ya watu au dini nyingine!! Na wala usitake kuonesha hapa kuwa sasa serikali imemshinda Allah kwa kufunga chomba anachokitumia kuzungumza na binadamu!! Biblia inasema "Kila kitu kitapita isipokuwa neno la Mungu". Redio imani imepita angalau kwa hii miezi 6!! Na sauti ya redio imani imenyamazishwa na mamlaka za kidunia. Sauti ya Mungu itabaki mioyoni mwa wanaomfuata!!

Mipaka ninayoizungumzia mimi ni ya kuheshimu uwepo wa dini na watu wengine!! Uwepo wa mawazo mengine na uhuru wa kuchagua namna ya kuishi bila kuvunja sheria za Taifa linaloitwa Tanzania. Usizungumzie riba, zinaa, pombe wakati nchi yako inaendeshwa kodi za pombe, sigara na vitu vingine.

Nitaacha mada hii, ninagundua una uelewa finyu wa mada yangu kuu - kuhatarisha misingi ya utaifa kwa kutumia sababu za kidini!!
 
Mwana JF SCarmble. Clouds ni redio inayopendwa na Mkuu wa Kaya. Nakumbukaaliwahi kusema akitaka muziki basi Ruge huwa anamuwekea ktk Ipod. Clouds wanashabikia kila jambo la CCM has kupitia Jahazi. Clouds walikuwa mbele kuwananga madaktari wa Tanzania. Kila hoja za wabunge wa upinzani wanazinanga. Hivyo usitegeem TCRA ya magamba wawafungie Clouds fm. Ile imetumika kama cover ya kuwamaliza Imaan FM. Inshaalah ukweli na haki itadhihiri. Imaan FM pamoja na kufungiwa itapanda chati zaidi ikirudi hewani.
 
inaelekea hujawahi kuisikiliza hiyo redio. mimi siyo mfanyakazi wa redio imaan. nimeleta mada hii kwa sababu leo redio imaan kesho zitakua redio nyingine. hoja yangu ni kwamba kuwe na sababu zenye mantiki za kukifungia chombo cha habari. leo hii watu wanalalamika kuhusu gazeti la mwanahalisi..........

umewahi kuisikiliza redio imaan? una uhakika kuwa mimi ni muislamu? jenga hoja acha ushabiki wa kijiweni
Mkuu siyo ushabiki ni kitu ninachokwambia, uwezi jua labda iliundiwa tume, na majibu ndo wametoa baada ya hiyo miezi saba.. tume ngapi zinaudwa hazitoe majibu? Na bora hiyo iliyopewa madaraka yakuchunguza iman imetupa majibu. shem on u, eti si msilamu? thubutu......
 
Back
Top Bottom