Kufungua kituo cha radio kinagharimu kiasi gani?

Kufungua kituo cha radio kinagharimu kiasi gani?

Zipo nyingi ila watu hawajawekeza serious, ukiweka mzigo kama alionao jamaa hapo juu unatoboa, una vijana wako kibao wa habari, unaajiri vijana wa kuandaa makala zako japo kila week,

Lazima utoboe mzee
Siku hizi wanawekeza kweli. Kuna online media zinasajili watangazaji kutokea electronic media.
 
Natamani sana kama hili nitalifanikisha, kuwepo vipindi vya vijana na ujasiriamali,mambo ya uvumbuzi, mijadala ya vijana kuhusu ukuaji, wkend nyimbo za injili na za kiafrika; mambo ya habari na siasa yanakuwa hayapo.
Kwa mazingira hayo nitakuwa naingiza maokoto kweli?​
Kwa mujibu wa sheria taarifa ya habari ni lazima kwa kila chombo vha habari mainstream (Radio, TV)
 
Habari za jioni wakuu?

Kufungua kituo cha redio, ni vitu gani vinahitajika, na kinaweza kugharimu kiasi gani?
Uje nikufanyia Business Proposal and cost analysis laa sivyo uziwaze usivyovijua

"Usione vyaelea...."
 
Siku hizi wanawekeza kweli. Kuna online media zinasajili watangazaji kutokea electronic media.
Ni kweli, lakin uzuri wa Online media chance za kufanikiwa ni kubwa, pia hazina mambo mengi sana kama hizi za live, kama una 50M bank wekeza kwenye online media, ndani ya mwaka utaanza kupata faida ya kuanzia, kina swahili times wapo vizuri unaweza jifunza kwao
 
Kwa hiyo ukimchangia kama 150,000/= inaweza kumtosha kabisa kwa kuanzia?
Kwa uzoefu wangu ili upate Vijana wa hiyo tasnia ebu jilink na vyuo vya uandishi wa Habari.
Hata hiyo 150 Vijana wanachukua tu nilifanya kazi media flan nikawa nalipwa hiyo pesa.
 
Yaani unatumia Tsh 50,000,000+ ili wenzio ambao hata huwajui wasikilize bure redio na wengine labda kutangaza biashara zao kwa malipo kiduchu huku ukiajiri wataalam/watangazaji? Hii kitu haina utofauti sana na kubet.
Kuna kanisa moja lilifungwa hapa kwetu lilikuwa na kituo chake cha redio wakauza vifaa vyote kwa $20,000 (obo) kasoro jengo tu. Nilitaka kuvununua kwa $17,500 lakini nilipoulizia hapa kuhuse faida za biashara hiyo nikakatishwa tamaa
 
Habari za jioni wakuu?

Kufungua kituo cha redio, ni vitu gani vinahitajika, na kinaweza kugharimu kiasi gani?
Endapo gharama ikiwa kubwa ni lazma iwe kubwa but unaweza ukaanza online media ambapo unanunua u tube channel yny subscribes wengi then unaanzia huko huku ukipima upepo wa radio.
 
Ahsante mkuu kwa kuja! Last seen yako ilikuwa inaonesha ni 2022 nikajua hata nikikukwoti hutakuja lakini hatimaye umekuja kutoa ufafanuzi.
Kazi nyingi kuanzisha maradio ya watu. Nilipoonq thread nikaona mtu kanitaja ndo kuanza kutafuta "pasuwedi" mwisho nikaweza kuingia.

Kwasasa tunakampuni kubwa inadeql na haya mambo:-

1. Ushauri wa Awali wa Hatua za kuanzisha radio.
2. Kuandaa nyaraka za maombi ya leseni.
3. Tuna duka la mitambo ya radio. Sasa hauhitaji kuagiza Italy.
4. Tunafanya design za radio na tunakazi nyingi za mfano.
5. Tunafunga mitambo (installations)
6. Tunafanya matengenezo (Repair and Maintanance).
Huduma zote zinazohusu radio na TV utazipata kwetu.

Karibuni sana.
 
Habari za jioni wakuu?

Kufungua kituo cha redio, ni vitu gani vinahitajika, na kinaweza kugharimu kiasi gani
Mkuu naomba mawasiliano yako whatsapp nikutumie muongozo 100% kuanzia A-Z.

Tumewezesha zaidi ya radio 20 kuanzishwa hapa Tanzania since 2012.

Asante
 
Kuna kanisa moja lilifungwa hapa kwetu lilikuwa na kituo chake cha redio wakauza vifaa vyote kwa $20,000 (obo) kasoro jengo tu. Nilitaka kuvununua kwa 417,500 lakini nilipoulizia hapa kuhuse faida za biashara hiyo nikakatishwa tamaa
Kwamba walikuwa wakiuza vifaa vyote kwa bei gani na wewe ulitaka kuvinunua kwa bei gani? Sijakuelewa.
 
Kwamba walikuwa wakiuza vifaa vyote kwa bei gani na wewe ulitaka kuvinunua kwa bei gani? Sijakuelewa.
Nilitaka kununua kwa $17,500 (ile alama ya $ haikuonekana, badala yake ikajitokeza kama 4 kwenye keyboards za kimarekani). Bei ilikuwa ni $20,000 (or Best offer). Havikupata mnunuzi kwa karibu wiki tatu na nilikuwa nataka kutoa offer ya $17,500.
 
Nilishawahi kufungua kituo cha radio and the day nikamuuzia mwamposa kama upo serious njoo pm nakupa info zote na kuku conect na wahusika kuanzia vifaa mafundi, usajili nakila kitu we ni kusubir tu uisikilize uje serious sio unakuja kuulizia tu kama kuuliza tuu endelea kusubili wahusika wanakuja watakujibu
Pipa kama pipa
Chai
 
Kuanzisha ni jambo rahisi, kuendesha huwa ndio kugumu.
Kwa wastani wa shilingi 50m inatosha kuanzisha kwa kufanya haya;
1. Kupata vibali
2. Kununua/kukodisha masafa
3. Kufunga mitambo ya kurusha matangazo umbali usiopungua km 100 pande zote (Radius distance), yaani ukiweka transmition tower ya urefu wa mita 10 pale Mwenge kwenye jengo lenye urefu usiopungua ghorofa 10, basi jiji la Dar lote na wilaya za jirani na Dar ikiwemo Zanzibar watasikia matangazo yako.
4. Kununua na kufunga vifaa muhimu vya studio ya vyumba viwili. (Hii ikijumuisha Computer, Sound system, standby generator, office furniture.

Kimbembe huwa ni gharama za uendeshaji. Kwa mfano, kwa kuanzia inabidi uwe na haya.
1. Wafanyakazi wa kudumu sita (watangazaji wawili, Fundi mitambo wawili, wasaidizi wa kazi zisizo rasmi wawili), hapo jiandae kuwalipa wastani wa kiasi cha shilingi laki tano kila mmoja kila mwezi (jumla 3m kwa mwezi)

2. Utility bill charges za kuendesha studio za kila siku (Kodi ya pango, Umeme, mafuta, simu, internet, maji, Posho, chakula, ulinzi) wastani ni 1m kwa mwezi.

3. Gharama zingine muhimu (Kodi za serikali, matengenezo ya vifaa, insurance, malipo/posho ya kuwalipa freelancer journalists, Promotion), hapo ni wastani wa shilingi 1m kila mwezi.
 
Back
Top Bottom