Kuanzisha ni jambo rahisi, kuendesha huwa ndio kugumu.
Kwa wastani wa shilingi 50m inatosha kuanzisha kwa kufanya haya;
1. Kupata vibali
2. Kununua/kukodisha masafa
3. Kufunga mitambo ya kurusha matangazo umbali usiopungua km 100 pande zote (Radius distance), yaani ukiweka transmition tower ya urefu wa mita 10 pale Mwenge kwenye jengo lenye urefu usiopungua ghorofa 10, basi jiji la Dar lote na wilaya za jirani na Dar ikiwemo Zanzibar watasikia matangazo yako.
4. Kununua na kufunga vifaa muhimu vya studio ya vyumba viwili. (Hii ikijumuisha Computer, Sound system, standby generator, office furniture.
Kimbembe huwa ni gharama za uendeshaji. Kwa mfano, kwa kuanzia inabidi uwe na haya.
1. Wafanyakazi wa kudumu sita (watangazaji wawili, Fundi mitambo wawili, wasaidizi wa kazi zisizo rasmi wawili), hapo jiandae kuwalipa wastani wa kiasi cha shilingi laki tano kila mmoja kila mwezi (jumla 3m kwa mwezi)
2. Utility bill charges za kuendesha studio za kila siku (Kodi ya pango, Umeme, mafuta, simu, internet, maji, Posho, chakula, ulinzi) wastani ni 1m kwa mwezi.
3. Gharama zingine muhimu (Kodi za serikali, matengenezo ya vifaa, insurance, malipo/posho ya kuwalipa freelancer journalists, Promotion), hapo ni wastani wa shilingi 1m kila mwezi.