Kufungua trust fund kuhifadhi ardhi ya watoto

Kufungua trust fund kuhifadhi ardhi ya watoto

TOMNOTKAT

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2013
Posts
836
Reaction score
1,080
Wasomi naomba ushauri. Mimi siku zangu hapa duniani zinahesabika, hivyo nimeanza kuandaa mirathi. Ninakapori kangu kadogo nataka kukahifadhi kwenye TRUST FUND kwa ajili ya watoto wangu waliochini ya miaka mitano.

Kapori hako nimekanunua mwenyewe na kako kwenye jina langu. Nimeshapima nusu, ila sijamaliza, Hivyo hati hazijatoka ila ninamhutasari wa kijiji na nyaraka za manunuo toka kwa aliyeniuzia.

Sasa kwavile baba watoto ni bado kijana, najua nikishakufa ataoa upya, na anaweza pata watoto wengine. Hivyo nataka kulinda haki ya wanangu, wasije gawanywa shamba na hao watoto wengine.

Ningependa mume wangu awe TRUSTEE na aendelee kuwa na haki ya kulitumia shamba kwa kilimo kama tufanyavyo sasa, ila akijua hilo shamba ni mali ya watoto.

Naomba ushauri jinsi gani na hatua zakupitia kufungua hiyo TRUST FUND.

Pamoja na muda na garama zake....

Natanguliza shukurani zangu.
 
Umeonyesha kutomuamini mume sidhani kama utaungwa mkono....si waislamu tu hata wakristo hapo wanaweza nyamaza
 
Sasa ya waisilamu na wakiristo yanatokea wapi? Mie nahitaji ushauri wa kisheria nilinde watoto, sihitaji kuungwa mkono na yeyote.
 
consult lawyer yeyote...pole sana kwa unayopitia.
 
kesho asubui piga hodi ofsi yoyote ya mwanasheria, amaweza kukusaidia au kukuelekeza kwa mwanasheria mwingine aliye competent upande huo.
 
Kama kweli upo serious hili sio jambo la kuongelea hapa.

Formation of trust itategemea na aina ya trust unayoitaka.

Zipo zinazofanya kazi baada ya wewe kufariki, zipo zinazofanya kazi ukiwa unaishi na zaidi
 
Kama kweli upo serious hili sio jambo la kuongelea hapa.

Formation of trust itategemea na aina ya trust unayoitaka.

Zipo zinazofanya kazi baada ya wewe kufariki, zipo zinazofanya kazi ukiwa unaishi na zaidi

Tuongee hapa hapa ili na Ss wengine tuelike !
 
Back
Top Bottom