Wasomi naomba ushauri. Mimi siku zangu hapa duniani zinahesabika, hivyo nimeanza kuandaa mirathi. Ninakapori kangu kadogo nataka kukahifadhi kwenye TRUST FUND kwa ajili ya watoto wangu waliochini ya miaka mitano.
Kapori hako nimekanunua mwenyewe na kako kwenye jina langu. Nimeshapima nusu, ila sijamaliza, Hivyo hati hazijatoka ila ninamhutasari wa kijiji na nyaraka za manunuo toka kwa aliyeniuzia.
Sasa kwavile baba watoto ni bado kijana, najua nikishakufa ataoa upya, na anaweza pata watoto wengine. Hivyo nataka kulinda haki ya wanangu, wasije gawanywa shamba na hao watoto wengine.
Ningependa mume wangu awe TRUSTEE na aendelee kuwa na haki ya kulitumia shamba kwa kilimo kama tufanyavyo sasa, ila akijua hilo shamba ni mali ya watoto.
Naomba ushauri jinsi gani na hatua zakupitia kufungua hiyo TRUST FUND.
Pamoja na muda na garama zake....
Natanguliza shukurani zangu.