Kufungulia Nchi? Kurudi Kujivunia Umaskini?

Samia Gang Vs Magufuli Gang...we've come this far!
 
Mtulivu.
Ana hekima
Busara
Hana maneno makali
Anathamini utu wa wengine
Anatengeneza urafiki na kila mtu.

HAYA YALIMSHINDA JOHN, HATA ALIPOELEKEZWA HAKUKUBALI
 
M
1. Huogopi kuitwa MATAGA?

2. Wewe ni Sukuma Gang!

3. Utaambiwa unamchukia Mama 🤣.

4. Usisahau kuwa huyu Mama hakosolewi! Ukithubutu tu, utaambiwa unamtaka Magufuli ila bahati mbaya harudi tena!
Mzee mwenzangu baada ya miaka zaidi ya ishirini ya kuitwa Kila majina kwenye mitandao sidhani kama hawa wanaweza kunishtua.... Ila tunao hawa.
 
Jiwe aliamua kuwakorofisha majirani zetu na kuamua kuishi kama tupo kisiwani maana majirani zetu nao waliona isiwe tabu wakatufungia vioo
Ni ujirani gani wa chetu ni chao na chao ni chao?
 
Usingetolea mfano wa 邓小平 kwa sababu haviendani na utaratibu wa nchi yetu kiuchumi.acheni kuwa mnatolea mlinganyo wa mataifa yenye njia tofauti za uchumi na uthubutu.
 
1. Huogopi kuitwa MATAGA?

2. Wewe ni Sukuma Gang!

3. Utaambiwa unamchukia Mama [emoji1787].

4. Usisahau kuwa huyu Mama hakosolewi! Ukithubutu tu, utaambiwa unamtaka Magufuli ila bahati mbaya harudi tena!
Ukikosoa tu utashambuliwa na makundi makubwa yakiwemo MATAPA, akina bwa shee, wanawake (wale wa gruuu), baadhi ya wanadini na upande wa pili ukivuka maji.
 
Umemaliza kila kitu. Asante.
 
Unasema ukweli mtupu hii nchi ilitolewa kabisa katika utaratibu tulijitenga na kila nchi iliyotuzunguka na ndani nchi ilikuwa ikiongozwa kwa amri za magufuli hakuna sheria wala katiba tunashuku mungu kututowa katika madhila yale.
 
Mzee wangu Mwanakijiji leo unahasira, ni Sawa kabisa kwani hata mimi mjukuu wako ninazo pia tena pima, zimejaa pomoni, ile nuru imezima katikati ya tafrija, maandishi yakambeba mama, akakiri kuwa na jinsi ya kike lakini yeye ndiye rais na salam mpya kutufundisha. HEWALA SI UTUMWA.

Unayo haki ya kukasirika, nchi haiendeswi kwa huruma, hii si familia bali nchi. Tumepiga U-TURN bahati mbaya hatujui sababu.

Naumia sana kuona nchi yangu ikirudi hatua 10 nyuma na bila kujali watu wanapiga makofi ya hongera.

WACHA TUISHI, NDIO TUISHI KWA KUWA KUISHI NI KAZI NGUMU KULIKO KUFA.
 
Kwani lini Tz ilikua tajiri? na lini ilifilisika?
 
Kwa kifupi mama anairudisha nchi nyuma, period
 
Watanzania tunataka nini?
Siku ukiielewa kauli hii ndio utajua ni nini hawa watu walitaka.

...............Safi sana Mama kasema mwendo ni ule ule, lazima waisome namba.

Hapo utajiuliza, ina maana kazi ya Rais ni kusomesha namba watu, kuumiza watu, kutaabisha watu au kuteka na kuua watu.

Then, utakuja kugundua kuna watu ambao furaha yao huwa ni kuona watu wanaumizwa, kuuawa na kutaabishwa na bahati nzuri walifanikiwa kuwa na mtu wao Ikulu miaka 5 iliyopita na mpaka sasa hawaamini kilichotokea.

Ukisikia ile stori ya malaika kumtokea mtu mmoja na kumwambia aombe kitu kimoja ambacho, akipewa jirani yake atapata mara mbili. Huyo mtu akaamua kuomba atolewe jicho moja, ili jirani yake atolewe macho yote awe kipofu ndio utawaelewa vizuri watu wa aina hii.

Ni watu ambao siku zote wanafurahia makatili kama kina Sabaya, Makonda, Chalamila. Huwezi kuwakuta wanamfagilia kiongozi kama Antony Mtaka au Anna Mgwira.

Wao wako tayari kuvumilia hata mateso au sheria kandamizi ili mradi tu hizo sheria zinawaumiza watu wengine pia.

Na binafsi huwa naona ndivyo walivyo kimaumbile, hawawezi kuwa tofauti hata kama wakijifanya watu wa dini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…