Katika dunia hii ya globalization huwezi kuifungia nchi na wala huwezi kuifungulia nchi na kumeza kila kitu kama dodoki! Kwa hiyo unachofanya ni kuiunganisha nchi na dunia in away ya win win situation.
Sasa, naona kuna upotoshaji wa makusudi kuhusu notion ya Rais Samia kuhusu "Kufungua nchi!" Kwa makusudi kabisa wapotoshaji hawajadili mantiki bali ajenda ovu. Rais amekuwa wazi ana maanisha nini. Kwamba lengo ni kuweka mazingira mazuri ya kibiashara yanayotabirika. Ni pamoja na mfumo wa haki wa kodi, usimamizi na utekelezaji wa sheria na sera ya Uwekezaji na kuondoa urasimu. Kwa kifupi ni kuboresha Mpango wa Blue print.
Utekelezaji wa miradi mikubwa unahitaji pesa nyingi ambazo hazitaathiri shughuli nyingine za kiserikali, kama haki ya kuongeza mishahara watumishi wa umma, dawa hospitalini, elimu bure, mikopo elimu ya juu, ajira na operesheni nyingine. Sasa huwezi kufanya yote hayo bila kuwa na wigo mpana wa wawekezaji wa walipa kodi. Ukiendesha miradi kwa kukopa utaizamisha nchi katika dimbwi la deni lisilolipika! Sasa faida ya globalization ukifungua nchi ; ni kuruhusu mitaji ya uchumi na biashara kumiminika.
Utazalisha kwenye viwanda na ni rahisi pia kufanya Mapinduzi makubwa ya kilimo. Binafsi natamani tupate wawekezaji wakubwa katika sekta ya kilimo ili tufanye Mapinduzi ya Kilimo. Tuna tatizo kubwa la umasikini wa kurithi (Generational poverty), kwa sababu asilimia 70 ya wakulima ni sawa na 'toto lililodumaa!' Kwa hiyo hujikuta masikini wanazaa masikini.
SULUHU: Ni kufungua nchi waje wawekezaji wakubwa katika sekta mbalimbali hasa kilimo, ili tufanye Mapinduzi ya Kilimo, tukuze viwanda, kodi, ajira, uchumi, biashara, tuondoe umasikini wa KURITHI, tu export na kuongeza pato la mtu.
MSIMAMO: Naamini Serikali itafanya haya katika mazingira ya win win situation. Ndicho ninachojua katika focus ya Rais wetu Mama Samia. Tumuunge mkono na tumpe muda.
SISI NI TAIFA.