Kufungulia Nchi? Kurudi Kujivunia Umaskini?

Kufungulia Nchi? Kurudi Kujivunia Umaskini?

Namuomba tu "akerwe" na umasikini wa watanzania walio wengi. Pesa za umma zielekezwe zaidi kuinua hali za maisha ya watu masikini hasa kwenye elimu na mazingira ya kutolea elimu kwa ujumla. Hizi zawadi za mabenzi (kama kweli ni zawadi na sio replacement) ni non starter!
Ubarikiwe mkuu, na zaidi Sana tuendelee kumwombea na kuiombea nchi yetu, Mungu akiwako upande wetu, Chini ya Raisi Samia, tunaweza kila kitu
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Kumbuka hayo maneno aliyasemea wapi.

Maana yake ililenga hadhira hiyo. Bila shaka baada ya kunogewa aliyoyasikia yakisemwa mahala hapo.

Sasa katika kunogewa huko, asije akajisahau kwamba kazi yake kubwa ni kuwapambania waTanzania na siyo wahusika wa mkutano huo pekee.

Picha ninayoiona kama atatimiza dhamira hiyo ya "kufungua nchi", tutaanza kuona maluweluwe mengi na hadaa chungu nzima huku jamaa wakibeba tunavyotegemea vitunyanyue sisi.
Approach tunayokwenda nayo yaitaji umakini mkubwa na abnormal strategies....lkn kwa mfumo na mazingira yalipo ualakn ni mwingi

Tuzidi tu kuiombea nchi hii
 
Inawezekana wakati mama anaenda kufungulia nchi anaweza kufungulia hizi hisia za kutukuza na kukumbushana juu ya kile kinachoitwa umaskini wetu?

Tunatakiwa kutokujaribu au kuthubutu kufanya makubwa kwa sababu sisi ni masikini? Ndio mwanzo wa kuanza kuombaomba tena...maskini wa fikra hatajiriki na hawezi kutoka kwenye umaskini ambao anaamini unamnufaisha. Inanikumbusha kile kisa cha"Mtumwa Mpendwa" aliyefurahia kupendelewa na bwana wake hadi siku ile yule bwana alipokufa.

Mama ana kazi na kibarua kigumu..maana hata kufoka hawezi na akiwabwatukia watalia hawa kama watoto waliodekezwa, wakadeka, na kudekeka..mtaa mzima utawasikia...na hawanyamazi hadi wapewe "fanta"
Lini tuliwahi kuacha kuomba ? Hebu rejea deni la taifa ukiwa unajibu hili, lini tulifanya hao unayoita makubwa na lini hatukufanya? Mataga bwana . ..
 
Lini tuliwahi kuacha kuomba ? Hebu rejea deni la taifa ukiwa unajibu hili, lini tulifanya hao unayoita makubwa na lini hatukufanya? Mataga bwana . ..
Kuomba kweli kabisa hatujawahi Acha, Ila ni vema kupunguza, na hata hivyo mkuu, kukua Kwa deni ni namna tulivyokopa na sio tulivyooomba!

Kwa hiyo, kukopa ni sehemu ya kutaka kuacha kuombaomba, na hili huwa zuri zaidi Ikiwa Miradi inayoombewa mkopo iwe ni Miradi itayoleta uzalishaji mkubwa, Jambo lingine, usimamizi mzuri na sio ufujaji
 
China chini ya Deng Xiaoping alifungulia nchi, huku ndiko mama anavyomaanisha.
Kuondoa vikwazo vya kipuuzi vya kuleta investment na kuondoa urasimu kwenye kuanzisha business.

Sasa kufungulia nchi na kuomba mbona haviendani naona mko busy kutwist maneno yake na kuyafanyia spinning ili kupotosha!

So far so good, Nchi inaenda vizuri vhini ya mama Samia, kafanya kazi nzuri sana kwenye siku zake 50 za kushika usukani, aneonyesha njia nzuri mno
Hawajui kanuni hii: Y = C + I + G + NE.
Wako busy kupotosha wasiojua kanuni hii.
 
Inawezekana wakati mama anaenda kufungulia nchi anaweza kufungulia hizi hisia za kutukuza na kukumbushana juu ya kile kinachoitwa umaskini wetu?

Tunatakiwa kutokujaribu au kuthubutu kufanya makubwa kwa sababu sisi ni masikini? Ndio mwanzo wa kuanza kuombaomba tena...maskini wa fikra hatajiriki na hawezi kutoka kwenye umaskini ambao anaamini unamnufaisha. Inanikumbusha kile kisa cha"Mtumwa Mpendwa" aliyefurahia kupendelewa na bwana wake hadi siku ile yule bwana alipokufa.

Mama ana kazi na kibarua kigumu..maana hata kufoka hawezi na akiwabwatukia watalia hawa kama watoto waliodekezwa, wakadeka, na kudekeka..mtaa mzima utawasikia...na hawanyamazi hadi wapewe "fanta"
Mimi huwa namsikiliza vizuri sana mama anapokuwa anaongea, hadi kuna wakati mwingine huwa narekodi speech zake anapokuwa anaongea na baadaye kurudia kumsikiliza tena. Kuna siku katika speech yake amewahi kusema "hatuwezi kurudi tena kule tulikotoka........"

Si ujanua tena mtu wa kwanza kubahatika kuitwa 'mama" na watu zaidi ya million 60, na possibly hadi wazazi wake waliomzaa nao pia wanaweza kuwa wanamwita hivyo hivyo
 
Kwanza unalinganisha nchi tofauti kabisa China ya Xiaping na Tanzania ya Samia, hilo ni kosa lakwanza linaloonyesha hujui mlinganisho hata kabla ya kuzungumzia mengine.
China ya Xiaoping ilikuwa tayari. Hawakufungulia tu holela kila takataka zije kuondoa hicho walichokuwa tayari wamekiweka sawa kiwaletee manufa.

Tanzania ya Samia, hivi ni lini imefungwa, na imefungwa vipi? Wawekezaji walizuwiwa kuja kuwekeza; au nati zilikazwa ili wakija hapa wasitufanye kama shamba la bibi?
Nitaonekana kama shabiki wa Magufuli kwenye mambo haya; lakini sikuwahi kupenda yale maovu yake.

Mama asitupeleke tena kujinadi na kunadi mali za taifa hili kwa hasara ya wananchi wake. Ni wakati angalau ahimize, waTanzania wachangamkie fursa nyingi tu zilizopo hapa na aweke mifumo ya kuwawezesha kuliendeleza taifa hili, na siyo kuonyesha kana kwamba maendeleo ya nchi hii bila ya wawekezaji toka nje haiwezi kuendelea. Huku ni kujidharau kusikofaa kabisa.

Na usije ukanirukia na kusema sitaki wawekezaji wa nje. Waje kwa wingi, lakini kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania na sio kuja kupora mali zao.

Wanaowezesha wawekezaji wawe wa nje au ndani kupora nchi ni viongozi wa serikali wenye mipango ya dili na ufisadi, period. Ndio wanaoandaa mikataba yenye vipengele vya kujinufaisha na familia na marafiki zao.

Hakuna mwekezaji anayeweza kuliibia taifa kama viongozi wa nchi hawataki. Tangu turuhusu uwekezaji viongozi wetu wamekuwa wakiendekeza tamaa na kuchangamkia wawekezaji wezi. Mwekezaji muadilifu akikataa kukubaliana na mipango ya kiwizi hunyimwa fursa.
 
Rais mstaafu wa JMT, mzee Mwinyi alifungulia mpaka na majongoo yakaingia, sasa mama inabidi awe makini.
 
Jiwe aliamua kuwakorofisha majirani zetu na kuamua kuishi kama tupo kisiwani maana majirani zetu nao waliona isiwe tabu wakatufungia vioo
we mzee uko around 50+..Kwa jinsi ulivyo na chuki na huyo jiwe kuna uwezekano ktk utawala wake kuna kitu kilikukumba siyo bure asee..vyeti feki nini?

Ukiondoa Kenya hebu taja nchi zingine majirani ambazo Tz ilikuwa nazo na migogoro serious
 
Kwahiyo Kenya unaidharau
 
Kwahiyo Kenya unaidharau
Sidharau Ila Unakuza sn tatizo Mzee wangu..kwa umri wako unajisahaulisha kwamba hao Kenya tulishafungiana Hadi mipaka enzi hizo za mwalimu,Ila wewe unakomaa na jiwe Tu[emoji1787][emoji119]

Sisi wengine tulisoma vitabuni maana hatukuzaliwa bado enzi hizo lkn tunakumbuka mbn
Anyway sipo hapa kufanya argument mkuu ni maoni yangu tu
 
Tatizo letu kama taifa linaanzia mbali sana tofauti na wanasiasa wanavyotuaminisha kwa sasa. Fikiria huyu mama alikuwa msaidizi wa hayati lakini baada ya kupokea uongozi ndani ya siku 50 tu anaonekana kimatendo alikuwa hakubaliana na jpm walau hata kwa asilimia 50 tu. Huwa najiuliza ingetokea magufuli amekuwa mahtuti halafu mama akashika nchi kwa kipindi cha mpito walau miezi 3 tu,angekuwa anafanya anayoyafanya hivi sasa au angetekeleza matakwa ya jpm?
Tunakosa dira ya taifa kwa sababu wanasiasa wanataka kupendwa kwanza kuliko kufikiria maslahi mapana ya taifa. Hii mark time tunayopiga miaka nenda rudi haitakaa iishe sababu kila mtu anatengeneza legacy yake.
Swali la kizushi: kwani mtu akichaguliwa kuwa msaidizi na akashindwa kuridhika na utendaji wa boss wake haruhusiwi kujiuzuru ili kuonyesha uwajibikaji?

Ijue “realpolitik” ya Tanzania. Chini ya chama tawala, wanasiasa wanajua lengo hasa la siasa ni kushika madaraka na kuzifika fursa kuu za ulaji wa rasilimali ya taifa KIRAHISI. Inaitwa kleptocracy. Ndugu zetu wa Afrika ya Kusini wanaita “State Capture”. Nje ya hapo ni kujipa mahangaiko na hata kuhatarisha hatma yako.

Kinachoitwa “kulitumikia taifa au uzalendo” wao wote wanajua ni porojo (hogwash) la kuwazuga wananchi wasioelewa mazingira yao waendelee kukushangilia na kukuimbia mapambio ya sifa na utukufu! Hata JPM alilijua hilo na kulitumia vizuri sana.

Kwa hiyo, mtu mwenye matamanio (ambition) ya kufika mbali katika mafanikio, kamwe hawezi kufanya “ujinga” wa kuachia madaraka kwa hiyari eti kuonyesha uwajibikaji na kujijengea “heshima”. Hiyo itakuwa “naivety” ya hali ya juu sana. Unamuachia fisi bucha? Mama akaamua kukaa tuli (biding her time) akijua kuna siku mbio za sakafuni zitaishia ukingoni. NA IKATOKEA.

Sasa ni zamu yake. Bado tunasubiri kuona gia kubwa atakayoondokea nayo bila kusahau kuwa “CCM ni ile ile”.

Hivi sasa huko Afrika ya Kusini, Rais mstaafu Zuma na ANC yake wanachemshwa mahakamani kuhusu alivyotumia madaraka ya uRais kuteka taasisi za dola na kuzitumia kufanya ufisadi mkubwa wa rasilimali za nchi. Kwetu sisi “state capture” ni jadi ya CCM. Hakuna anayesumbuka tena na hilo. Tulishanyoosha mkono juu siku nyingi. Hata Dr. Slaa wa Mwembechai siku hizi ana vipaumbele vinginee!
 
Sidharau Ila Unakuza sn tatizo Mzee wangu..kwa umri wako unajisahaulisha kwamba hao Kenya tulishafungiana Hadi mipaka enzi hizo za mwalimu,Ila wewe unakomaa na jiwe Tu[emoji1787][emoji119]

Sisi wengine tulisoma vitabuni maana hatukuzaliwa bado enzi hizo lkn tunakumbuka mbn
Anyway sipo hapa kufanya argument mkuu ni maoni yangu tu
Nakubaliana na wewe sana ila kila jambo lina umuhimu wake.

Mimi ni mtanzania lkn muda mwingi shughuli zangu nazifanyia Kenya .
Hivyo basi kitendo cha kuwa na mahusiano yasiyo mazuri kilinikwamisha sana kishughuli zangu.

Ninapo lalamika namaanisha jambo ambalo sitokaa nilisahau.
 
Kuomba kweli kabisa hatujawahi Acha, Ila ni vema kupunguza, na hata hivyo mkuu, kukua Kwa deni ni namna tulivyokopa na sio tulivyooomba!

Kwa hiyo, kukopa ni sehemu ya kutaka kuacha kuombaomba, na hili huwa zuri zaidi Ikiwa Miradi inayoombewa mkopo iwe ni Miradi itayoleta uzalishaji mkubwa, Jambo lingine, usimamizi mzuri na sio ufujaji
Ukitaka kujua Magu alivyokuwa gwiji la kuomba, uthibitisho ni uwepo wa COVID-19 bungeni kinyume na katiba kabisa.

Hii yote ni kuvizia misaada kutokana na masharti ya jumuiya ya madola.

Magu alikuwa omba omba mnafiki ambaye alikuwa anaomba kutoka mpaka vinchi masikini kama Morocco.

Lakini kutokana na uporaji wa demokrasia na mauaji ya watu wasio na hatia, akijikuta wahisani wengi wanajitoa au kupunguza misaada. Akaanza kuendesha nchi kwa kupora watu Pesa zao na kukopa mikopo ya kibiashara.

Ndani ya miaka 5 kakopa kuliko Kikwete alivyokopa miaka yote 10.
 
Labda tupate tafsiri pana ya kufungulia nchi wewe umeielewaje.
Kwani uwanja wa mpira wa kwa mzee beni wanaposema wanafungulia uwanja zikiwa zimebaki dakika 10 mpira kuwekwa kwapani wanakuwa wanamaana gani?
 
Wanaowezesha wawekezaji wawe wa nje au ndani kupora nchi ni viongozi wa serikali wenye mipango ya dili na ufisadi, period. Ndio wanaoandaa mikataba yenye vipengele vya kujinufaisha na familia na marafiki zao.

Hakuna mwekezaji anayeweza kuliibia taifa kama viongozi wa nchi hawataki. Tangu turuhusu uwekezaji viongozi wetu wamekuwa wakiendekeza tamaa na kuchangamkia wawekezaji wezi. Mwekezaji muadilifu akikataa kukubaliana na mipango ya kiwizi hunyimwa fursa.
Akina Acacia walikuwa hapa, hata ikawa wanatuonea huruma wao wenyewe jinsi tulivyokuwa tukionewa!
 
Back
Top Bottom