Wenzake wakina nani? Nao pia walifia ofisini ndani ya miaka 5+ ya utawala wao?? Acha blah blah za kuandika vitu bila ushahidi au mantiki yeyote, wataje hao walio acha reli toka Tanzania mpaka Zambia na hayo mengine ili tuwajadili. Hayati muheshimiwa Jiwe, alikuwa na mapungufu kemkem kama binadamu yeyote yule, ila ninyi wapinzani wake, shutuma zenu nyingi ni za kutengeneza, uongo wa dhahiri, hamna ushahidi na mnaongeza chumvi mno wakati mwingine. Kitu ambacho hamtaweza kumnyang’anya muheshimiwa, marehemu Magufuli ni uthubutu wake na ‘visheni’ yake kuwa Tanzania ilipasa kwanza kufunguliwa ndani kabla ya kufunguliwa kiholela nje ili watanzania wanufaike na Tanzania badala ya kubaki manamba, wafagiaji na waosha vyombo wa wageni. Kama ambavyo muheshimiwa Jiwe haku maliza muda wake, hii ngoma bado! Kumbuka kuna uchaguzi 2025....au kama dada Samia ana ubavu, avunje serikali, tufanye uchaguzi sasa ili apate “mandate” ya kufanya vurugu anazotaka. Vinginevyo, hii kitu inaonyesha kama kuna faulo...