BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
Kwani huyo aliyekuwa akifoka kutwa kucha alifanya lipi la maana pamoja na kufoka kwake, kufanya udhalimu na dhuluma za kutisha?
Inawezekana wakati mama anaenda kufungulia nchi anaweza kufungulia hizi hisia za kutukuza na kukumbushana juu ya kile kinachoitwa umaskini wetu? Tunatakiwa kutokujaribu au kuthubutu kufanya makubwa kwa sababu sisi ni masikini? Ndio mwanzo wa kuanza kuombaomba tena...maskini wa fikra hatajiriki na hawezi kutoka kwenye umaskini ambao anaamini unamnufaisha. Inanikumbusha kile kisa cha"Mtumwa Mpendwa" aliyefurahia kupendelewa na bwana wake hadi siku ile yule bwana alipokufa...
Mama ana kazi na kibarua kigumu..maana hata kufoka hawezi na akiwabwatukia watalia hawa kama watoto waliodekezwa, wakadeka, na kudekeka..mtaa mzima utawasikia...na hawanyamazi hadi wapewe "fanta"