Humu JF kuna vichwa bwana...!! Naona hadi mtoa post kakimbilia ndani, chumbani na kujificha kabatini..!!Tukiacha ushabiki awamu ya tano nchi ilikuwa imejifunga na hali ya mzunguko wa hela ilikuwa ngumu kuanzia kwa wafanyabiashara mpaka wafanyakazi.... ushahidi ni pale JPM mwenyewe kila meimosi alipogoma kuongeza mishahara na kusema mpaka miradi iishe, upande mwingine makampuni kadhaa yalifunga biashara na confidence ya uwekezaji ikawa imeshuka kabisa.. Serikali awamu ya tano ilitoa watu kazini maelfu kwa kisingizio cha vyeti feki na haikuajili kureplace hao waliotoka, Serikali iliacha kuajili maelfu kwa malaki wakabaki mtaani hawana kazi...
Mbinu zilizotumika awamu ya tano kwa kuwataka watu wafunge mikanda ndio maendeleo yaje, ni mbinu za kizamani, karne ya sasa modal za uchumi ni kuleta maendeleo kwa pamoja kwa maana ya maisha ya watu na vitu kwa pamoja hiyo ndio akili.... na ndio tunaposema nchi imefunguka..
Uchumi wa Tanzania ni mdogo, uzarishaji wa Tanzania ni mdogo, watanzania ni masikini wa akili na kipato huu ndio ukweli bila propaganda..Kuifungua nchi ni kufanya wepesi wa mitaji kuja na watanzania kuingia kwenye mzunguko, watu kuja watanzania kupata uzoefu na exposure, investments kubwa kufanyika maelfu na malaki wapate ajira serikali iingize kipato...
Mwisho kabisa, nitajie awamu moja toka uhuru ambayo haijawahi kusaidiwa, kukopeshwa au kupewa msaada...
Jamani mjibuni huyu anauliza kama kuna awamu yoyote toka uhuru hadi sasa haijawi kukopa au kuomba msaada..!! Ipo?