Kufungulia Nchi? Kurudi Kujivunia Umaskini?

Hivi ni wakati gani nchi hii iliacha kuomba omba? Wamekuj marais kadhaa hapa wakiwemo wa Misri,Uturuki,China, Waziri Mkuu wa India n.k wote hawa kwa nyakati hatukuwaacha salama lakini sote tunakumbuka mkopo wa benki WB ulivyotuenyesha,ni vyema muwache unafiki kama huyo mama hamumpendi semeni sababu zenu wazi wazi kuliko kusingizia mambo ambayo hatukuwahi kuyaacha halafu leo mseme anataka kuturudisha!
Tuliomba hadi kwa nchi kama Namibia halafu mtu anamsifia magu
 
Tatizo letu kama taifa linaanzia mbali sana tofauti na wanasiasa wanavyotuaminisha kwa sasa. Fikiria huyu mama alikuwa msaidizi wa hayati lakini baada ya kupokea uongozi ndani ya siku 50 tu anaonekana kimatendo alikuwa hakubaliana na jpm walau hata kwa asilimia 50 tu. Huwa najiuliza ingetokea magufuli amekuwa mahtuti halafu mama akashika nchi kwa kipindi cha mpito walau miezi 3 tu,angekuwa anafanya anayoyafanya hivi sasa au angetekeleza matakwa ya jpm?
Tunakosa dira ya taifa kwa sababu wanasiasa wanataka kupendwa kwanza kuliko kufikiria maslahi mapana ya taifa. Hii mark time tunayopiga miaka nenda rudi haitakaa iishe sababu kila mtu anatengeneza legacy yake.
Swali la kizushi: kwani mtu akichaguliwa kuwa msaidizi na akashindwa kuridhika na utendaji wa boss wake haruhusiwi kujiuzuru ili kuonyesha uwajibikaji?
 
Inawezekana wakati mama anaenda kufungulia nchi anaweza kufungulia hizi hisia za kutukuza na kukumbushana juu ya kile kinachoitwa umaskini wetu? Tunatakiwa kutokujaribu au kuthubutu kufanya makubwa kwa sababu sisi ni masikini? Ndio mwanzo wa kuanza kuombaomba tena...maskini wa fikra hatajiriki na hawezi kutoka kwenye umaskini ambao anaamini unamnufaisha. Inanikumbusha kile kisa cha"Mtumwa Mpendwa" aliyefurahia kupendelewa na bwana wake hadi siku ile yule bwana alipokufa...

Mama ana kazi na kibarua kigumu..maana hata kufoka hawezi na akiwabwatukia watalia hawa kama watoto waliodekezwa, wakadeka, na kudekeka..mtaa mzima utawasikia...na hawanyamazi hadi wapewe "fanta"
Mzee Mwanakijiji jiheshimu!! Hata tukiwa masikini ni sisi kwenye nchi yetu. Tulimuondoa Mkoloni ili tuwe huru.

Hivi kwa heshima unayopewa JF kweli unaunga mkono Watanzania wenzio kuuliwa na kunyang'anya fedha kwa kisingizio cha kodi?
Mbona Mkapa na Kikwette walikusanya bila kuua watu.?

Tanzania itapiga hatua kubwa chini ya Rais SSH, hivyo anavyotupekeka ndiyo tumezoea. Amani, upendo, mshikamano
 
Kuna awamu ambayo nchi hii haikufanya lolote kubwa?

Na kwanini mnapenda sana kufokewa wewe mzee MM? ndivyo mlivyozoea toka mkiwa wadogo, tufikirieni na sisi ambao hatujazoea kufokewa basi! Mko kama watumwa eti mfokewe fokewe kutwa.
 
Ukweli mwingine ambao mpaka sasa hausemwi.

Makosa yaliyofanyika awamu ya tano yataitesa hii nchi kwa miaka miiingi sana, na huu ukweli ni ngumu kuonekana au kusemwa kwa sababu ya unafiki wetu na staili ya uongozi wa propaganda awamu iliyopita..

Madeni yaliyoachwa, big projects zilizoachwa kila mahala huku nchi ikitegemea funds za kuunga unga kuendesha miradi, diplomasia mbovu kuanzia ya uchumi, siasa na jamii ni misalaba itakayomtesa sana mama... Propaganda na brainwashing iliyofanyika kwa watu kama special project ni changamoto nyingine kwenye utawala wa mama maana akili zilijaa propaganda kuliko uhalisia wa mambo..
 
Inasikitisha sana ukifuatilia page na post mbalimbali za Chadema wanavyotukanwa kwenye comments na wachangiaji.
Kuna group linaitwa Chadema in blood kule facebook yani kila wanachopost ni kutukanwa tu na watu, huko instagram ndiyo balaa kabisa, njoo Jamii forum hali ni hiyo hiyo!

Nimeangalia comments za kwenye hotuba ya Mbowe aliyoitoa akisema vibaya utawala wa hayati Magufuli, kwa kweli ni huzuni raia walivyomtukana Mbowe. Swali la kujiuliza Chadema imefikaje huku?

Enzi za Dr Slaa ulikuwa unavaa gwanda la Chadema kwa maringo yote ,leo tuvae kwa aibu ya kujifichaficha?
Je Tundu Lisu ameharibu image ya chama baada ya kuanza kutetea mabeberu?

Je ni Mbowe ameharibu image ya chama baada ya kuwa anaangushwa na konyagi anasingizia amepigwa na wasiojulikana?, au ule uongo wake wa kuibia familia inapompeleka mahakamani anasingizia amefungiwa akaunti zake na serikali??

Kiukweli inahitajika tathimini ya haraka sana kuikoa na kuirudisha Chadema kwa wananchi ili waiamini tena kama zamani.
Wewe sonofobia ni MATAGA ambaye umevaa mawani ya mbao. Wenzio wameshtuka wanajiunga na Rais SSH ambaye amezika MAUJINGA yote ya Mwendazake
 
Jiwe aliamua kuwakorofisha majirani zetu na kuamua kuishi kama tupo kisiwani maana majirani zetu nao waliona isiwe tabu wakatufungia vioo
Kama Magufuli aliwakorofisha majiran zetu na wawekezaji wa nje kwa nini wawekazaji wa Kenya hapa Tanzania ni 500+ lakin wawekezaji wa Tanzania waliopo Kenya ni 30 tu? Kwa matintinki kati ya nchi hizi mbili ipi ina manzingira mazur ya biashara?
 
Mama ana kazi na kibarua kigumu..maana hata kufoka hawezi na akiwabwatukia watalia hawa kama watoto waliodekezwa, wakadeka, na kudekeka..mtaa mzima utawasikia...na hawanyamazi hadi wapewe "fanta"
Yaani akili yako inakutuma kuwa Kiongozi ili awe mzuri ni kufokea watu?? Kwani kuna Mtoto? Sisi sio ng'ombe zake.

Kuachia machinga wapange vitu barabarani na kutuaminisha kuwa sisi ni wanyonge ndio uongozi mzuri?

Kwahio unataka Samia nae aanze kujibu watu kuwa " Baki na Mavi yako nyumbani"?? Au "kama huna hela piga mbuzi"?
 
Ukweli mwingine ambao mpaka sasa hausemwi.

Makosa yaliyofanyika awamu ya tano yataitesa hii nchi kwa miaka miiingi sana, na huu ukweli ni ngumu kuonekana au kusemwa kwa sababu ya unafiki wetu na staili ya uongozi wa propaganda awamu iliyopita..

Madeni yaliyoachwa, big projects zilizoachwa kila mahala huku nchi ikitegemea funds za kuunga unga kuendesha miradi, diplomasia mbovu kuanzia ya uchumi, siasa na jamii ni misalaba itakayomtesa sana mama... Propaganda na brainwashing iliyofanyika kwa watu kama special project ni changamoto nyingine kwenye utawala wa mama maana akili zilijaa propaganda kuliko uhalisia wa mambo..
Kwa mleta mada haya ndio maendeleo eti
 
Kuna muda tafakari zinakuwa nyingi

Kama amebadilisha mahindi na gasi, anafaa kuendelea kutuongoza?

Kama ametoa zawadi ya milioni 400 kwa birthday ya Mzee mmoja tajiri anayeedelea kutunzwa na serikali hadi are, anatufaa?

Inaonekana akili yake ameaiacha Kenya

Kama Dunia imeitangaza Tanzania kuingia uchumi wa kati, na bado kuna mtu anaona wakati wa JPM uchumi ulifungwa, akapimwe akili
 
SSH ni sellout, Rais anayeruhusu mwekezaji aje na expatriates wengi kadri anavyotaka huyo si Rais bali ni hasara, kila siku anatafuta vimatukio visivyo na maana kwa watz kuuza sura ila watz wameshaanza kumdharau baada ya kuonyesha yeye ni Rais wa wawekezaji na sio watz.
 
Kama Magufuli aliwakorofisha majiran zetu na wawekezaji wa nje kwa nini wawekazaji wa Kenya hapa Tanzania ni 500+ lakin wawekezaji wa Tanzania waliopo Kenya ni 30 tu? Kwa matintinki kati ya nchi hizi mbili ipi ina manzingira mazur ya biashara?
Wafanya biashara wa Tanzania hawana uthubutu wa kufanya biashara nchini Kenya .

Wafanya biashara wa Kenya wana uthubutu wa kufanya biashara nchini Tanzania .

Wewe ulitaka wa Kenya wawafunge kamba wafanyabiashara wa Tanzania waende kufanya biashara Kenya?

Unaweza kumlazimisha ngamia kwenda mtoni but huwezi kumlazimisha kunywa maji.
 
Tatizo letu kama taifa linaanzia mbali sana tofauti na wanasiasa wanavyotuaminisha kwa sasa. Fikiria huyu mama alikuwa msaidizi wa hayati lakini baada ya kupokea uongozi ndani ya siku 50 tu anaonekana kimatendo alikuwa hakubaliana na jpm walau hata kwa asilimia 50 tu. Huwa najiuliza ingetokea magufuli amekuwa mahtuti halafu mama akashika nchi kwa kipindi cha mpito walau miezi 3 tu,angekuwa anafanya anayoyafanya hivi sasa au angetekeleza matakwa ya jpm?
Tunakosa dira ya taifa kwa sababu wanasiasa wanataka kupendwa kwanza kuliko kufikiria maslahi mapana ya taifa. Hii mark time tunayopiga miaka nenda rudi haitakaa iishe sababu kila mtu anatengeneza legacy yake.
Swali la kizushi: kwani mtu akichaguliwa kuwa msaidizi na akashindwa kuridhika na utendaji wa boss wake haruhusiwi kujiuzuru ili kuonyesha uwajibikaji?
Jiwe hawezi kuwa na legacy yoyote maana hakuna alichofanya
 
Mzee Mwanakijiji jiheshimu!! Hata tukiwa masikini ni sisi kwenye nchi yetu. Tulimuondoa Mkoloni ili tuwe huru.

Hivi kwa heshima unayopewa JF kweli unaunga mkono Watanzania wenzio kuuliwa na kunyang'anya fedha kwa kisingizio cha kodi?
Mbona Mkapa na Kikwette walikusanya bila kuua watu.?

Tanzania itapiga hatua kubwa chini ya Rais SSH, hivyo anavyotupekeka ndiyo tumezoea. Amani, upendo, mshikamano
Hao wote wapo kwenye kundi linalo mpinga mama yetu.

Usiwaone wanajichekesha lkn moyoni mwao wapo kama kenge tu.
 
Jiwe aliamua kuwakorofisha majirani zetu na kuamua kuishi kama tupo kisiwani maana majirani zetu nao waliona isiwe tabu wakatufungia vioo
Aliwakorofisha vp?hebu tupe mifano hai walau 3 tu.
Na lini majirani waliifungia TZ mipaka?, au ni ile ya kipindi cha corona?
Hii mentality ya baadhi ya watu kama wewe mnaotaka Taifa hili liendelee kuishi kwa kuwanyenyekea mataifa mengine ni ya kipumbaf sana.
 
Back
Top Bottom