INTRO: Takriban kilomita 180 mashariki mwa Beijing, mji mkuu wa China, kuna mji unaoitwa Tangshan, ambao ni mji mkubwa zaidi wa chuma katika Mkoa wa Hebei, unaochangia takriban moja ya nane ya uzalishaji wa chuma nchini China. Zamani Tangshan ilikuwa mojawapo ya miji yenye uchafuzi mkubwa zaidi nchini China.
Hii ni siku moja ya mwaka 2022. Kulingana na data za satilaiti za kufuatilia mazingira, tumerejesha anga safi nchini China, na milima na tambarare zinaonekana wazi. Tunarudi nyuma hadi miaka kumi iliyopita, ambapo maeneo mengi yamefunikwa na ukungu wa kijivu.
Kwa msaada wa picha za satilaiti, inaonekana wazi kwamba miaka kumi iliyopita, Kiwanda cha Chuma na Chuma cha pua cha Jinxi huko Tangshan kilifunikwa na vumbi la rangi ya kijivu. Hadi kufikia Machi 2021, eneo la kiwanda, karakana na vifaa saidizi vinaonekana kwa uwazi kwenye picha za satilaiti.
Nini kilitokea katika miaka kumi?
Nilipokuwa nikitembea kwenye yadi ya kiwanda hiki cha chuma, niliona vifaa 10 vya uchunguzi vyenye mionzi, mizinga 15 ya ukungu, na vichwa 2,500 vya kupuliza vikiwepo kwa saa 24. Mara vumbi lilipozidi kiwango, walipuliza na kukandamiza vumbi mara moja. Katika karakana ya tanuri la kulipulia, tundu la bomba limefungwa na kifuniko cha vumbi, na feni lenye nguvu kubwa linatawanya moshi na vumbi. Mfumo mzuri wa usimamizi na udhibiti wa utoaji wa hewa kwa kiwango cha chini zaidi unafuatilia hali zote za hewa na mchakato mzima wa vyanzo 2,619 vya utoaji wa vumbi.
Kiwanda cha Chuma na Chuma cha pua cha Jinxi kimeanza kuangaliwa zaidi, wakati wa "Mpango wa 13 wa Miaka Mitano" (2016-2020), ambapo uwezo wa uzalishaji wa chuma uliopunguzwa ulichangia theluthi moja ya jumla ya nchi. Sambamba na hilo, wastani wa mkusanyiko wa PM2.5 katika Mkoa wa Hebei umepungua kutoka mikrogramu 108 kwa kila mita ya ujazo katika mwaka 2013 hadi mikrogramu 38.8 kwa kila mita ya ujazo katika mwaka 2021. Pia huko Hebei, katika muongo mmoja uliopita, wakati uchafuzi wa viwandani umepunguzwa, muundo wa nishati umekuwa safi zaidi.
Miale ya nuru inayoinuka inaonesha kuongezeka kwa uwezo uzalishaji wa umeme kwa nishati ya upepo na jua katika China nzima ndani ya kipindi cha muongo mmoja uliopita. Katika muongo uliopita, uwezo uliowekwa wa China na uzalishaji wa umeme wa nishati mbadala ulishika nafasi ya kwanza duniani. Leo, kwa kila kWh 3 za umeme zinazotumiwa na watu, kWh 1 ni umeme safi. Tuliangalia siku bora zilizotangazwa na miji 339 ya ngazi ya wilaya na zaidi nchini China, na kugundua kuwa ikilinganishwa na siku 280 za mwaka 2015, idadi ya siku zenye anga safi ya buluu kwa kila mji iliongezeka kwa wastani wa siku 39 mwaka 2021, na kufikia siku 319.
Ubora wa hewa kwa ujumla unahusiana moja kwa moja na furaha ya umma. Kiongozi mkuu wa China, Xi Jinping, alisema: "Anga ya buluu na mawingu meupe na nyota zinazometa zirudishwe kwa watu wa kawaida."
Miaka kumi iliyopita, kutoka marekebisho ya muundo wa viwanda hadi uingizwaji wa nishati safi, kutoka kuzuia na kudhibiti uchafuzi wa hewa wakati wa majira ya mpukutiko na baridi hadi uzuiaji na udhibiti wa pamoja wa kimaeneo, vita vya kulinda anga ya buluu vimetekelezwa kikamilifu. Anga ya buluu, mawingu meupe na nyota zinazometa inayoongezeka kila siku huleta furaha ya kweli kwa watu.
Nyota zinazometa, anga ya buluu na mawingu meupe, nyuma ya yote haya linathibitishwa azimio thabiti la China na juhudi zisizo na kikomo za kushinda vita dhidi ya uchafuzi wa mazingira.