Kufuzu AFCON-2019: Stars yashindwa kufunga mahesabu mapema! Yakubali kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa Lesotho

Timu ya Taifa la Tanzania maarufu kama Taifa Stars leo inashuka dimbani dhidi ya Lesotho katika mchezo wa leo kuwania kufuzu fainali mataifa ya Afrika AFCON 2019.

Taifa stars wataanza mechi ya leo kwa kumkosa mshambuliaji wake hatari Mbwana Samatta kutokana na Kadi ya Njano aliyoonyeshwa mchezo uliopita.

Kikosi cha Taifa Stars kinachotatajiwa kuanza katika mechi ya leo.

Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya Tanzania, Taifa Stars imekubali kichapo cha goli 1-0 dhidi ya Lesotho kwenye mchezo wa kufuzu AFCON 2019.

Kwa matokeo hayo Taifa Stars inakuwa na alama 5 ikiwa imecheza michezo mitano jambo ambalo itahitajika kushinda dhidi ya Uganda kwenye mchezo wake wa mwisho huku ikiwaombea Cape Verde wenye alama 4 waitandike Lesotho.

Bado matumaini ni madogo kwa Taifa Stars kufuzu kwenda AFCON 2019.
 
Ndoto tasa ....I rebuke this dream in Jesus name!
 
Mmhhhh. Hiki kikosi ngoja nijipe moyo kwa kusema kocha anawajua wachezaji wake.
 
We siyo mzalendo, unatamani tufungwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…