Wakuu leo naona tunapigwa kabisa kwakweli tujipange kuvumilia maumivu
=====
UPDATES
View attachment 938796
Kikosi cha timu ya Taifa cha Tanzania 'Taifa Stars' leo kimeshindwa kuandika historia ya kukata tiketi ya kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika(Afcon) baada ya kupoteza pointi tatu mbele ya Lesotho kwa kufungwa bao 1-0.
Stars wapo kundi L lenye timu ya Uganda iliyofuzu baada ya kufikisha pointi 13 huku timu ya Lesotho ikifikisha pointi 5 sawa na Stars, Cape Verde ina pointi 4
View attachment 938798
Kwa kupoteza mchezo wa leo matumaini ya ya timu itakayoungana na Uganda Afcon Cameroon mwakani kwa kundi L yamebaki kwenye mechi za mwisho zitakazofanyika mwakani
Stars watacheza na Uganda nyumbani mwezi Machi mchezo wa marudiano, huku Lesotho wakicheza na Cape Verde wenye pointi 4
Ikumbukwe kuwa mara ya mwisho Stairs kufuzu kucheza michuan hiyo ni mwaka 1979
View attachment 938797