Kufuzu AFCON 2023 | Taifa Stars 0-2 Algeria | Uwanja wa Benjamin Mkapa

Kufuzu AFCON 2023 | Taifa Stars 0-2 Algeria | Uwanja wa Benjamin Mkapa

Kuna wale wanasemaga* zamani na haohao wa zamani hatujawahi kwenda hata world cup na afcon....utasikia Pondamali, Mohamed Mwameja,Mwamba kizota,Mzee wa Kiminyio,Salvatory Edward,Sele Matola,Lunyamila,Kenneth Mkapa etc sisi uongo uongo ndiyo mwingi ni sawa na kila mzazi anapomwambia mwanaye alikuwa anakuwa namba moja darasani
Inshort hatujawahi kuwa na timu ya maana iliyotufikisha mahali pazuri
 
Tanzania kipindi kile waliwahonga Uganda wakawaachia kufuzu Afcon ya 2019 kule Misri ili tu ionekane kwamba wamefuzu tu Magufuli akiwa rais baada ya karibu miaka 40.
 
Ukiacha uwekezaji mdogo katika soka, kingine kinacho wanufaisha wenzetu ni uraia pacha.
Nchi nyingi za Afrika zinafaidika na wachezaji ambao wamezaliwa na kupata misingi ya soka Ulaya tangu wadogo ila wamekosa nafasi katika mataifa makubwa katika nchi hizo za Ulaya, wachezaji hao wanakuja kuchezea nchi zao za asilia uku wakifaidika na uraia pacha.
 
Kuna wale wanasemaga* zamani na haohao wa zamani hatujawahi kwenda hata world cup na afcon....utasikia Pondamali, Mohamed Mwameja,Mwamba kizota,Mzee wa Kiminyio,Salvatory Edward,Sele Matola,Lunyamila,Kenneth Mkapa etc sisi uongo uongo ndiyo mwingi ni sawa na kila mzazi anapomwambia mwanaye alikuwa anakuwa namba moja darasani
Uko sahihi, wengine wamesimuliwa tu

Sent from my Redmi Note 8 Pro using JamiiForums mobile app
 
Taifa stars wachovu.

Hawawezi kuanzisha mpira haraka wa goal kick kwa kutumia walinzi wa pembeni.

Space ya mchezo wao ni wa polepole kupita kiasi hasa kuanzia mstari wa ulinzi na kujikuta wanazibiwa nafasi na timu pinzani.

Line ya mbele ya Taifa stars ya kina Kibu Denis, Mbwana Samatta wamejitahidi, tatizo mpira unapoanza toka back line hawajiamini kutumika kama watia mbinyo bali nao wanabakia kucheza ndani ya 18 yao badala ya kupandisha kwa kasi.

Nini kifanyike? Back line yote ifumuliwe abaki Mohamed Hussein , watafutwe wengine maana upande wa ushambuliaji wapo wapya walioongezwa kama kina George Mpole na wakaweza kufanya majukumu.
Yaani abaki Mohamed Hussein ambaye leo ndiyo ilikuwa barabara ya Waalgeria kupita
 
Yaani abaki Mohamed Hussein ambaye leo ndiyo ilikuwa barabara ya Waalgeria kupita

Kumbuka huyu amecheza mechi nyingi za kimataifa ngazi ya klabu na mashindano mengi ya CAF klabu bingwa na confederation hivyo atakuwa akielekeza wachezaji wapya wa sehemu ya ulinzi watakaoitwa Taifa stars.

08 June 2022
Hali ilivyokuwa Benjamin Mkapa stadium

Back
Top Bottom