Kufuzu AFCON 2023 | Taifa Stars 0-2 Algeria | Uwanja wa Benjamin Mkapa

Kufuzu AFCON 2023 | Taifa Stars 0-2 Algeria | Uwanja wa Benjamin Mkapa

Dickson Kibabage ni mchezaji hewa,hana msaada wowote kwenye pitch.

Simon Msuva siku mbaya kazini.

Kibu Denis ni bora aingie kuongeza nguvu kule mbele.

Simba ile kamati yenu ipo wapi muinusuru timu..[emoji3064]
Hahahaaaaa weweeee utuache simba hatuhusiki huku.Kwanza si huwa mnatuponda ninyi!

Aje GSM anunue mechi kama alivyofanya msimu huu
 
Hiyo nidhamu itapatikana wapi kwa aina ya mabeki wetu wa kati! Bakary Mwamnyeto ni beki anayejisahau sana awapo uwanjani!

Na hata ukimfuatilia kwenye timu yake ya Yanga, amekuwa akisababisha mara nyingi timu kufungwa magoli ya kizembe kwa sababu ya kujisahau kwake.

Dickson Job naye anakula sana daruga nje ya 18! Jambo ambalo ni hatari sana iwapo hawa jamaa watatumia nafasi vizuri.
Mwamnyeto kasababisha tena lakini sio mbaya tumejitahidi hii hii moja tuliyopigwa twende nayo hivyo hivyo.

Japo pia hata sammata na msuva pale walichezea nafasi pia.

Dickson job amejitahidi sana
 
Yaani watu mnashupaza mishipa ya shingo kabisa kwa ajili ya Taifa stars

Mpira kwenye national level bado tupo chini wazee
 
Hahahaaaaa weweeee utuache simba hatuhusiki huku.Kwanza si huwa mnatuponda ninyi!

Aje GSM anunue mechi kama alivyofanya msimu huu
Mkuu linapokuja swala la team ya taifa,Ni manufaa yetu sote sio Simba au Yanga ambaye ananufaika.

Mkuu wabembeleze hao wazee wako wa msimbazi [emoji16]
 
Back
Top Bottom