Kufuzu AFCON 2023 | Taifa Stars 0-2 Algeria | Uwanja wa Benjamin Mkapa

Kufuzu AFCON 2023 | Taifa Stars 0-2 Algeria | Uwanja wa Benjamin Mkapa

Bado tunajipa uhakika mkubwa kuwa tutavuka?, ni kichaa tu ndo ataamini kuwa tuna timu nzuri ya ushindani!, hatuna hata ubavu wa kushindana kishindani na timu hata za majirani zetu sembuse Algeria ambayo nayo ni Kama inapitia kipindi kigumu na Cha mpito.
 
Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) leo Jumatano ya Juni 8, 2022 kinashuka katika dimba la Benjamin Mkapa kukivurumisha na timu ya Taifa ya Algeria.

Ni fusra kwa Stars kuweka hai ndoto za Nchi kuweza kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) endapo watapata matokeo ya ushindi dhidi ya Algeria baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika mchezo wa kwanza wa kundi F ugenini dhidi ya Niger.

Mchezo hautakuwa rahisi, mchezo unatarajiwa kuwa ni mgumu, lakini la muhimu kwa Taifa Stars ni nidhamu ya mchezo na kufanyia kazi mbinu ya Kocha pamoja na kupambana kwa nguvu zote ndani ya dakika 90 kwenye mchezo huu, hakika watafanikiwa kuwapa furaha Watanzania.

Kila la heri Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Kumbuka mchezo ni kuanzia majira ya saa 1: 00 Usiku kwa saa za Afrika Mashariki na Kati..Usikose Ukaulizia

============================

00' Mpira umeanza Uwanja wa Benjamin Mkapa | Tanzania 0-0 Algeria

05' mchezo wa kasi kiasi mpaka sasa hakuna timu imeona lango la mwenzake.

10' Algeria wanajaribu shambulizi lakini golikipa Manula anatoka na kudaka mpira ule..!

15' Ameinga Zargane upande wa Algeria, ametoka mchezaji jezi namba 14 baada ya kupata rabsha

20' Algeria wanaliandama lango la Tanzania, ila Tanzania upande wa mbele bado hawajafanikiwa kuitia kashi kashi.

Unapigwa mbele kuleee lakini golikipa Manula anatoka na kudaka, Islam alikuwa karibu akivizia.

Faisal anapiga shutii lakini mpira unatoka nje ya lango na kuwa goal kick

30' Hakuna bao, mpira unachezwa katikati ya Uwanja, Tanzania bado hawajapenya ngome ya Algeria

Almanusura Algeria wapate bao kama si uimara wa golikipa Manula huku Samatta naye akikosa nafasi ya kufunga upande wa Tanzania.

35' Faisal anafungua shuti kali, lakini mpira unambabatiza Mandi wa Algeria, ilikuwa nafasi nzuri ya kufunga.

40' baada ya mashambulizi kwa pande zote mbili, mpira umepoa, huku Novatus akiwa chini baada kupata rabsha

Kona inapigwa kuelekea Algeria, inapigwa kulee lakini mpira anao Faisal anajaribu kutafuta nafasiii

45+2' Free Kick kuelekea stars, inapigwa kulee, Mandi anarudisha ndani hatariiiii | Goooooooooaaal, Rami Bensebaini anaipatia Algeria bao la kwanza kwa kichwa baada ya mabeki wa Stars kushindwa kuruka na kuondosha mpira

HT: Tanzania 0-1 Algeria

Kipindi cha pili kimeanza, mabadiliko kwa Tanzania | Ameingia Kibu Denis na ametoka Kibabage

53' Kibu alishakwamisha mpira wavuni, lakini refa anasema Kibu kabla ya kufunga alisukuma, huku Novatus akionyeshwa KADI ya njano

55' Kazi nzuri ya Msuva inashindwa kuzaa bao, namna gani Tanzania hapa.

Mohamed anarukaaaa kichwa lakini mpira unatoka nje, huku Mzamiru akionywa na mwamuzi kwa mchezo mbaya.

61' Faisal anapiga shutii kali sana lakini golikipa wa Algeria anarukaa na kuwa Kona ambayo haikuzaa bao

64' George Mpole na Kelvin John wameingia kuchukua nafasi za Faisal na Msuva

66' Bakar Mwamnyeto anaonyeshwa KADI ya Njano baada kucheza kwa mkono, mpira umechangamka lakini Stars bado hawajaona lango.

72' Rami Bensebaini ametoka na ameingia Touba upande wa Algeria

Ibrahim anapiga shuti, lakini golikipa Manula anapangua na kuwa Kona ambayo haikuzaa bao

80' Algeria wanafanya mabadiliko huku Stars wakishindwa kabisa namna ya kupenya mabeki wa Algeria

Ametoka Novatus na ameingia Abubakar upande wa Tanzania, je yapo Matumaini ya kupata bao? Ngoja Tuone.

87' Kevin John anafanyiwa madhambi eneo, karibu kabisa na box ni nafasi nzuri hii, free Kick, inapigwa kulee lakini golikipa anapangua.

Goooooooooooooaaal Algeria wanapata bao la pili kupitia kwa Mohamed Amoura | Tanzania 0-2 Algeria.

90+4' Matumaini ya kusawazisha yanatoweka hapa, Kibu anapiga Krosi lakini mpira unaokolewa.

Hatari nyingine upande wa Tanzania, lakini mpira unaokolewa, Tanzania wanapata Kona ambayo haikuzaa bao

Naaam mpira Umekwishaaaaaa ambapo Tanzania imelala nyumbani kwa mabao mawili kwa bila.

FT: Tanzania 0-2 Algeria
Kwanza msisahau Kati ya timu za taifa Bora Africa Algeria wapo na ukichukulia moja ya timu zinazotola ukanda was kaskazini zenye kiwango Bora Cha soka Algeria Ni wazuri kucheza na Tanzania Ni Kama walikuwa wankuja kamilisha ratiba kwasbb wanjua kiwango Cha mataifa ya East Africa ukanda wa maziwa makuu ukiacha wacongo mpira hatuna tunajua kuruka ruka Kama bisi Kuna wakt natamani awepo forward Kama mayele pale mbele na viungo wazuri Kama tshabalala ,day pakawa na nguvu katika na mbele alfu paswepo beki vichochoro mpira wetu ungekuwa mbali Sana Kama ligi yetu inavyotambulika Africa mzima ,Tukiacha siasa na upigaji bongo mpira upo mwing Sana kuliko hata hao tunaowaona SEMA michongo mingi Yan mtot wa mtu Fulani aweke wafulani aachwe ili mradi ulaji wa kifamilia uwepo watu wasilale njaa. Hiv Kama fay ,mpole na wengn wanaupiga mpira hvyo vip wale ambao wameachwa mtaani n ywezekan walikuwa wazuri kuliko wao. #Mchongo Ni kufelishana Babu, taifa la michongo maendeleo y michongo tunaishi kimichongo
 
Hawa Taifa Stars walivyocheza leo polepole sana wangefaa wakacheze mechi za kimataifa za walking football

„You'll never walk alone“ - Fußball im Gehen bei der SGD



Walking football inspires more and more people around the world every year. Since this season, the SGD has also been offering age-appropriate and health-promoting sport exclusively for "55 plus" club members.

Around 30 members came to the opening event at the Rudolf Harbig Stadium. In the presence of honorary captains Hans-Jürgen Dörner and Hansi Kreische as well as dynamo legend Udo Schmuck, coach Holger Hums explained the special features of the new trend sport. Then he asked for the first training session.

DynamoTV
 
Tuongee Tu Ukweli, na Tuachane na Habari ya Ufupi na Urefu.
.
Algeria ni Bora sana Kuliko Team Yetu ya Taifa.
.
Ubora Wa Algeria na Taifa Star Iko Tofauti Kabisa, Hawafanani Kwa Lolote.
 
Uyo Novartus yupo macabi gani mbona uko hachezagi kabisa?
 
Back
Top Bottom