Mati Mkenda
Senior Member
- Mar 4, 2018
- 171
- 211
Kwa muda mrefu chama cha ACT-Wazalendo kimekuwa kikiwashawishi Viongozi wa CHADEMA ili wakubaliane na wazo lao la kushirikiana au kuungana katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu. Ikumbukwe kuwa ACT-Wazalendo ndio wameonekana kuwahitaji zaidi Chadema, kuliko wao kuhitajiwa na CHADEMA.
Taarifa za kuaminika kutoka kwa mmoja wa wajumbe waliohusika kwenye mazungumzo hayo ni kuwa CHADEMA wamekataa katakata baada ya kugundua mchezo mchafu ambao ACT-Wazalendo wametaka kuucheza ili kujijenga kisiasa. CHADEMA bado wanahangaika kuuguza majeraha waliyoyapata baada ya kubadili gia angani mwaka 2015 kwa kumsajili, kumsafisha na hatimaye kumpa nafasi kubwa mtu waliyemchafua kwa muda mrefu, ambaye mwisho aliwakimbia. Lakini pia CHADEMA bado wanahangaika kujenga imani kwa wafuasi wao ambao wameonekana kufurahishwa na namna serikali ilivyotekeleza yale yote ambayo wao walikuwa wakiyalilia kwa muda mrefu, licha ya viongozi wao kubeza juhudi hizo za serikali.
Kutokana na hilo CHADEMA wamesema kila mtu afe kivyake na mchakato wa kupitisha wagombea ndani ya vyama hivyo umeanza. ACT-Wazalendo wanahaha kwa sababu wanajua kuwa mtu wanayetaka kumsimamisha kama mgombea kwa nafasi ya Urais hana mvuto mkubwa kisiasa, kwani mwaka 2015 wananchi wengi sana walimkataa kwa nguvu zote. Mtu huyo hafahamiki kabisa nje ya ukanda wa Kusini anakotokea, na ndio maana muda mwingi wamekuwa wakijinadi huko.
Wakati UKAWA ukiwa umesambaratika, vyama vingi vilivyokuwa ndani ya umoja huo vimeamua kumuunga mkono Mgombea Urais aliyepitishwa na CCM katika nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mh. John Pombe Magufuli.