Hakuna chama chochote kinaweza kuitoa CCM madarakani.
CCM inajeshi vyama vyote vinasajiriwa na msajiri wa CCM, kupata vibali vya mikutano vinaomba majeshi ya ccm, mikutano inalindwa na majeshi ya ccm kasoro CCM wenyewe hawalindwi, wanajilinda na chipukizi wao.
Kwa sasa vyama vinafundishwa kumsifia Mamama kwenye kampeni za siasa, kama fadhila ya kuwaruhusu kufanya siasa nchini halafu huyo ndiyo mnafanya siasa mumshinde.
Tanzanzania hakuna Siasa ni ujinga.
Kila chenye mwanzo kina mwisho. Kuna tawala nyingi duniani ambazo zilikuwa na nguvu kubwa lakini ziliangushwa.
Utawala unaotegemea nguvu ya polisi na jeshi mara nyingi huanguka kwa sababu ya kupoteza uaminifu wa vikosi hivyo (Mgawanyiko), vuguvugu la umma, na shinikizo la kimataifa. Hii baadhi ya mifano ya hivi karibuni (Karne ya 20):
1. Utawala wa Idi Amin (Uganda)
•Muda wa Utawala: 1971-1979.
•Mbinu za Utawala:
o Idi Amin alitegemea vikosi vya jeshi na polisi kubaki madarakani, akiwatishia wapinzani wake na kutumia ukatili dhidi ya raia.
o Alifukuza wapinzani wake wa kisiasa na kuanzisha hali ya hofu kupitia mauaji ya watu zaidi ya 300,000.
•Sababu za Kuanguka:
o Vita vya Ndani na Mipaka: Alianzisha vita dhidi ya Tanzania mwaka 1978, lakini alishindwa vibaya.
o Kuasi kwa Jeshi: Jeshi lake lilianza kupoteza uaminifu kwake, na vita vilivyopiganwa na majeshi ya Tanzania vikachangia kuondolewa kwake madarakani.
•Matokeo: Amin alikimbilia uhamishoni nchini Saud
2.Utawala wa Nicolae Ceaușescu (Romania)
•Muda wa Utawala: 1965-1989.
•Mbinu za Utawala:
o Ceaușescu alitegemea polisi wa siri maarufu kama Securitate, mojawapo ya vikosi vya polisi wa siri vilivyokuwa na nguvu zaidi duniani. Vikosi hivi vilitumia mbinu za ujasusi, ukandamizaji, na hofu kudhibiti upinzani, uhuru wa habari na kujieleza.
o Jeshi lilitumika kuzima maandamano ya umma, na hofu ilikuwa silaha kuu ya kulinda utawala wake.
•Sababu za Kuanguka:
o Uchumi Mbaya: Nchi ilikumbwa na hali mbaya ya kiuchumi, njaa, na ukosefu wa huduma za msingi kutokana na sera zake za kifedha na viwanda.
o Vuguvugu la Umma: Maandamano ya umma dhidi ya ukandamizaji na hali duni ya maisha yalianza mjini Timișoara mnamo Desemba 1989.
o Jeshi Kugawanyika: Wakati maandamano yalipozidi, sehemu kubwa ya jeshi ilikataa kuwashambulia waandamanaji na badala yake ikajiunga na wananchi.
•Matokeo: Mnamo Desemba 25, 1989, Ceaușescu na mke wake Elena walikamatwa, kuhukumiwa haraka, na kuuawa kwa kupigwa risasi.
3.Utawala wa Augusto Pinochet (Chile)
•Muda wa Utawala: 1973-1990.
•Mbinu za Utawala:
o Pinochet alitumia jeshi na polisi kwa ukandamizaji wa wapinzani wa kisiasa kupitia mauaji, ukamataji, na mateso.
o Alifuta taasisi za kidemokrasia na kudhibiti vyombo vya habari.
•Sababu za Kuanguka:
o Shinikizo la Ndani na Nje: Nchi nyingi zikiwemo, Sweden, Norway, uholanzi, uhispania, na Nchi nyingi za Amerca kusini zilipinga utawala wake na kuweka shinikizo kubwa. Wananchi walipiga kura ya maoni mwaka 1988, ambapo wengi walikataa kuendelea na utawala wake.
o Jeshi na Polisi Kukosa Uungwaji Mkono: Jeshi la polisi liligawanyika Wananchi wa kapata nguvu ya kushinikiza demokrasia kwa maandamano makubwa, ilimlazimu Pinochet kuruhusu mabadiliko ya kisiasa.
•Matokeo: Aliondoka madarakani mwaka 1990 na demokrasia kurejeshwa