Kuhamia CHAUMMA ni ujinga mwingine wa Watanzania soma hapa ujue kwanini!?

Narudia tena, lazima nipige kura. CHADEMA wakishiriki nitawapigia kura wao. Wasiposhiriki nitawapigia kura CHAUMMA
 
hiyo mifano ya utawala wa military junta (Id Amin) na one party socialist system (Nicolae Ceaușescu) haifanani na siasa za leo hata kidogo,
 
Umakini wa CHADEMA ni rasilimali watu, sio jina. Watu hao hao wakihamia CHAUMMA, basi CHAUMMA itakuwa na umakini ule ule kama wa CHADEMA
 
Hii nchi haiwezi kuja kombolewa.

99% ya wanasiasa wanaingia kwenye siasa kwa ajili ya kipato, lazima wawe wanasiasa malaya malaya.

Wananchi tupo kama mazomwe zomwe vile.

Wazee wa mabaka mabaka na mgwanda ya kaki nao wanatumika kisiasa.

Hatuwezi kufika.
 
Unakimbia kuongozwa na Lissu na Heche unakimbia kuogozwa na Mzee wa Ubwabwa na Minja ila hii nchi ina wehu wengi sana baada ya Uchaguzi nawashauri chadema wasiopokee ile mizoga itayotaka kurudi kwenye chama
 
Mkuu watu wanatafuta pesa madaraka ni njia tu.
 
Lakin hakuna mtu aliyeajiriwa kuwa mpinzan. Ukiacha kulaum watu utafanya wewe
 
kukombolewa toka kwa nani?
 
walio hamia CHAUMA ni Condom tupu na maji maji yake- Period- Sahamani kwa lugha hiyo.
 
Chaumma ni kama ngao ya cxm kwa sasa
 
Wale ni CCM, CCM imewapaki hapo kwa muda, CHAUMA ni stand wapo safarini kuelekea CCM
 
N
Chauma inatumika kama walivyotumika Covid 19 kuihadaa dunia kuwa kuna demokrasia nchini na kuficha uharamia wa CCM katika uchaguzi.
Naunga mkono hoja. Chaumma ni mpango wa CCM kujaribu kudhoofisha upinzani wa kweli nchini.
 
Msome Tena mtoa mada.. utapita wapi? CCM inamiliki kila kitu, kuanzia majeshi, bunduki, pesa za nchi, wafanyakazi, tume ya Uchaguzi na mfumo wake, mahakama.
Ndiyo maana wenzetu wanataka Reforms!
Reforms mbona wala sio swala la msingi..yaani unamshauri au kuomba CCM ifanye reforms ili wewe ushinde uchaguzi? Ili ni tatizo kubwa sana.. bora tungeshiriki ili tupate wabunge wa kusukuma hoja yetu hii tofauti na hapo tumeingia chaka
 
Sio wanasiasa tu, hata wananchi, Ukombozi wanaouamini ni wa mtu mmoja mmoja kivyake vyake sio wa kisiasa kupitia kundi la wanasiasa au wa kiharakati.

Kama huaminini ita watu watoke kukomboa unachoamini kinahitaji ukombozi, idadi haitafika kiwango cha polisi na jeshi kusema hapa tutulie tusikilize sababu kila mmoja atakuwa na kinachomfanya asitoke meaning, mwananchi mmoja mmoja ana kaukombozi kake asikotaka kukahatarisha kwa kukomboa wengine.
 
CHAUMMA imegeuzwa kuwa chama shikizi cha muda tu kuelekea uchaguzi mkuu ili kuihujumu chadema iliyo chama mahsusi kwa siasa za mabadiliko nchini. Baada ya uchaguzi chaumma itageuka tena kuwa chama cha vituko kisicho na uelekeo. Maharamia wa siasa za kikora wanakitumia kwa muda maalumu tu
 
Hapa nimekubali uchambuzi wako ni uhalisia ila hapa kwetu tinayosafari ndefu sana.

Tunaambiwa yanayofanywa siyo yeye anayeamuru bali ni viongozi wa kati kutafuta sifa ili wapate madaraka ndio hufanya yote tuyaonayo.

Siamini hilo, kwasababu statements zake zibaashiria yeye kuhusika mojakwa moha.

Ila naona tofauti kati ya mtawala kutumia nguvu pekeyake na hizi nguvu za kushirikiana kati yake na vikosi vya ulinzi na usalama wa nchi.

Najua ndanibya chama hakubaliki lakini wanaotafuta kula wengi wanajinadibu kuwa wanampenda ili kumuonyesha yeye wasikose teuzi, na hao ndio hutuumiza wananchi.

Na hawa middle leaders hutaka kupanda juu, hivyo kufanya kika waliwezalo kumuaminisha kwamba kila wafanyacho ni kulinda nchi na kumuhakikushia yeye ulinzi wa mamlaka yake.

Ningetamani kuwe na uhuru wa kisiasa, haki na usawa nchini lakini kila kukicha naona marumaini yana potea.

Tunaona majeshi yana linda chama tawala na kuumiza upinzani, kuwapoteza kila wanao kosia serikali na utawala uliopo.

Ndio maana nika conclude kwa kusema hakuna chama kibawrza kuiondoa ccm madarakani.
 
Tusiporuhusu siasa safi tutakaribisha civil unrest nadhani ndio kitu ccm wanataka.
CCM hawataki civil unrest wanataka civil obedience, wao wanataka umma/wananchi wawe makondoo, wanaseama UTII BILA SHURUTI.
Yani uamke umetii, ushinde umetii, ulale umetii bila kujali unatii nini.
Wakiiba mali ya umma usiseme, wakifanya ndivyo sivyo usiseme kwasababu wao ni nusu miungu wanaoongozwa na Mungu mtu kutoka magogoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…