Kuhamisha au kubadilisha makazi kwenye maisha ya kila siku...

Kuhamisha au kubadilisha makazi kwenye maisha ya kila siku...

KikulachoChako

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2013
Posts
19,185
Reaction score
37,239
Habari za muda huu ndugu jamaa na marafiki. Natumaini sote tu wazima wa afya na wenzetu ambao wanapitia magumu Mungu awafanyie wepesi.

Kila mmoja wetu ana makazi katika eneo fulani. Makazi ndio stara kubwa kwa mwanadamu, ndio maana wazee wetu wa zamani walifanya mpaka mapango kuwa sehemu ya makazi.

Lakini pia makazi sio stara pekee bali makazi yako yana mchango mkubwa sana kwenye maisha yako ya kila siku kwa namna ya moja kwa moja au isiwe moja kwa moja.

Mchango wa makazi yako kwenye maisha yako inaweza kuwa hasi au chanya kulingana jamii ya watu waliokuzunguka.

Kipimo cha matokeo ya mchango wa makazi yako kwenye maisha yako ni kupima muda ulioishi hilo eneo na mabadiliko kwenye maisha yako.

Hivyo ni vyema vijana kuwa makini au kuongeza umakini wanapochagua eneo la makazi iwe ya kudumu au la muda mfupi.

NB:

 
Back
Top Bottom