Kwa nilivyoelewe mwajiri anajaribu kukwepa kusema uliajiriwa Mtwara anasema Tanzania. Sasa ulivyoandika hujafafanua mna mgogoro gani. Hata hivyo kama alikuajiri Tanzania lazima itamkwe ni sehemu gani ya Tanzania. Sisi wote tumeajiriwa Tanzania, wengine Mtwara, Iringa Dar nk. Mkataba wako unataja wapi? Kama hautaji andaa vielelezo kuonyesha kituo chako cha kwanza kilikuwa Mtwara yeye mwajiri akathibutishe vinginevyo. Kusema Tanzania ni too General, haikubaliki. Labda kama wewe umetoka Nje ya nchi.