Kuhani Musa Richard Mwacha ni nani?

mama D

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Posts
19,981
Reaction score
35,581
Imani ni ufunuo wa Mungu kwa mwanadamu; ni ile hali ya akili ya mtu kupokea ukweli uliofunuliwa na Mungu akiambatanisha nafsi yake kwa Mungu.

Kuhani Musa Richard Mwacha amejulikana kama mtumishi wa Mungu mwenye imani kwa Kristo. Na amekua na huduma yake katika jiji la Dar es salaam kwa miaka michache sasa.

Ukifuatilia ni muda mfupi tangu aanze huduma ila utakutana na mambo mengi sana na kati ya hayo mengi ni style ya mahubiri yake, miujiza na maajabu kwenye ibada zake na idadi kubwa ya waumini alionao ndani ya muda mfupi sana maana miaka 3 au mi4 bado huduma ni changa.

Watu wengi tunajiuliza mengi sana juu ya mtumishi huyu. Wengi wetu hatuamini kama yanayonekana kuotokea ni ya kweli lakini pia wapo wanaoamini ni kweli.

ILA SWALI MOJA LA MSINGI "KUHANI MUSA NI NANI HASWA?

Shuhuda zimetolewa hadharani, na ni shuhuda zinazodhihirisha mambo magumu kufikirika katika hali ya kawaida. Ila hawa walioshuhudia wapo kati yetu, mtaani kwetu hata majumbani kwetu, kigoma, chato, kilimanjaro, sumbawanga, kagera, Dar es salaam mmetisha sana. Wenyeji wa huko mnasemaje kuhusu Kuhani Musa?

Fred William Rwegasira.
Your browser is not able to display this video.

Mr Rwegasira ni mzaliwa wa mkoa wa Kagera, Bukoba kule, Mkazi wa Salasala - Dar es salaam. Na sasa anaishi kimara


Innocent Carol Paulo
Your browser is not able to display this video.

Innocent Carol Paulo ni mzaliwa wa Chato. Na mkazi wa Tabata - Dar es salaam


Levina Lyamuya na mdogo wake
Your browser is not able to display this video.

Levina ni mwenyeji wa Kilema, Moshi- Kilimanjaro

Malkia

Wakorinto




KUHANI MUSA RICHARD MWACHA NI NANI??
[/QUOTE]



Sumbawanga mtoto afufuka
ttps://youtu.be/PHUUbiYOEBY

Cancer

Your browser is not able to display this video.


Baada ya siku2
Your browser is not able to display this video.



Baada ya miezi 2

Your browser is not able to display this video.



Mimi naamini kuna kuponywa na kufufuliwa kwa mtu/watu ikiwa anayeomba anamwamini Mungu na Mungu amempa karama ya uponyaji.

Walishafufuka wengi kabla na baada ya kuja Yesu Kristo.

Nimekuelewa sana. Ufufuo upo na uponyaji upo


Babu Ochu; mimi, wewe, huyo malkia wa freemason sote ni watanzania. Kila kitu kiko wazi upande wa Kuhani Musa tena vipo online hapo.

Sasa nadhani ili kuuthubitishia umma kwamba huo ni upuuzi kama unavyosema lazima uthibitishe kwamba hizo shuhuda ni za uongo. Hivi vitu havihitaji hata hasira vinahitaji tuu kuthibitishwa

Kuhusu matumizi ya biblia vifungu vya kuogofya vya ufunuo na agano la kale sioni kama vinaogofya kuliko matendo yanayofanyika na wanadamu wa leo, na wala hauna kipande cha maandiko matakatifu kisichotakiwa kutumika

Zaidi ya yote ili neno liweze kuwasaidia watu lazima lihubiriwe kwa nyakati na mazingira waliyomo na wanayoishi






'WATU' wakija kuamka tayari jamaa hawahitaji tena, ... na huenda akawa hata mbunge! 😅
mama D ameshakula fweza ya promo! ... KALAGA BAHO
..!

Kwanini tunaongea maneno mengi ya kukataa bila kusema hayo anaayofanya yapo au hayapo?

Turudi kwenye maada, tuje na shuhuda kwamba yanayotendeka pale ni ya uongo au ni ya ukweli kwa maslahi makubwa ya umma



Umesema "Mtu akianza mara nabii, mtume au kuhani, mwulize ni nani aliyempa hicho cheo;" mimi nitakuuliza je, kina Ibrahimu, Musa, Yakobo walipewaga vyeo vyao na nani

Nimepata video ya Kuhani Musa akielezea historia yake kwa ufupi sana



Kuhusu hilo la kuandamana kwenda mortuary na kiongozi wa dini ili akafufue wafu nalo ulifikirie vizuri.
Habari za miujiza ya kufufua wafu ipo tangu enzi za manabii na Yesu Kristo mwenyewe lakini sio kila mtu anayekufa alifufuliwa

Nimesikiliza baadhi ya shuhuda za watu kufufuka sikuona popote pale ambapo amesema anataka kuwafufua; waliofikwa na hayo matukio ndio wamerudi kupaza sauti ya ufufuo




Sijawahi kusikia hilo la kuwako na kiingilio au la kutoa pesa ili watu waponywe. Labda mama kubwa na wengine hao walioshuhudia hapo juu au ndugu na jamaa zao watupatie ukweli wa hili ili tumjue Kuhani Musa zaidi






GREAT THINKERS wa Jamiiforums hivi huyu KUHANI MUSA RICHARD MWACHA ni nani haswa?
 
Hii huduma ya kiroho siku hizi imekuwa biashara, na miongoni mwa vitu wanavyotumia kuvutia wateja ni kufufua misukule nk, bila mkristu kuutambua ukwelI huu utahangaishwa sana na hawa wajasiriamali wanaotumia jina la Yesu Kristu kwa biashara zao, watu wasome biblia huko ndiko kwenye njia ya kweli na uzima.
 
Mimi nampendeaga kwenye mahubiri yake yuko vizuri sana katika kufafanua mambo mbalimbali katika biblia. Kitu kinachonikwaza kwake ni namna anavyochelewesha ibada bila kujali watu wanatoka mbali mara nyingi nikipita tembeon siku za ijuma ana jumanne utawakuta watu wamezagaa kule had saa saba wanatoka ibadani kweli hii sio salama sana,ajitahidi amalize ibada walau saa mbili na nusu watu wawahi kwao.

Mengine jamaa yuko vizuri sana na nazani ndio maana amepata mafanikio Makubwa kwa muda mfupi an kuwazidi hata waliomtangulia
 

Ungepitia huo uzi wote ungekuja na maelezo ya kusaidia zaidi.

Sikiliza na mahubiri





 
Ungepitia huo uzi wote ungekuja na maelezo ya kusaidia zaidi.

Sikiliza na mahubiri




Mitazamo yetu inawezekana inatofautiana kwenye haya masuala ya kiimani, binafsi napenda zaidi kumtafuta na kumjua Yesu Kristu kwa njia zangu nikiamini hata kama kuna mahala nakosea ni yeye kupitia roho mtakatifu ndie atakayenisahihisha kwa wakati wake.
 
Watu wa Dar katika ubora wenu. Ngoja na mimi nitafute kibali nije nianzishe Ministry yangu. Maana kuna uwezekano hela zenu hazina matumizi mengi kama za huku Kijijini niliko.

Hivyo siyo mbaya nikija kula fungu lenu la 10 la mapato ghafi! 😋 Miujiza na mambo mengine yote, yatakuwepo.
 
Pale Kuna maombi kulingana na kiwango chako Cha pesa kuna maombi ya laki laki maombi ya Elfu hamsini ,maombi ya Elfu ishirini na n.k

Uliona WAPI maombi kulingana na umaskini au utajiri WA MTU

Unahitaji kiwango Cha juu Cha upumbavu kumuelewa yule tapeli

USSR
 

Tate Mkuu tuanze kujifunza kwa hawa waliotutangulia
 

USSR umesikiliza hizo clips?
 
Mama D umeisha nasa tiyari, makuani wa Sasa sio wa kuamini mama D
 
Ndio nimeweka hapo washudiaji na uwenyeji wao na makazi yao ili tujue hayo maigizo yanafanyikaje

Bila proof ya unachokisema itazidi kuaminika na kubaki palepale kwamba miujiza inatendeka
Miujiza kutendeka sio ishu maana hata shetani ni mtenda miujiza ,MUNGU ni roho kama alivyoshetani , nguvu ya Giza(shetani)na nguvu ya Nuru (MUNGU)

Nvyojua pale Kuna nguvu ya Giza na inatenda KAZI kwa matambiki ya kigiza bila watu kujua

USSR
 
Kama watu wote wangejua hiki unachokisema Hawa manabii wangefunga huduma.

Tatizo watu siku hizi wanapenda miujiza na kutabiriwa Kama wayahudi wa wakati wa Yesu
 
Sio clips TU dada huyu yupo mitaa ninayoishi namsikia kila siku HASA USIKU ,ni mganga wa kienyeji TU aliyechangamka yesu alitoa Bure, hizi shuhuda ni michongo japo miujiza ipo

USSR


Fanya tumnase basi USSR
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…