Kuhatarisha usalama wa Taifa? Give me a Break!

Kuhatarisha usalama wa Taifa? Give me a Break!

itabidi wawezeshwe kwani wengine wamejiunga humo sababu ya njaa tu na sio kwa kuipenda hiyo kazi..
 
Kwa muda mrefu sana watanzania tumekuwa tukikilalamikia kitengo chetu cha Usalama wa Taifa TISS na bado kinalalamikiwa sana na watanzania. Hiki Kitengo kimegeuzwa kuwanichakichama, kinaacha Kazi yake ya Kulinda nchi yetu na Rasilimali zake tukiwamo sisi Watanzania. Kitengo hichi kimekuwa ndio kitengo cha uchakachuaji kura, kutisha watanzania wanaotetea maslai ya nchi na vitu vingine vinatokea bila hata sisi Watanzania kujua kwenyehicho kitengo.

CCM wamekuwa wanakitumia hiki kitengo kwa maslai yao binafsi, hasa pale panapokuwa na uchaguzi na mambo mengine ambayo yanawagusa watanzania kwenye nchi yao. Fisadi Mkapa amekitumia hiki kitendo sana hasa kwenye ngwe yake ya mwisho ya uraisi, hiki kitengo kama kingekuwa kinafanyakazi kama enzi za Rais JK Nyerere basi Mkapa na Mawaziri wake saa hizi wapo Jela. Mkapa ndio aliasaini mikataba mingi ya Ufisadi. Fisadi Kikwete alioingia madarakani amekigeuza hiki kitengo kuwa juu ya tume ya Uchaguzi NEC. Leo hii kitengo Usalama kimegeuzwa kuwa Kitengo cha uchakachuaji kura, sio tena kulinda nchi yetu kama walivyokuwa zamani. Tunaibiwa kila idara hasa Rasilimali zetu lakini TISS wapo kimya na wameyafumbia macho mambo muhimu na kulinda mafisadi wanaoliangamiza taifa letu.

The question is ARE WE SAFE IN OUR COUNTRY? Iwapo vitengo vyote vya ulinzi vipo chini ya CCM?

JWTZ lipo chini ya CCM, hasa wakubwa wengi walio jeshini ni makada wa CCM na wengi wao wakistaafu wanapewa tunzo za Ukuu wa Wilaya na Mikoa. TISS imegeuzwa kuwa NEC na Ikulu Mawasiliano imegezwa kuwa Kitengo Cha Propaganda. Nchi yetu inaeleke wapi? Tafakari na uchukue hatua kabla ya nchi kuangamia.
 
Ni kweli kabisa tutaangamia kama hatutabadilisha huu mfumo. Kwenye katiba labda, wakichelewesha sijui itakuwaje lakini nahisi machafuko.
 
Chonde chonde Usalama wa Taifa nyie ni watanzania muwe wazalendo kwa kutulindia wapiganaji na watetea watanzania na rasilimali zake.

Jamani nauliza tena usalama wa taifa hawawezi kuwa wazalendo na kukataa kutumiwa kuwadhuru viongozi waadilifu?

Wana JF karibuni kwa mjadala.
 
Kwa ufahamu wangu,national Interests are preserved or safeguarded through national security.Hilo liko very applicable mostly kwa mataifa makubwa.Kwa maana kwa mfano wakivamia taifa jingine ili kulinda national security yao,basi wananchi wao hunufaika kwa kazi,sometimes mafuta, ama rasilimali nyinginezo, na pia contracts za rebuilding etc. Hence national interest.

Kwa kuangalia pande zote,yani kati yetu sisi na wezetu,nimeona kuna tofauti kubwa kama jinsi mfano huo hapo juu unavyoonyesha.

Kwa upande wetu sisi, nimepata shida sana ya kuweza kutambua tofauti zilizoko (kamazipo)kati ya maslahi ya Taifa (National interests) vs yale ya usalama wa Taifa.(National security)

Nimekuwa mara nyingi nikijiuliza kama usalama wa Taifa ina maana sawa na kusema usalama wa wananchi?Ama kuna Taifa bila wananchi?

Lakini kutokana na yale yanayotokea kwenye taifa letu,pertaining to Nationa security and national ineterests,basi napata shida kubwa sana kutambua usalama wetu waTaifa kazi yao kubwa haswa ni kusimamia usalama upi?

Je wanasimamia usalama wa wananchi? Maana binafsi nadhani hiyo ndiyo bottom line.Hata usalama wa wananchi kwetu ni upi haswa?Je ni uwezo wa kwenda kazini salama ama ni uwezo wa kupata kazi na kuilisha familia na kujikimu?Pia si uwezo wa kunufaika na rasilimali zetu?Je hayo si ndiyo maslahi ya Taifa ambayo tunadhani ni ya wananchi?

Je ni kweli hali yetu sisi usalama wa Taifa equals usalama wa wananchi?

Kuna matukio kadhaa wa kadha yaliyopelekea mimi kuanzisha thread hii ili niweze kuelimishwa humu jamvini. Nina imani kabisa kuwa nitaelimishwa.

Kumekuwepo na mijadala kadhaa kuhusiana na viongozi ambao wamekufa ama kuuwawa.Na kumekuwa na speculations mbali mbali kuhusiana na sababu za ni kwanini wameuwawa.

Kwa mfano,kuuwawa kwa Meja jenerali Imrani Kombe aliyewahi kuwa mkurugenzi mkuu wa usalama wa Taifa.Sababu zinazotajwa mojawapo ni kwamba alitoa siri kwa Mrema nawenzake.Siri ambazo zilitakiwa kufichwa ili kulinda usalama wa Taifa.

Wote tunakumbuka kipindi hicho ni kile Mrema alipokuja na ile style ya kulipuwa mabomu.Kweli ilikuwa mshike mshike.

Taarifa hizo ie zile za Loliondo, Chavda, Mohammed Enterprise na mchele mbovu, Kilontsy Mporogonyi na minofu ya samaki nanyinginezo nyingi ikiwemo ile ya dhahabu za Bibi Sitti pale DIA,z ilisaidia kuwa amsha wengi wa wananchi na vijana kipindi hicho.

Machoni pa wananchi, taarifa hizo zilionekana kuzingatia maslahi yao hence usalama wao.Wananchi wengi waliamini kuwa ufisadi huo badala ya kufanywa,basi huduma muhimu za jamii zingepewa kipaumbele kama si miundo mbinu,kilimo,shuguli za uzalishaji nk.Pia waliamini kabisa kuzuiliwa kwa mchele mbovu ni usalama wa wananchi.

Kwa upande mwingine, usalama wa Taifa wao walikuwa na mtizamo wa tofauti. Ama at least bossi (Director)wao pamoja na Rais wakati huo akiwa Mkapa na Mwinyi kabla ya hapo.

Wao sasa ina maana waliona kuwa yale aliyofanya Kombe ni kuhatarisha usalama wa Taifa.Kuna wata kaosema ni lazima u uwawe kama ukitoa siri ya usalama huo wa Taifa.

However, tukiangalia na kufikiri kwa undani,je wali uwawa simply kwa kutoa siri ama kwasababu ya kutoa siri zenye kuhatarisha usalama wa Taifa?Na je usalama wa Taifa,taifa nikina nani hao?

Ni wananchi wote ama ni baadhi tu ya watu?

Wakati nikisubiri maoni,nimepata fundisho kubwa.Labda nitabadili mawazo baada ya maoni yenu.However ninaamini kabisa kuwa usalama wa Taifa ni usalama wa wachache waliopo madarakani na wale wenye kuhodhi rasilimali za taifa kwa kigezo cha soko huria.

Ni muhimu sana tukatanabaisha kati ya salama hizi zinazo simamiwa nawana usalama wetu.Wakati tunafikiria kuhusu katiba mpya.Pia muundo na majukumu ya usalama wa Taifa ni vya kufanyiwa kazi.

Siyo kifo hiki pekee kilichonifanya nigubikwe na maswali haya yasiyoisha.Ni vingi tu kuanzia viongozi wa kisiasa kama Kolimba, Sokoine, Balali pamoja na wengineo kwenye tasnia ya uandishiwa habari ie Stan Katabalo(Stand to be corrected)

Swali kubwa nikwamba,je ni kwa namna gani tutahakikisha kuwa usalama wa Taifa wanaya simamia maslahi halisi ya wananchi?Na kwa maskahi ya wananchi ni kuahikikisha kuwa wananchi wanashare keki ya Taifa lao na si watu wachache.
 
Hapo chini ni functions za TISS ....Baadhi zina utata,wenye kuelewa tueleweshane.
a) to obtain, correlate,and evaluate
intelligence relevant to security,
and to communicate any such intelligence to the Minister and to
persons whom, and in the manner which, the Director-General
considers it to be in the interests of security;

Kwa hiyo Director General hafanyi kazi kwa mujibu wa katiba?Maana hapo wanasema watakachofanya kinategemea kama director ana consider to be in the interests of security.Hawajasema security ya nani!
(b) to advise Ministers,
where the Director-General is satisfied that
it is necessary to do so, in respect of matters -relevant to security,
so far as those matters relate to departments or portfolios of
which they are in charge;

Again hatujui ni nini kinamfanya director general ambaye anateuliwa na Rais kuwa satisfied.

(c) to cooperate as far as practicable and necessary with such other
organs of state and public authorities within or outside Tanzania
as are capable of assisting the Service in the performance of its
functions.
Hata kushirikiana na walioko nje ya nchi kufanikisha hizi functions ambazo hazi outline ni kivipi maslahi ya wananchi ama ni kwa vipi functions hizo zinarelate to national security and interests.

(d) to inform thePresident, and any other person or authority which
the Minister may so direct, of any new area of potential espionage,
sabotage, terrorism or subversion in respect of which the Director-General hasconsidered it necessary to institute surveillance.
Kifungu hiki cha mwisho ndicho haswa kazi yao.Lakini katika kukuru kakara zao,sijaona ni kivipi waliouwawa walikuwa wanakaribia kufanya lolote kati ya hayo yaliyomo kwenye functions,especially hii ya kifungu d.
 
Maswali ni ya msingi kabisa ukitazama hali halisi tuliyokuwanayo. Ila mara nyingi hawa jamaa hawataki kabisa issue kama hizi zijadiliwe. Pengine kuna linalofichwa.
 
Kwa ufahamu wangu,national Interests are preserved or safeguarded through national security.Hilo liko very applicable mostly kwa mataifa makubwa.Kwa maana kwa mfano wakivamia taifa jingine ili kulinda national security yao,basi wananchi wao hunufaika kwa kazi,sometimes mafuta, ama rasilimali nyinginezo, na pia contracts za rebuilding etc. Hence national interest.

Kwa kuangalia pande zote,yani kati yetu sisi na wezetu,nimeona kuna tofauti kubwa kama jinsi mfano huo hapo juu unavyoonyesha.

Kwa upande wetu sisi, nimepata shida sana ya kuweza kutambua tofauti zilizoko (kamazipo)kati ya maslahi ya Taifa (National interests) vs yale ya usalama wa Taifa.(National security)

Nimekuwa mara nyingi nikijiuliza kama usalama wa Taifa ina maana sawa na kusema usalama wa wananchi?Ama kuna Taifa bila wananchi?

Lakini kutokana na yale yanayotokea kwenye taifa letu,pertaining to Nationa security and national ineterests,basi napata shida kubwa sana kutambua usalama wetu waTaifa kazi yao kubwa haswa ni kusimamia usalama upi?

Je wanasimamia usalama wa wananchi? Maana binafsi nadhani hiyo ndiyo bottom line.Hata usalama wa wananchi kwetu ni upi haswa?Je ni uwezo wa kwenda kazini salama ama ni uwezo wa kupata kazi na kuilisha familia na kujikimu?Pia si uwezo wa kunufaika na rasilimali zetu?Je hayo si ndiyo maslahi ya Taifa ambayo tunadhani ni ya wananchi?

Je ni kweli hali yetu sisi usalama wa Taifa equals usalama wa wananchi?

Kuna matukio kadhaa wa kadha yaliyopelekea mimi kuanzisha thread hii ili niweze kuelimishwa humu jamvini. Nina imani kabisa kuwa nitaelimishwa.

Kumekuwepo na mijadala kadhaa kuhusiana na viongozi ambao wamekufa ama kuuwawa.Na kumekuwa na speculations mbali mbali kuhusiana na sababu za ni kwanini wameuwawa.

Kwa mfano,kuuwawa kwa Meja jenerali Imrani Kombe aliyewahi kuwa mkurugenzi mkuu wa usalama wa Taifa.Sababu zinazotajwa mojawapo ni kwamba alitoa siri kwa Mrema nawenzake.Siri ambazo zilitakiwa kufichwa ili kulinda usalama wa Taifa.

Wote tunakumbuka kipindi hicho ni kile Mrema alipokuja na ile style ya kulipuwa mabomu.Kweli ilikuwa mshike mshike.

Taarifa hizo ie zile za Loliondo, Chavda, Mohammed Enterprise na mchele mbovu, Kilontsy Mporogonyi na minofu ya samaki nanyinginezo nyingi ikiwemo ile ya dhahabu za Bibi Sitti pale DIA,z ilisaidia kuwa amsha wengi wa wananchi na vijana kipindi hicho.

Machoni pa wananchi, taarifa hizo zilionekana kuzingatia maslahi yao hence usalama wao.Wananchi wengi waliamini kuwa ufisadi huo badala ya kufanywa,basi huduma muhimu za jamii zingepewa kipaumbele kama si miundo mbinu,kilimo,shuguli za uzalishaji nk.Pia waliamini kabisa kuzuiliwa kwa mchele mbovu ni usalama wa wananchi.

Kwa upande mwingine, usalama wa Taifa wao walikuwa na mtizamo wa tofauti. Ama at least bossi (Director)wao pamoja na Rais wakati huo akiwa Mkapa na Mwinyi kabla ya hapo.

Wao sasa ina maana waliona kuwa yale aliyofanya Kombe ni kuhatarisha usalama wa Taifa.Kuna wata kaosema ni lazima u uwawe kama ukitoa siri ya usalama huo wa Taifa.

However, tukiangalia na kufikiri kwa undani,je wali uwawa simply kwa kutoa siri ama kwasababu ya kutoa siri zenye kuhatarisha usalama wa Taifa?Na je usalama wa Taifa,taifa nikina nani hao?

Ni wananchi wote ama ni baadhi tu ya watu?

Wakati nikisubiri maoni,nimepata fundisho kubwa.Labda nitabadili mawazo baada ya maoni yenu.However ninaamini kabisa kuwa usalama wa Taifa ni usalama wa wachache waliopo madarakani na wale wenye kuhodhi rasilimali za taifa kwa kigezo cha soko huria.

Ni muhimu sana tukatanabaisha kati ya salama hizi zinazo simamiwa nawana usalama wetu.Wakati tunafikiria kuhusu katiba mpya.Pia muundo na majukumu ya usalama wa Taifa ni vya kufanyiwa kazi.

Siyo kifo hiki pekee kilichonifanya nigubikwe na maswali haya yasiyoisha.Ni vingi tu kuanzia viongozi wa kisiasa kama Kolimba, Sokoine, Balali pamoja na wengineo kwenye tasnia ya uandishiwa habari ie Stan Katabalo(Stand to be corrected)

Swali kubwa nikwamba,je ni kwa namna gani tutahakikisha kuwa usalama wa Taifa wanaya simamia maslahi halisi ya wananchi?Na kwa maskahi ya wananchi ni kuahikikisha kuwa wananchi wanashare keki ya Taifa lao na si watu wachache.

Maswali mazuri sana! Ngojea nikipata nafasi nitayapitia kwa undani!
 
Hapo chini ni functions za TISS ....Baadhi zina utata,wenye kuelewa tueleweshane.
Kwa hiyo Director General hafanyi kazi kwa mujibu wa katiba?Maana hapo wanasema watakachofanya kinategemea kama director ana consider to be in the interests of security.Hawajasema security ya nani!

Again hatujui ni nini kinamfanya director general ambaye anateuliwa na Rais kuwa satisfied.

Hata kushirikiana na walioko nje ya nchi kufanikisha hizi functions ambazo hazi outline ni kivipi maslahi ya wananchi ama ni kwa vipi functions hizo zinarelate to national security and interests.
Kifungu hiki cha mwisho ndicho haswa kazi yao.Lakini katika kukuru kakara zao,sijaona ni kivipi waliouwawa walikuwa wanakaribia kufanya lolote kati ya hayo yaliyomo kwenye functions,especially hii ya kifungu d.

Hii sheria ilipitishwa enzi la bunge la NDIO MZEE. Bado hatujafikia hatua ya kupitisha sheria kiukweli. Ukiangalia nchi nyingine zinavyopitisha sheria, unaweza penda. Kwanza wale top law graduates ndio wako employed na parliaments na govt katika kuhakikisha sheria inatungwa kwa maslahi ya wananchi. Hii sheria imeandikwa na kuacha gaps kubwa sana.
Nadhani pia iwe mwamko wa Chadema kuwapa vijana wanasheria ajira ya kufanya uchambuzi na analysis ya hizi bills zinazokuwa introduced. Ni muhimu sana.
 
Mhmh, kuna washkaji nimesoma nao, wengine tumekua pamoja, tumecheza michezo ya utotoni....

Ila kuwaanika hapa kuwa washkaji ni NYOKA naona roho inasita, kama wanakusoma ni heri wabadili tabia.

Ingawa wanalipwa kwa kusaliti watanzania wenzao tuwaambie tu kuwa hela za damu ya watu hazina raha. Wekeni uzalendo wa taifa lenu mbele....
 
Ukiisoma TISS Act ya 1995, utagundua ina mapungufu kadhaa, of course, may be kwa zama zile inasukwa hiyo Act hakukuwa na changamoto za kiusalama (socio economic and political) kama za sasa, nonetheless, nadhan ilikuwa ina suffocate from post~SB philosophy ya kufanya kazi. Nadhan hii n changamoto kwa wao kuifanyia kaz for the prosperity of this nation.

Nonetheless, Intelligence organisation nyingi kazi yao kuu n kuishaur serikali, hvo basi kuna a subtle (Blur), layer btn kushaur na kufanyia kaz kile unachoshaur..at the end of the day inabakia political will ya mshauriwa on hw to get n handy na kile anachoshauriwa...let alone, its all abt fight abt bureacrats and politicians fights, who is at the top and who is at the tap.

Political will ya kutumia int. organs kwa nchi za dunia ya tatu n very low naona.

Ni mtizamo tu.
 
Ndugu zangu siku zote nimekuwa nikifuatilia utendaji kazi wa usalama wa taifa nachelea kusema imekuwa ikitumika kwa maslahi binafsi hasa kuwanufaisha watu wachache na si taifa kwa ujumla.

Usalama wa taifa umekuwa ukisishwa na mambo maovu na si kulinda usalama wa taifa kwa maslahi ya watanzania wote. Usalama wa taifa umekuwa ukitumika kwenye wizi wa kura na mambo mengine maovu na hili la kutaka kuwachafua wabunge wa CDM.

Je usalama wa taifa umekuwa wapi kwa masuala muhimu ya kitaifa kama kusafirishwa kwa wanyama pori kwenda nje, kuingiza madawa ya kulevya na mengineyo mengi.

Usalama wa Taifa wanapaswa kulinda maslahi ya taifa na si binafsi. Wakumbuke hata IRAQI, MISRI, NA KWINGINEKO ni matokeo ya usalama wa taifa kufanya kazi kwa maslahi ya watu binafsi na si ya taifa.
 
Hii sheria ilipitishwa enzi la bunge la NDIO MZEE. Bado hatujafikia hatua ya kupitisha sheria kiukweli. Ukiangalia nchi nyingine zinavyopitisha sheria, unaweza penda. Kwanza wale top law graduates ndio wako employed na parliaments na govt katika kuhakikisha sheria inatungwa kwa maslahi ya wananchi. Hii sheria imeandikwa na kuacha gaps kubwa sana.
Nadhani pia iwe mwamko wa Chadema kuwapa vijana wanasheria ajira ya kufanya uchambuzi na analysis ya hizi bills zinazokuwa introduced. Ni muhimu sana.
You said it all kamanda.The need is imminent,hatuwezi kukaa tu na kulalamika kama ni vile simba anakula watoto wetu na hatuna la kufanya.
 
Mhmh, kuna washkaji nimesoma nao, wengine tumekua pamoja, tumecheza michezo ya utotoni....

Ila kuwaanika hapa kuwa washkaji ni NYOKA naona roho inasita, kama wanakusoma ni heri wabadili tabia.

Ingawa wanalipwa kwa kusaliti watanzania wenzao tuwaambie tu kuwa hela za damu ya watu hazina raha. Wekeni uzalendo wa taifa lenu mbele....

Kama haujajua vizuri duties and responsibilities za TISS hauwezi kujua nini cha kuchangia humu. Think clear..
 
Katika siku za karibuni Idara ya Usalama wa Taifa imekuwa ikitajwa tajwa sana katika vyombo vya habari. Kutajwa tajwa kwa idara hiyo pengine kunatokana na malalamiko ya wananchi hususani viongozi wa vyama vya siasa kwamba wamekuwa wakifuatwa fuatwa na kutishiwa na maafisa wa idara hiyo kiasi cha kuamini kuwa maisha yao yako hatalini. Pia yamekuwepo malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kwamba idara hiyo imeshindwa kupambana na ufisadi, rushwa, biashara ya madawa ya kulevya na kuendelea kukua kwa tabaka kati ya matajiri na masikini.

Aidha katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, idara ya usalama wa Taifa ilipigiwa kelele sana kwa madai kwamba ilihusika kikamilifu katika kuchakachua kura zilizo muwezesha Rais Jakaya Kikwete kupata ushindi dhidi ya Dr Slaa. Tuhuma hizo zilikuwa nzito kiasi cha Naibu Mkurugenzi wa idara hiyo ndugu Nzoka kufanya mkutano maalumu na waandishi wa habari ili kukanusha uvumi huo. Hata hivyo, pamoja na maelezo mazuri ya mkurugenzi huyo, wananchi wengi bado wana amini mpaka leo kwamba maelezo hayo yalikuwa ni siasa na kujiosha tu lakini ukweli ni kwamba idara hiyo ilihusika katika uchakachuaji..

 [TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Rais Jakaya Kikwete
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

 Mambo hayo kwa ujumla wake yamenifanya nijifunze mambo makuu matatu: Kwanza kabisa wananchi walio wengi hawaijui idara ya Usalama waTaifa. Hawajui shughuli zake, utendaji wake, na mipaka yake. Kuto kujua huko kuna wafanya wananchi kuifananisha idara hiyo na iliyokuwa idara ya usalama wa Taifa ya Uganda- Bureau of State Security (wakati wa Iddi Amini) ambayo ilihusika na mauaji na mateso ya raia wengi wa nchi hiyo; jambo ambalo si sahihi. Aidha, kuto ifahamu idara hiyo kunawafanya wananchi wengi wailaumu idara kwa mambo ambayo pengine haihusiki.

Pili, wananchi wengi hawajui tofauti kati ya Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) na Idara ya upelelezi wa makosa ya jinai (CID). Hali hiyo inawafanya wananchi wasiojua tofauti kuilaumu Idara ya Usalama wa Taifa na maafisa wake hata kwa makosa yaliyofanywa na askari wa idara ya upelelezi wa makosa ya jinai. Hata hivyo zipo nyakati ambazo idara hiyo hufanya makosa mbalimbali na hivyo inastahili kupokea lawama kwa makosa iliyofanya.

  [TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Mkurugenzi mstaafu Hassy Kitine
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

 Tatu,IdarayaUsalama wa Taifa haifanyi jitihada za kuwaelimisha wananchi kuhusu muundo wa idara hiyo, majukumu yake na mipaka yake ili kuwafanya wananchi waielewe idara hiyo (wasiiogope), wawe karibu nayo na hivyo kushiriki kikamilifu katika utoaji wa taarifa za ki itelejensia kitu ambacho ni muhimu sana katika mafanikio ya kazi za idara hiyo.

Katika nchi zilizoendelea kama Marekani na Uingereza, Idara za Usalama wa Taifa hususan Central Intelligence Agence (CIA), National Security Agency (NSA), Secret Service, FBI za Marekani na MI 5 ya Uingereza huendesha programu maalum za kuelimisha umma ambapo huwafahamisha wananchi kuhusu kazi za idara hizo, mafanikio na 'challenges' ambazo idara hizo inakutana nazo katika utekelezaji wa majukumu yake. Proglam hizo huendeshwa katika luninga (TV) za Taifa, Radio mbali mbali na vijarida. Utaratibu huo unasaidia sana katika kuwafanya wananchi wazielewe idara hizo, waziheshimu na kuziunga mkono badala ya kuzichukia, na kuzi kashifu na hivyo kutoa ushirikiano mkubwa.katika kufanikisha kazi zake.

Katika kipindi cha utawala wa Mwalimu Nerere, Idara ya Usalama wa Taifa ilikuwa na proglamu za uelimishaji umma kama ilivyo kwa idara nilizo zitaja hapo juu ambapo maafisa wa idara hiyo walishiriki kutoa mafunzo kwa wana mgambo, vyuo vya siasa, makongamano ya viongozi na Jeshi la kujenga Taifa. Hata hivyo proglamu hizo zilidorola baada ya kuanza kwa mfumo wa vyama vingi kutokana na imani ya baadhi ya watu kuwa idara hiyo inafanya kazi ya kuwalinda viongozi wa CCM ili chama hicho kiendelee kubaki madarakani. Hivi sasa Idara hiyo hutoa mafunzo ya utunzaji siri tu kwa walimu wanaoteuliwa kusimamia na kusahihisha mitihani.

 [TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Naibu Mkurugenzi
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Ni kutokana na sababu hizo, pamoja na nyingine ambazo sijazitaja ndio maana nimeona ni vema niandike makala hii ya kuelimisha umma kuhusu idara hiyo. Makala hii itazungumzia muundo wa Idara ya Usalama wa Taifa, Majukumu yake na mipaka yake. Aidha makala hii itaeleza mafanikio ya idara hiyo na 'Challenges' ambazo inapambana nazo katika kutekeleza majukumu yake. Makala hii pia itachambua tofauti kati ya idara ya Usalama wa Taifa (TISS), Idara ya upelelezi wa makosa ya jinai (CID) na Idara ya usalama ya jeshi (Millitary Intelligence). Makala hii pia itaeleza jinsi wananchi wanavyoweza kuwa karibu na idara hiyo, jinsi ya kuweza kupata ajira katika idara hiyo na sifa zinazohitajika kwa waombaji.

Imetoka,

mwana dikala: Ijue idara ya USALAMA WA TAIFA (TISS)

ITAENDELEA.....

Angalizo:

Muandishi wa makala hii HANA UHUSIANO wa aina yoyote na IDARA ya Usalama waTaifa.
 
huna uhusiano na UWT, why should we trust anything you say? So far UWT haufanyi kazi zake vema la sivyo kuna kesi zingekuwa zimefanyiwa kazi!
 
Kasaidia kutoa mwanga, na pia ikumbukwe TISS haiendeshi kesi zaidi ya kushauri tu pale inapokuwa na taarifa na ushahidi wa kutosha!
Ndugu zangu watanzania kwa jinsi nijuavyo Idara ya usalama ya taifa ipo karibu na watu na inahitaji watu, tatizo watu wanataka zaidi ya hapo.
Nionavyo mie, Kuna ofisi za DSO kila wilaya, RSO kila wilaya na wale wako karibu na watu tatizo Binadamu wanataka kujua makrasha ya ofisi zao ndo hapo utata unapoanza
 
Back
Top Bottom