Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hii ni aibu kwa wana-korogwe kwa kumchagua huyu jamaa.Na hata hilo la kushindwa kutofautisha kati ya Polisi, Jeshi, UWT, Mgambo, Sungusungu, Polisi Jamii, Polisi Shirikishi n.k. ni kutokana na elimu yake ndogo ya Std 7.Iwepo sheria ya kudhibiti vilaza kama hawa kuingia bungeni.
unaweza kutolea ushahidi hayo unayoyasema au unabwabwaja tu?
unaweza kutolea ushahidi hayo unayoyasema au unabwabwaja tu?
Ukipita mitaa ya wanayoishi usalama wa taifa, ukiangalia maisha yao na watoto wao ni sawa na maisha ya wananchi wanaolia kila siku ugumu wa maisha. Wanaishi kwenye lindi la umasikini na karaha. Hata wakati mwingine wanagandamizwa na sheria wanazozilinda au kuzifanyia kazi. Wananyanyaswa kimaisha na kujikuta wanatumikia tumbo badala ya taaluma zao. Ukiwauliza wengi wamekata tamaa, wanafanya kazi kwa maelekezo kwa sababu waliapa kufuata mlolongo wa amri.
Sisi ndio usalama wa taifa sisi ndio tunatumika sisi ndio wananchi sisi ndio tunaadhirika. Umefika wakati chombo hiki muhimu kijitambue. Tuelezane kuwa maisha haya magumu ni kushindwa kwa taasisi zetu nyingi kwa kumtumikia mjomba. Hakuna sababu ya usalama wa taifa kukubali kutumika kuiba kura ya mwanao, mjomba , mke au mume. Kuiba kura na haki ya baba yako na mama yako kisa tu wewe usalama wa taifa. Kuiba kura ya daktari halafu kesho unahitaji matibabu bora, kuiba kura ya mwalimu halafu kesho unadai elimu bora kwa mwanao. Usalama wa taifa semini sasa basi tumechoka kuzulumu watu wetu na ndugu zetu, semeni tunataka kufanya kazi kwa heshima na mujibu wa mafunzo yetu.
Polisi, chokeni: wamefikia mahala sasa wanaowaona vikaragosi, kila mwenye shati la kijana anawaona hamnazo, matusi yamekuwa chakula chenu. Wanawatumia pale wanapotaka kama taulo, wanawatumia pale wanapotaka kama choo. wakisha maliza haja zao wanawatukana, hawajali maslahi yenu, mna maisha duni na ya kusonesha, hamna uhakika wa kesho. Msiposaidia kwenye wimbi hili la demokrasia na vita vya kiuchumi, matusi yataongezeka kwani mashati ya kijani yanawakumbuka tu kwenye kuiba kura.
Polisi kumbukeni ninyi ni sisi, tunaishi sote kwa taabu na familia zetu, kwanini mfie watu wasio wathamini. Simamieni haki semeni imetosha, jitokezeni wajasiri mtakumbukwa daima.
chief Mkwawa wa kalenga
Uhuru ni pamoja na kujua aliyekuweka utumwani