Kuhatarisha usalama wa Taifa? Give me a Break!

Kuhatarisha usalama wa Taifa? Give me a Break!

Mtazamaji nimeipenda hii analysis yako.....ila kwenye hizo kazi za CIA ni kwamba tungependa TISS wafanye hivi...... lakini tatizo Tanzania patriotism/uzalendo umeenda na Mwl Nyerere....sasa hizi ni ufisadi tu...ukiwa na hela, ukiwa na nyumba ukiendesha gari zuri ndio kitu....oh, bila kusahau ukiwa usalama wa taifa (hata kama hufanyi kazi ya maana).

Ila mi nitaendelea kuuliza mpaka tujue, naamini Usalama wa Taifa au jamaa zao wakaribu watasoma hii thread na kurekebisha panapohitajika.

Binafsi kama kuajiriwa na tasisi ningependa niajiwe kitengo cha Economic or Technological Intelligency sijui kama kipo ? Naamin kuwa Economi Intelligency officer wala hautaji kufanya kazi kwa siri


  • Ukipewa Desk kwenye Office ya Ubalozi wa Tanzania China kazi inakuwa kukusanya data may bekwa kwa nn china inanua chai ya Brazil na sio tanzania.
  • Mchumi yeyoye akipewa Desk Kwenye Ofisi ya South africa unatafuta data ni makampuni gani ya nje yanayonunua Tanzanite kupitia South africa na kwa nn yasinunue moja kwa moja Tanzania? Hii sio kazi ya siri.
  • Wafanyabiashra na makampuni ya dhahabu makubwa ni ya waisrael. Kwa nini tanzania haina uhusiano wa moja kwa moja na israel? Je ni kwa manufaa ya taifa au ni sababu za kisiasa zaidi? Unaweka vikwazo kwa muwekezaji halisi musirael matokeo yake tunapata wawekezaji second class wa South africa. Tunashangaa kenya inauza dhahabu kuliko au iko sawa na Tanzania
Utagundua Tanzania ina waambata wa kijeshi kwenye mabalozi kama south africa. Hii inaonyesha Inteligency priorities zetu si tu haziendani na wakati bali pia ni wrong. Kwa nini hatuna waambata wa kiuchumi au Kiteknolojia wenye majukumu kwenye sekta hizo. Kwenye Ubalozi wa south africa, Japan, China lazima kuna waambata wa kichumi wanatuma data za kichumi za Tanzani zenye manufaa kwa nchi zao na wawekezaji wao.

Sina utaalamu wa mambo ya ubalozi lakini je role na resposibility ya mwambata wa kijeshi ubalozini South africa na nchi nyingine ni nini? Kwa nini msisitizo usiwe tofauti?

Kama wapo watu wa system na kuna hivi vitengo vya uchumi na tekonolojia ningependa niwe 1ja wao.
 
DERIMTO.
nimekusoma vyema na ninakubali kuwa kazi hiyo ni ngumu. ila inapaswa uzalendo uweke mbele.

Mtu huruhusiwa kujiunga endapo amefikisha miaka mingapi? na anakosa sifa za kuajiriwa akiwa umri gani???
 
Ni watumishi wenye mzigo mzito wakuwa Waaminifu, Waadilifu na wapimaji mambo kwa kina cha ajabu ambao hawatarajiwi kuitikia kila sinema ijitokezayo usoni mwao wanasiasa na makundi yenye ushawishi fulani katika kutekeleza jukumu lao la msingi la kulinda MASLAHI YA UMMA wa Tanzania kwa usiku na mchana, period!!!!

Lakini, endapo chombo kama hiki kitaanza kukumbatia itikadi nyinginezo na maslahi BINAFSI na kuzifanya kuwa ndio nguzo, mhimili na kitovu kinacho waelekeza ndugu zetu hawa wafanye vipi kazi walizopewa na walipakodi, basi watajikuta wakiua watu kiholela kuliko hata nduli Iddi Amin wa Uganda kwa waendea 'maadui wa kuchonga' pindi watu kama hao wanapojaribu kutetea kilicho cha kwao.
 
Habari,

Nimekuwa interested na mada iliyopo bandikoni, ila ningependa kufahamu kutoka kwa wana JF...

Jeshi la Ulinzi wa Taifa na Usalama wa Taifa nani superior kwa mwenzako? Kwasababu kwa mtazamo wangu ni kwamba they both play vital roles in the security of our nation.Kuna mtu mmoja ni mechanic ktk garage ya kaka'ake inayotengeneza gari za Ikulu, so the guy kind of shows of kuwa yeye ni UWT, anatembelea GX 100 ambayo windscreen haija bandikwa chochote, alichowahi kunikera ni kwamba alikuwa ananishawishi nijiunge na Police ila nikamtania kuwa its better nijiunge na TPDF but jamaa akaniambia wanajeshi ni WAS*NGE! I was a bit infuriated...

Naomba mnifahamishe nani ni nani?Tafadhali
Kwa uelewa wangu mpaka sasa hivi ni kwamba TPDF ni walinzi wa nchi kwenye mipaka na nje......almost like POLICE, ila police wao ni walinzi wa ndani ya nchi.

Usalawa wa Taifa ni walinzi wa viongozi tu.....zaidi ya kulinda viongozi kazi yao nyingine ni kufanya utafiti na kuwashauri viongozi..

Kwa hiyo kwenye nani zaidi, mi nadhani majenerari wanawatoa hawajamaa noki vibaya sana.
 
Oh, na pia, police wana wizara ya mambo ya ndani

jeshi lina wizara ya ulinzi

usalama wa taifa hawana wizara, wao ni ki-department (idara) kwenye ofisi ya raisi.

ni kama vile CIA na US Army
 
Chifunanga nimekusoma,pia Derimto umesomeka...I believe hizi pillars za security whether external or internal zinategemeana kwasababu kama Derimto ulivonijuza kuwa hata Jeshini watu wa UWT wapo ni imani yangu kwamba wanaenda sawa.

Kuna Colonel mmoja niliwahi kumuuliza hilo swali akanijibu simply,"wale watu tunaheshimiana,wapo kwetu na pia tupo kwao" quite an answer right?...Sikuwa na further questions on that matter
 
Kuna kila sababu kwamba hii nchi inatafunwa na hawa wanaojiita usalama wa taifa kwasababu kila jambo linalotokea hapa nchini wao kwa njia nyingine watakua wameshiriki

Mifano:-
Kikwete- sidhani kama huyu mweshimiwa anakosa lolote inawezekana hawa jamaa michongo yote wanatumia migongo ya watu na wao kujiweka pembeni.
-Aiwezekani kitu chochote kufanywa na rais bila kupata prove ya hawa wanausalama hata hotuba zake lazima zipitie kwao then ndio inaidhinishwa kwenda kuitumia.
-Hapa nchini kampuni zote zile zilizokua chini ya serikali hata hizi za kigeni walijipenyeza uko na kushika vyeo kama vya u CEO walikua wao kwenye kampuni za serikali na ndio maana zilikufa kwa ufanisi mbovu aidha rushwa na kadhalika
-kipindi cha nyerere wengi wao walikua standard seven ila walijitaidi kujisomesha ili kuja kushika atamu
-Wana JF ccm aiweza kufanya kitu bila wao kukubali wakifanye na baadhi yao ndio walishakula kiapo na wakigeuka malipo ni kifo.
-Je?ulishasikia bajeti yao hata siku moja? au mkurugenzi wao nani anamjua?
-Na kwa taharifa tu any government organisation start from CEO ni lazma awe kachero(mwana husalama)
-Kwao ukiwa mwerevu sana basi utajengewa propaganda ili mradi usipati nafasi stahiki
- wanachoitaji sana mtu mbumbumbu ili wamcontrol or mtu wa ndio mzee wao kwao ni super kama mkuu wetu wa nchi
-Ninashangaa na kujiuliza kila mara kwanini wale watu vichwa kama kina Sita, Mrema,Magufuli, Mwakyembe, Slaa kwao ni mwiba? ni kwasababu wanajua akiwa mtu makini pale juu basi awataweza kumtawala kama alivyo kuwa nyerere na mambo yao yatakua hayaenda
-Inawezekana sana rushwa haitaisha na ufisadi cause wao ndio #1 kwa kuifilisi hii nchi na mikataba mibovu ya nchi.
-Namaanisha kwamba hata inawezekana kuwa CCM ni chambo tuu ila wahusika ni wao ila ni lazima wapitie mgongo wa chama ili wao wawe na amani
-Bila wao CCM isingeshinda na ukifuatilia sana hata rais ni wao wanamchagua na baya zaidi wanamchagua mtu atakayefuata matakwa yaho na wale wenye sifa ni adui kwao
-Ni kitu gani kitakachofanyika hapa nchini bila wao kujua? hizi propaganda zinazoenezwa nchi nzima kufuta hoja za msingi ni wao wanafanya na kuziandaa
-Wao ndio waliofikisha hii nchi hapa ila kwa kupitia mgongo wa CCM ndio maana tunakilaumu chama bila kujua mizizi halisi ni akina nani.
wana JF anayejua zaidi atufahamishe.
 
Tunaposema tunataka mabadiliko, tunajumuisha na system yote ikiwemo idara hii nyeti. Mengine uliyotaja nilikuwa siyafahamu, kweli yamezidi kunitisha kama ni hivyo.
 
kwani hawa usalama wa Taifa wa nchi yoyote ile wao wanaongozwa au wao ndio wanayoingoza nchi,hivi raisi hata kama akiwa mpinzani atawafanya nn?
 
Tunaposema tunataka mabadiliko, tunajumuisha na system yote ikiwemo idara hii nyeti. Mengine uliyotaja nilikuwa siyafahamu, kweli yamezidi kunitisha kama ni hivyo.

Nakumbuka wachezaji wa mchezo wa utamaduni wa mganda maarufu huko kando ya ziwa nyasa na malawi, hali kadhalika chihoda kwa wanawake. Kuna mtu wa makamu au mzee anayezungukia wachezaji muda wote, nikauliza mtu huyu kazi yake nini? Nikajibiwa anaitwa lifuma, na kazi yake ni mlinzi wa mazingira kwa wachezaji. Kama mtu anataka kuwadhuru wachezaji kwa siri kimazingira basi huyu ni mwonaji anaona na kumwondoa mbaya huyo. Ila wabaya hao huwezi kuwaona kwa macho ya kawaida ila tu kama umepata dawa pekee wanayotumia hawa ili kuona mazingiri sirini wanaofanya uovu kwa siri wasionekane kutokana na kupakaa dawa inayoficha macho ya kawaida wasionekane.

Niliduwaa na kushangaa kwamba ndo yanayoendelea tuwaonapo hawa walinzi wa mchezo wa mganda?
Labda na hawa wa usalama wa taifa ndo kazi yao? :majani7:​
 
Usalama wa Taifa na changamoto mpya

Evarist Chahali

Machi 30, 2011

Wakati umefika iache kuwa kitengo cha ushauri cha CCM

KILA mwisho wa mwaka, jarida maarufu duniani la TIME (la Marekani) huwa na utaratibu wa kumtangaza "mtu wa mwaka" (Person of the Year). Mwaka 2004 tuzo hiyo ilikwenda kwa Rais wa zamani wa Marekani, George W. Bush.

Katika mahojiano yake na jarida hilo, Rais Bush alitoa kauli moja ambayo kwangu imebaki kuwa nukuu muhimu. Kwa kifupi, alieleza kwamba ukisema kitu au kutenda jambo, na kisha wakajitokeza watu kukupinga au kukuunga mkono, basi, kwa vyovyote vile ulichosema au kutenda kimewagusa wanaopinga au kupongeza. Maana; kama kisingewagusa, wasingepoteza muda wao kukupinga au kukupongeza.

Katika Raia Mwema, toleo la Oktoba 13, 2010, kulikuwa na makala yangu iliyohoji iwapo tuhuma zilizotolewa na aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, kuwa Idara ya Usalama wa Taifa inamhujumu zinaweza kuwa kweli au la.

Makala hiyo iliyobeba kichwa: Ni kweli mashushushu hutumiwa kuhujumu uchaguzi? ilimuibua msomaji mmoja aliyejiita Almasi Kajia ambaye aliijibu makala yangu kwa kueleza kuwa "kazi ya mashushushu ni usalama si kuhujumu uchaguzi".

Kwa kuzingatia ‘hekima' za Bush, kuibuka kwa Kajia kujibu makala hiyo kunamaanisha aliguswa. Sasa kama aliguswa kama mzalendo au mtu mwenye maslahi kwenye taasisi hiyo, si suala la msingi.

Awali, sikutaka kumjibu lakini ukimya wangu wa muda mrefu ungeweza kuleta tafsiri potofu kuwa niliafikiana na utetezi wake kwa taasisi hiyo nyeti nchini mwetu.

Kwamba jukumu kuu la Idara hiyo ni usalama, hilo halina ubishi; kwani hata jina lake linaashiria hivyo. Lakini hata kazi ya askari wa usalama barabarani ni kuhakikisha usalama barabarani. Lakini, Kajia na wengine wote, tunajua namna trafiki wetu walivyogeuka ‘mamlaka ya mapato kwa njia ya rushwa'.

Hoja yangu hapa ni kwamba taasisi kuwa na jukumu fulani haimaanishi kuwa lazima inatekeleza jukumu hilo ipaswavyo. Na ni katika namna hiyo hiyo Idara ya Usalama wa Taifa kuwa na "kazi ya usalama" haimaanishi kuwa wanatekeleza jukumu hilo kwa ufanisi; japo si tu wanapaswa kufanya hivyo; bali lazima wafanye hivyo.

Si siri kwamba kushamiri kwa ufisadi Tanzania ni dalili za wazi kuwa taasisi hiyo haitekelezi wajibu wake ipaswavyo. Licha ya kanuni ya usiri kuendelea kuisadia idara hiyo kuogopwa na wengi, ikiwa ni pamoja na baadhi ya mafisadi, kadri siku zinavyokwenda ndivyo taasisi hiyo inavyozidi kuonekana kama ‘mbwa asiye na meno'.

Idara ya Usalama wa Taifa haina sababu yoyote ya msingi ya kuiacha Tanzania ikielekea kusikoeleweka.Watumishi wa idara hiyo wanatimiziwa kila hitaji lao la kuwawezesha kufanya kazi kwa ufanisi.

Lakini hiyo haikuweza kuzuia ujambazi wa EPA, utapeli wa Richmond, mazingaombwe ya Dowans, na mengineyo yanayofanya ufisadi kuonekana kana kwamba ni kipengele muhimu kwenye Katiba ya nchi yetu.

Tatizo la msingi la chombo hiki muhimu lipo kwenye kuishia kushauri tu. Wanakusanya taarifa, wanazichambua, na kisha wanashauri. Basi. Lakini hata ushauri wao ukipuuzwa,wao wanaona wameshatimiza wajibu wao.

Taasisi hiyo inafahamu fika kuwa popote pale ilipo, kuna nyakati inalazimika kulazimisha ushauri wake ufuatwe kwa maslahi ya Taifa. Wanajua sana namna ya kulazimisha ushauri wao ufuatwe kwa maslahi ya Taifa, lakini kwa sababu wanazojua wenyewe wameendelea kuridhika na nafasi yao ya ushauri tu.

Binafsi, naamini kuwa kama idara hiyo ingeamua kwa dhati kutimiza wajibu wake ipaswavyo, hii hali ya sasa ya kukithiri kwa ufisadi nchini, ingekomeshwa. Sambamba na hilo, viongozi wasio na uwezo wala maadili ya uongozi wasingejipenyeza hadi ngazi za juu za uongozi nchini.

Maana; ikiamua, idara hiyo inaweza kabisa kukabiliana na majambazi walioingia kwenye siasa kwa lengo la kukwangua kila raslimali ya nchi hii. Yote hayo yanawezekana iwapo kanuni za asili na taratibu za utendaji kazi zitafuatwa ipaswavyo, na kuweka kando ‘uswahiba'.

Tuwe wa kweli. Hivi kama Idara ya Usalama wa Taifa inatoa ushauri mzuri, lakini unaishia kupuuzwa, si kwa vile una mapungufu, bali unakwaza maslahi ya kundi fulani, kwa nini mbinu nyingine zisitumike kuwashughulikia wahusika?

Kuwa na rundo juu ya rundo la mafaili kuhusu fisadi fulani; huku fisadi huyo akizidi kuikongoroa nchi, ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.

Lakini tatizo jingine linaloiharibu taasisi hii nyeti ni kuendelea kwake kuwa kama ‘Kitengo cha Usalama cha CCM '. Majambazi wa kisiasa na kiuchumi wanafahamu ukweli huo, na ukaribu wao na chama hicho - kama wafadhili au viongozi unawapatia si tu hifadhi; bali pia ukaribu na idara hiyo.

Tatizo hili ni la kihistoria na kiuongozi zaidi. Kihistoria, kwa vile katika zama za mfumo wa chama kimoja, taasisi hiyo ilikuwa ni chombo muhimu katika utendaji na ustawi wa chama tawala. Mageuzi katika mfumo wa siasa yaliyoruhusu mfumo wa vyama vingi yaliharamisha vyombo vya dola kujihusisha na siasa. Kwa bahati mbaya, haramisho hilo limeendelea kuwa la kinadharia zaidi kuliko kivitendo.

Kadhalika, kikatiba, Rais ndiye ‘mlaji' mkuu (consumer) wa taarifa kutoka Idara ya Usalama wa Taifa. Hadi hapo, hakuna tatizo. Lakini Rais huyo huyo ndiye Mwenyekiti wa CCM. Sasa kwa vile siasa zinapewa kipaumbele zaidi ya maslahi ya Taifa, uwezekano wa CCM kuitumia idara hiyo kupitia nafasi ya Rais kama Mwenyekiti wa chama hicho, ni suala la wazi kabisa. Hilo si tatizo tu; bali ni jambo la hatari hasa kama itatokea nchi kuangukia mikononi mwa rais dhaifu kweli kweli.

Lakini laiti maslahi ya Taifa yangewekwa mbele ya maslahi ya kisiasa, pengine isingekuwa vigumu kwa taasisi hiyo kuhakikisha rais hatumii "kofia zake mbili" kukinufaisha chama chake kwa sababu, kwa kiasi kikubwa, maisha ya kila siku ya rais yapo mikononi mwa taasisi hiyo.

Kiungozi, teuzi nyingi za viongozi wa taasisi mbalimbali zimekuwa zikielemea zaidi kwenye maslahi binafsi ya anayefanya uteuzi badala ya uwezo wa wateuliwa au manufaa kwa umma. Matokeo yake ni wateuliwa kuwa wanyenyekevu kupita kiasi kwa aliyewateua; huku wakiendelea kujiona wadeni wa fadhila kwa kuteuliwa huko.

Teuzi zinazofanywa kwa misingi ya urafiki zinasababisha hali ya kulindana. Hali huwa mbaya zaidi katika mazingira ambamo mteuliwa anafahamu "machafu" ya mfanya uteuzi, na uteuzi huo unakuwa wa ‘kulinda kopo la uozo lisifunguke'.

Laiti tungekuwa na mfumo wa uwajibikaji ambapo watawala katika ngazi mbalimbali hawakurupuki tu na kuamua fulani awe fulani, mambo yasingekuwa hovyo kama yalivyo hivi sasa.

Katika ngazi za juu, pengine yafaa jina la mteuliwa kupelekwa Bungeni na "wawakilishi wa umma" wakauwakilisha umma kumpitisha au kumkataa mteuliwa aliyependekezwa. Kama ili mtu aajiriwe, japo kuwa mesenja tu ni lazima afanyiwe usaili, iweje basi watu wanaokabidhiwa majukumu makubwa kabisa na nyeti kama ya kuongoza Idara ya Usalama wa Taifa, wateuliwe na rais tu?

Nimalizie kwa kuikumbusha Idara yetu ya Usalama wa Taifa kwamba angalau hadi sasa bado ina heshima kidogo miongoni mwa Watanzania wengi. Lakini heshima hiyo inamomonyoka kwa kasi kwa jinsi inavyoshindwa kukabiliana na ufisadi unaootesha mizizi nchini. Sababu zipo nyingi tu kwa idara hiyo kuanza kujitazama upya.


Blogu: KULIKONI UGHAIBUNI

Kiungo: http://www.raiamwema.co.tz/news.php?d=3055
 
.... analogy: ... kama yaliyojiri UK hadi kuanzishwa kwa GCHQ miaka ilee na masharti ya kuajiriwa mle
 
Tatizo ni la kimfumo na ambalo limefumbiwa macho kwa muda mrefu sana. Mara zote shughuli za idara hii zinaendeshwa kwa siri. Ni kwa siri kiasi kwamba hata baadhi ya watendaji wa idara hii hawajui ni nani mkurugenzi wa idara au hawajawahi hata kumwona. Lakini kwa upande mwingine ni kuwa idara imekuwa ikibeba sura na utashi wa rais aliye madarakani.

Kila rais akija anamleta mkurugenzi atakaemsikiliza. Na ni katika hili ndio hasa uelekeo unaanza kubadilika.

Policy za idara haziko wazi, watendaji wanasikiliza maelekezo ya mdomo zaidi na hayazingatii policy.

Kama wanavyotegemea kila kiongozi atakaeingia madarakani atabadilisha safu za utendaji wa juu ndivyo hivyo hivyo wanajipanga mara zote kuhakikisha wanawatumikia wanasiasa (waajiri) na sio usalama wa taifa. Taaluma yao inategemea sana wanasiasa,na ndio wanaowatumikia. Hadi tutakapopata viongozi wanaojiamini, ambao wataingia kuwatumikia watanzania na sio matumbo yao na ya marafiki zao. Hadi tutakapopata viongozi waliosimama, ambao mtizamo wao ni kujenga nchi iliyo imara na taasisi zilizo wazi na zinazojitegemea.
 
Kwanza kabisa hii thread iko juu sana. Lakini nimekuwa nikijiuliza nani hasa ni mteja wa usalama wa taifa. Raisi au Umma? Huu ni usalama wa viongzi au Taifa? na tunaposema taifa tuna maana gani.

Nimeuliza hayo ili tuweze kuliangalia kwa makini zaidi swala la kukosa mwelekeo.
Kuna aina ngapi za vyombo vya namna hii.:redfaces:
 
Hii Idara ni uhai wa nchi, kwa maana ya usalama na ina vijana wengi sana wazalendo ningependa wajitokeze sasa na kusema wanataka muundo wa idara uweje? Sisi tulio nje hatujui inavyofanya kazi, mimi huwa nawaona ona tu wengine wanabrand in kama raia na wengine tumesoma nao, na mambo yao yapo yapo tu.

Hii idara haipashwi kuwa chini ya mtu mmoja inapashwa iwajibike kwa rais sawa lakini akimshirikisha Spika wa Bunge au Jaji Mkuu au wote kwa pamoja kuondoa matatizo ya sasa, na pia wapewe uwezo wa kukosoa uteuzi wa viongozi wa nchi hii.
 
Tatizo ni la kimfumo na ambalo limefumbiwa macho kwa muda mrefu sana. Mara zote shughuli za idara hii zinaendeshwa kwa siri. Ni kwa siri kiasi kwamba hata baadhi ya watendaji wa idara hii hawajui ni nani mkurugenzi wa idara au hawajawahi hata kumwona. Lakini kwa upande mwingine ni kuwa idara imekuwa ikibeba sura na utashi wa rais aliye madarakani.

Kila rais akija anamleta mkurugenzi atakaemsikiliza. Na ni katika hili ndio hasa uelekeo unaanza kubadilika.

Policy za idara haziko wazi, watendaji wanasikiliza maelekezo ya mdomo zaidi na hayazingatii policy.

Kama wanavyotegemea kila kiongozi atakaeingia madarakani atabadilisha safu za utendaji wa juu ndivyo hivyo hivyo wanajipanga mara zote kuhakikisha wanawatumikia wanasiasa (waajiri) na sio usalama wa taifa. Taaluma yao inategemea sana wanasiasa,na ndio wanaowatumikia. Hadi tutakapopata viongozi wanaojiamini, ambao wataingia kuwatumikia watanzania na sio matumbo yao na ya marafiki zao. Hadi tutakapopata viongozi waliosimama, ambao mtizamo wao ni kujenga nchi iliyo imara na taasisi zilizo wazi na zinazojitegemea.
Hii inanichanganya; inakuwaje kwenye usalama wa viongozi na maslahi yao wako very smart. Lakini inefficient kulinda usalama wa watu binafsi wanaoonekana wazalendo? You could always evaluate impacts thru outcome, hapa inaonekana usalama wawahujumu uko vizuri sana kiasi sijawahi sikia wahujumu wakiwa na wasiwasi na maisha yao huku uhujumu wao tunauona hadi huku kwenye visible world. Sasa ni vipi usalama wa wale wanaoonekana kupinga hivi vitu visible kwenye jamii unakuwa hatarini na wakati mwingine evidence zipo wengine wamepoteza maisha yao. Je huu kweli tuuite usalama wa taifa?

Kama ni kujua ulinzi sina shaka kwani hakuna fisadi hata mmoja ambaye amepoteza maisha na naamini raia wengi hawawapendi mafisadi, hii inanionyesha its not easy to contact them kwani wako very secured so hii inathibitisha wanajua kulinda ila tatizo wanalinda nini na nani? Wheter mnawalinda ama mnatulinda jueni kuwa dhambi yenu ni kubwa kwa muumba. Kwani kwakutolinda maslahi ya Taifa mnasababisha vifo vingi vya watoto, wamama wanaokosa huduma wakati wa kujifungua, wasafiri wanaokufa kwenye ajali kwaajili ya poor public transport such as barabara mbovu; wanafunzi wanao drop out from school kwaajili ya kukosa ada na malezi ya familia kwani ndoa nyingi zimevunjika kwa sababu ya economic reasons.

I find your works to be very evil I wish you can read this and see how you are actually killing and not protecting and yet you are getting paid the basics and even in excess ili tu muweze kufanya kazi yenu vizuri. Hamwezi kuwapa uzima mafisadi kwani tayari wengi wao wako at dying stage ndiyo maana walipanga foleni za kwenda Loliondo. Yes I also will die but better i die physically and live forever in eternity for I do believe this and what I am actully doing is part of my purification kwani nawaona kwa macho yangu matunda yenu yalivyo maovu hivyo nikinyamaza kwa kuwaogopa napalilia kifo cha milele. Lakini nikiwasema these words are going to live forever as witness that I atleast told you how evil your dealings are. Hate me or love acknowledge or refuse I remain a preacher!
 
Wakuu... Amani iwe kwenu!!
Nimekuwa nikijiuliza kwa nini mara nyingi serikali inafanya makosa mengi na makubwa dhidi ya sheria? Nikagundua hatimaye kuwa tatizo kubwa la nchi hii ni kule kuongozwa na Usalama wa Taifa.

Viongozi wa serikali (wanaotokana na CCM) hawaoni sababu ya kuwajibika kutokana na kwamba wana namna wanavyolindwa au kukingiwa kifua na Usalama wa Taifa.
Uvunjaji wa haki za binadamu na kupoka demokrasia kunafanywa kwa kinga ama ngao ya Usalama wa Taifa. Watendaji wa serikali na viongozi wa CCM wanatumia Usalama wa Taifa kulipa visasi dhidi ya mahasimu wao.

Ni imani yangu kuwa inawezekana serikali ya Kikwete ingekuwa inafanya vizuri kama ingekuwa sikivu na kuwajibika kwa wananchi bila ya kutiwa kiburi na Usalama wa Taifa na kufuata porojo za propaganda za Usalama wa Taifa.

Usalama wa Taifa wanajilinda na sheria inayowapa kutekeleza wajibu wao kwa ku-suspend sheria za nchi kuwabana wazalendo na kuwalinda waporaji wa utajiri wa nchi.

Hata hivyo Kikwete ajiulize kuwa kama dawati la mwisho la kutumia kwenye kupambana na kutokukubalika ni usalama wa Taifa je kwa wakati huu anapolitumia kuendesha nchi litakaposhindwa atatumia nini?

Sithubutu kusema wazi kuwa itabaki kutumia tu jeshi dhidi ya wananchi wake wenyewe kujibu maswali marahisi kabisa.

Eee Mungu ihurumie Tanzania.
 
Hahaha...bado mna miaka kama minne hivi ya kununa.
 
Hanuni mtu!! Hapa ni kazi mbele kwa mbele kama Tahrir Square hadi kieleweke
 
Back
Top Bottom