Katika siku za karibuni Idara ya Usalama wa Taifa imekuwa ikitajwa tajwa sana katika vyombo vya habari. Kutajwa tajwa kwa idara hiyo pengine kunatokana na malalamiko ya wananchi hususani viongozi wa vyama vya siasa kwamba wamekuwa wakifuatwa fuatwa na kutishiwa na maafisa wa idara hiyo kiasi cha kuamini kuwa maisha yao yako hatalini. Pia yamekuwepo malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kwamba idara hiyo imeshindwa kupambana na ufisadi, rushwa, biashara ya madawa ya kulevya na kuendelea kukua kwa tabaka kati ya matajiri na masikini.
Aidha katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, idara ya usalama wa Taifa ilipigiwa kelele sana kwa madai kwamba ilihusika kikamilifu katika kuchakachua kura zilizo muwezesha Rais Jakaya Kikwete kupata ushindi dhidi ya Dr Slaa. Tuhuma hizo zilikuwa nzito kiasi cha Naibu Mkurugenzi wa idara hiyo ndugu Nzoka kufanya mkutano maalumu na waandishi wa habari ili kukanusha uvumi huo. Hata hivyo, pamoja na maelezo mazuri ya mkurugenzi huyo, wananchi wengi bado wana amini mpaka leo kwamba maelezo hayo yalikuwa ni siasa na kujiosha tu lakini ukweli ni kwamba idara hiyo ilihusika katika uchakachuaji..
 [TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Rais Jakaya Kikwete
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 Mambo hayo kwa ujumla wake yamenifanya nijifunze mambo makuu matatu: Kwanza kabisa wananchi walio wengi hawaijui idara ya Usalama waTaifa. Hawajui shughuli zake, utendaji wake, na mipaka yake. Kuto kujua huko kuna wafanya wananchi kuifananisha idara hiyo na iliyokuwa idara ya usalama wa Taifa ya Uganda- Bureau of State Security (wakati wa Iddi Amini) ambayo ilihusika na mauaji na mateso ya raia wengi wa nchi hiyo; jambo ambalo si sahihi. Aidha, kuto ifahamu idara hiyo kunawafanya wananchi wengi wailaumu idara kwa mambo ambayo pengine haihusiki.
Pili, wananchi wengi hawajui tofauti kati ya Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) na Idara ya upelelezi wa makosa ya jinai (CID). Hali hiyo inawafanya wananchi wasiojua tofauti kuilaumu Idara ya Usalama wa Taifa na maafisa wake hata kwa makosa yaliyofanywa na askari wa idara ya upelelezi wa makosa ya jinai. Hata hivyo zipo nyakati ambazo idara hiyo hufanya makosa mbalimbali na hivyo inastahili kupokea lawama kwa makosa iliyofanya.
  [TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Mkurugenzi mstaafu Hassy Kitine
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 Tatu,IdarayaUsalama wa Taifa haifanyi jitihada za kuwaelimisha wananchi kuhusu muundo wa idara hiyo, majukumu yake na mipaka yake ili kuwafanya wananchi waielewe idara hiyo (wasiiogope), wawe karibu nayo na hivyo kushiriki kikamilifu katika utoaji wa taarifa za ki itelejensia kitu ambacho ni muhimu sana katika mafanikio ya kazi za idara hiyo.
Katika nchi zilizoendelea kama Marekani na Uingereza, Idara za Usalama wa Taifa hususan Central Intelligence Agence (CIA), National Security Agency (NSA), Secret Service, FBI za Marekani na MI 5 ya Uingereza huendesha programu maalum za kuelimisha umma ambapo huwafahamisha wananchi kuhusu kazi za idara hizo, mafanikio na 'challenges' ambazo idara hizo inakutana nazo katika utekelezaji wa majukumu yake. Proglam hizo huendeshwa katika luninga (TV) za Taifa, Radio mbali mbali na vijarida. Utaratibu huo unasaidia sana katika kuwafanya wananchi wazielewe idara hizo, waziheshimu na kuziunga mkono badala ya kuzichukia, na kuzi kashifu na hivyo kutoa ushirikiano mkubwa.katika kufanikisha kazi zake.
Katika kipindi cha utawala wa Mwalimu Nerere, Idara ya Usalama wa Taifa ilikuwa na proglamu za uelimishaji umma kama ilivyo kwa idara nilizo zitaja hapo juu ambapo maafisa wa idara hiyo walishiriki kutoa mafunzo kwa wana mgambo, vyuo vya siasa, makongamano ya viongozi na Jeshi la kujenga Taifa. Hata hivyo proglamu hizo zilidorola baada ya kuanza kwa mfumo wa vyama vingi kutokana na imani ya baadhi ya watu kuwa idara hiyo inafanya kazi ya kuwalinda viongozi wa CCM ili chama hicho kiendelee kubaki madarakani. Hivi sasa Idara hiyo hutoa mafunzo ya utunzaji siri tu kwa walimu wanaoteuliwa kusimamia na kusahihisha mitihani.
 [TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Naibu Mkurugenzi
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Ni kutokana na sababu hizo, pamoja na nyingine ambazo sijazitaja ndio maana nimeona ni vema niandike makala hii ya kuelimisha umma kuhusu idara hiyo. Makala hii itazungumzia muundo wa Idara ya Usalama wa Taifa, Majukumu yake na mipaka yake. Aidha makala hii itaeleza mafanikio ya idara hiyo na 'Challenges' ambazo inapambana nazo katika kutekeleza majukumu yake. Makala hii pia itachambua tofauti kati ya idara ya Usalama wa Taifa (TISS), Idara ya upelelezi wa makosa ya jinai (CID) na Idara ya usalama ya jeshi (Millitary Intelligence). Makala hii pia itaeleza jinsi wananchi wanavyoweza kuwa karibu na idara hiyo, jinsi ya kuweza kupata ajira katika idara hiyo na sifa zinazohitajika kwa waombaji.
Imetoka,
mwana dikala: Ijue idara ya USALAMA WA TAIFA (TISS)
ITAENDELEA.....
Angalizo:
Muandishi wa makala hii HANA UHUSIANO wa aina yoyote na IDARA ya Usalama waTaifa.