Ashasembeko
JF-Expert Member
- Dec 14, 2017
- 225
- 910
Ni kawaida nchini kwa kila kiongozi mpya anapoingia madarakani, kuwepo kwa genge la wanufaika wa uongozi uliopita kulinda na kusukuma maslai yao. Mwinyi – kama alivyoandika kwenye kitabu chake – alisumbuliwa sana na ‘watu’ wa Nyerere, ikiwemo Nyerere mwenyewe. Mkapa hakusumbuliwa sana na hili.
Kikwete alisumbuliwa kidogo na watu wa Mkapa. Magufuli alisumbuliwa kwa sana na watu wa Kikwete ambao maslai yao kwa upana yaliguswa na walihisi kutengwa.
Kuna dalili za wazi, Rais Samia, ameaza kusumbuliwa na watu wa Hayati Magufuli, na nina hofu mpango huu una maono ya 2025. Kama umekua ukifuatilia kwa ukaribu kwenye mitandao, kila changamoto inayotokea nchini, kuna kakikundi - ambacho ukifungua profile zao - utagundua wengi hawana followers zaidi ya 10, wanacomment, mambo yanayolenga kumlaumu Samia, na “kumkumbuka” JPM kwani mambo haya “hayakuwepo” wakati wa uongozi wake. Hizi accounts kitaalamu zinaitwa bots.
Naomba tukumbushane
Matatizo Tanesco; Ni kweli kuwa matatizo ya umeme yalipungua wakati wa JPM, ila hitilafu zilikua zinajitokeza mara moja moja, ila hawa watu wana comment kana kwamba huko nyuma mambo yalikwisha kabisa. Huu ni upotoshaji wa maksudi. Mifano ya hizi hitilafu huko nyuma soma hapa, hapa na hapa.
Ujambazi; Kama ilivyo maswala ya umeme, ujambazi ulipungua kwa sana ila ulikuwepo. Soma hapa, hapa, hapa, hapa na hapa. Ipo mifano mingi, tafuteni kwenye mitandao. Ninajaribu tu kuwakumbusha maana watanzania ni hulka yetu kusahau. Kwa kuongezea wakati wa JPM ujambazi wa kihalifu ulipungua, lakini ujambazi wa kisiasa ulishamiri. Wanasiasa kupigwa risasi, wafanyabishara kutekwa, wengine kukatwa masikio, ila sisi watanzania kama kawaida ni wasahaulifu.
Sasa, anapokuja mtu kusema wakati wa JPM haya mambo hayakuwepo anakuwa na maana gani? Maana ni upotoshaji wa wazi. Ushauri wangu kwa Rais Samia, awe makini na usalama wake wa taifa na baadhi ya watu wake ndani ya uongozi.
Kuna watu wa JPM walioupata utajiri mkubwa katika uongozi wa JPM na wanajiaribu sana kutumia utajiri huo kuregain influence yao katika serikali. Kiufupi wanakujaribu na kujaribu kukukwamisha uonekana mbaya kwa watanzania.
Kama alivyofanya JPM wakati wa Kikwete, na wewe isuke team ya watu unaowaamini, hususani kwenye Usalama wa Taifa ambapo Magufuli alijaza wasukuma wake. Huyo Mkurugenzi wa Usalama unamwamini? Anafanya kazi kwa niaba yako au niaba ya genge la JPM? Najua upo karibu sana na Mabeyo, kaa nae mshauriane mnaisuka vipi usalama, hiki ndio chombo kitakachodetermine mafanikio ya uRais wako.
All the best!!