Shanily
JF-Expert Member
- Nov 4, 2024
- 856
- 1,662
Kuna msemo maarufu hasa huku mitaani kwetu watoto wakike wakiwa wanapigana au wanagombana na watoto wa kiume, utaskia wazazi wao hasa wa kike.
"Usipigane nae, huyo ni mwanamke"
Kwahy kama akiwa ni mwanamke hafai kupigana!?.
Binafsi naona kauli Bora ni kuwaambia "acheni kupigana, ugomvi sio Mzuri".
Maana ukimwambia mtoto wako wa kiume "usipigane nae , huyo ni mwanamke", unamjengea tafsiri kwamba.
a). Wanawake ni viumbe dhaifu hivyo hawafai kuwekewa uzito , wanafaa kupuuzwa.
b) Mwanamke hana hadhi mbele yake, ndomna hafai kugombana nae. Ndo utakuta kijana kakuwa , kaoa , unaskia anakwambia
"Utanambia nini , wewe si mwanamke tu".
Kashajenga fikra kwamba wanawake si lolote si Chochote.
Lakini tukisema " usipigane ugomvi sio mzuri, anajenga fikra ya jumla, ugomvi sio mzuri kwa wote, wake na waume na Kila mtu anastahili heshima yake.
Au hata tukisema hiyo usipigane nae, huyo ni mwanamke angalau ufafanue asipigane na mwanamke kwasababu gani!?. Ukiacha bila ufafanuzi ndo inaleta shida ukubwani, kwakua mazoea hujenga tabia.
Mwanaume hafai kupigana na wanawake, dhana ya kwanini ni muhimu kwa wazazi kuifafanua ili vijana wakue wakiwa wanaielewa.
a) Wanawake wanafaa kuhurumiwa.
b)Wanahitajia kuelezwa kwa upole.
c)Asili ya miili Yao haiwezi kuhimili kupigana mingumi , miteke.
Tuziweke wazi hizi sababu na nyinginezo kwa vizazi vyetu ili kutojenga dhana ya dharau na kumchukulia mwanamke kama kiumbe dhaifu hata wa fikra.