Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,186
- 7,492
iko hivi;
Dunia kwa asili yake kila kitu kimeumbwa na kinyume chake.Kushoto na kulia, fikiria kusipokuwa na kushoto utajuaje kulia?Nyuma na mbele, unajua nyuma kwa sababu kuna mbele, sio?Urefu ufupi, fikiria kama hakuna ufupi utajuaje urefu?Juu na chini?
Au fikiria; Giza mwanga, Ili ujue mwanga lazima pia kuwe na giza sio? Fikiria dunia ikawa ni mchana tu au mwanga tu hakuna giza?Baridi na joto, fikiria baridi bila joto? Mvua bila ukame je? Wanawake bila wanaume? Moto bila Maji je? N.k Fikiri siku kuwe na wanaume tu bila wanawake au wanawake bila wanaume, sasa wanaume hao watajuaje kama ni wanaume au wanawake watajuaje kuwa ni wanawake?
Ni kwa msingi huo ambapo “Law of polarity” imejengeka kwamba kila kitu kina kinyume chake na vitu hivyo haviko kwa ajili ya kusuguana na kumalizana bali kujaziliziana "Complements" japo inawezekana ikatokea wakati joto likawa kali hadi linakera ila baridi nayo ikiwa kali sana tunatamani joto na vikikutana katikati hapo inakuwa sawa.
Hakuna namna ambayo watu wawili wanaweza kuwa na mawazo yanayofanana kwa kila kitu ikiwa wote wanafiri. Ukiona wanafanana, ujue mmoja kaamua kutofikiri, au kaaamua kuwa mnafiki jambo ambalo ni hatari. Suala la msingi ni kuweka mfumo ambao kutofautiana huko kwa mawazo hakuwezi kuzua matatizo lakini watu kufikiri tofauti ni jambo la kimaumbile. Moto unaweza kuchoma nyumba lakini pia moto hupika chakula. Kwa hiyo moto tunauhitaji japo inabidi kuweka mazzingira rafiki ambapo hauwezi kulipuka na kuleta madhara.
Niwashawishi wale wenye kufikiria kwamba kufa au kuuawa kwa upinzani ni jambo jema wafikirie tena usahihi wa mtizamo huo kwa mantiki ya hoja hii.
Asante wote kwa kuelewa na kutoa michango safi kujenga uelewa zaidi.