Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,236
- 10,774
Wiki hii gumzo mitandaoni limechochewa na hatua ya TAWA pamoja na TANAPA kumkataza kijana maarufu wa mitandaoni, Jose Mlavichwa, kuendelea kupost video zake akila vyakula vya asili kama Kenge, konokono na viumbe wengine wa porini.
Wapo wanaohoji: “Hivi kweli kenge na konokono mtu akila ni kosa kubwa zaidi ya kuwapa vibali wageni kutoka Ulaya na Marekani kuwinda mamba, simba au kuzuia makundi ya nyumbu Serengeti?”
Ukitazama hoja ya TAWA na TANAPA ni kulinda taswira ya kitaifa na uhifadhi endelevu kwa maneno yao. Kwa mtazamo wao, kuruhusu video zinazoonyesha ulaji wa viumbe pori inaweza kuhamasisha uvunaji holela wa maliasili.
Hata hivyo, upande wa pili wa hoja unasema, kwa karne nyingi jamii za Kitanzania zimekuwa zikila vyakula hivi bila kuathiri ikolojia wala asili. Kwa nini leo kenge awe kiumbe wa “hadhi ya juu” zaidi ya kanga au bata? Yaani Kula Vichwa vya ng'ombe imekuwa ni kosa?
“Kumkataza kijana kama Jose ni kuua ubunifu na uhuru wa utamaduni. Hivi kweli kupiga marufuku kenge ni kipaumbele kuliko kushughulikia makundi ya wawindaji wanaowinda mamba ndani ya hifadhi ya Ruaha?” Je wakina Dudukwe na mwenzake Chaba wamepewa katazo hili?
TAWA na TANAPA wanapojikita kwa kijana mmoja wa mitandaoni, ni ishara ya kupoteza mwelekeo? Au kweli wanajaribu kusawazisha uhalisia na taswira ya taifa mbele ya dunia?
Je, Jose amekosea au ni mamlaka zetu ndizo zimetumia mkono mzito kupita kiasi? Wakati umma unahitaji majibu, msemo mmoja unabaki kuwa hai: “Haki bila mizani ni dhuluma.”