Kama Ni polisi alipwe hata milioni tano tu zinamtosha.
Hawa wajinga ndiyo wanaiweka CCM madarakani halafu linakuja kubwabwaja humu.
Kumbafu!
Tanzania tuna wajinga na wapumbavu wengi sana .
Ndio Maana CCM inatwala na Makonda anangara sana kuliko Mwanasheria Nguli Lisu . Yote ni Kwa Sababu ya Wanasiasa wapumbavu WASIOJUA nchi na Wananchi wake wanatawaliwa vipi na Nguvu ya Chama tawala Chini ya Katiba ya Mwaka 1977.
.
Hivi Polisi anaweza kubadilisha matokeo yaliyosomwa na Tume ya Uchaguzi ?
Hivi Mkurugenzi ámbaye ni Kada Wa CCM anapomtangaza Mgombea Wa CCM kuwa ameshinda Polisi anaweza akapinga na kumtangazia mpinzani.
Tuna Wanasiasa wapumbavu na wajinga sana ndio Maana CCM inafanya inavyotaka Kwa kuwanunua Wachache Kwa faida ya madaraka Ili wawaaminishe Wananchi kuwa aliyesabahisha mpinzani akashindwa ni Polisi.
Hivi kuna nchi Gani ambayo wanaodai Haki dhidi ya dhulma ya serikali wanaungwa mkono na Polisi. ?
Hata Marekani Kuna vikosi Vya kuzuia ghasia dhidi ya hasira za waandamanaji.
Kenya pamoja na Katiba Mpya lakini Polisi wanatawanya maandamano na kuzuia fujo . Halikadhalika Afrika Kusini n.k.
Jambo linalofanyaka ni Wapinzani kuwafundisha Kwa Udi na uvumba wawajue maadui wao wanaoimba rasilimali zao na kusababisha Umaskini Kwa walio wengi. Kwa nini Kwa Mfano Wapinzani wasiitishe maandamano makubwa Kupinga Kikokotoo na Kupinga wabunge na kupitisha muswada ya kujilimbikizia posho na mishahara kwenye nchi maskini Kama Tanzania?
Kwa nini Wanasiasa Wa CCM na Upinzani wanakwepa kuungana na Wananchi Kupinga Sheria kandamizi zinazowakandamiza wafanyakazi Wa Chini?
Kwa nini hatujawahi kusikia maandamano Kabla ya uchaguzi Kupinga Wakurugenzi na wakuu Wa wilaya makada Wa CCM watoke kwenye ofisi za umma.?
Wanasiasa wanataka tu Wananchi waandamane wao wanaponynganywa ubunge na udiwani ila Wananchi wakulima na wafanyakazi na wafanyabiashara wanapoumizwa na Sheria kandamizi Wanasiasa wanakaa mbali .
Bandari zimeuzwa, Loliondo kuna hujuma Iko pale miaka mingi sijawahi kusikia maandamano ya Kupinga dhulma na kuuzwa Kwa rasimali za umma kiholela na Kwa masharti yanayolipa taifa hasara.
Sasa mnataka Polisi Wawaambie andamaneni ?
Hakuna serikali Duniani inayopenda maandamano.
Na hakuna Katiba ya kiimla inayoondolewa kirahisi eti Kwa kukaa na kuomba kibali Cha maandamano na kutegemea Polisi iwaunge mkono.
Haki haiombwe Bali inadaiwa kama deni.
Polisi SIO ya CCM pekee lakini viongozi wake wanateuliwa na Mwenyekiti Wa CCM.
Majaji ambao ndio Wenye dhamana kubwa ya Haki nchini lakini pia wanateuliwa na Mwenyekiti Wa CCM na kisha kupewa maslahi makubwa yanayowafanya waanze kuionja Pepo wakiwa Duniani halafu utegemee kuwa watasimama na Wapinzani legelege wasiotabirika Wala kuaminika.
Wapinzani waliojawa na chuki na wivu Kwa Kila mtu. Mwabukusi amejitolea kuitisha maandamano lakini viongozi Wa chama kikubwa kama Chadema wakawakataza wanachama wao wasiandamane kumuunga mkono. Wivu tu wakuona kuwa Mwabukusi atapata umaarufu kuliko wao. Ujinga mtupu.
Huyo Polisi mmoja ameamua kuonyesha hisia zake na kukerwa na dhulma ya serikali ya chama tawala Badala ya kutumia Nafasi hiyo kumuunga mkono Ili wafanyakazi wengine wainuke Kupinga cha ajabu watu wale wale wanaojifanya kuwa wakiingia madarakani watajali maslahi ya watumishi Wa umma wanamkejeli ,CCM inazidi kujaa kiburu mana haioni chama ambacho kimesimama na Wananchi.
Ukweli ni ukweli tu Hata ukisemwa na Shetani Bado unakua ukweli.
Ni kweli Kabisa kuwa MTU aliyefanya KAZI miaka 32 hastahili kulipwa kiinuamgongo cha mil. 18.
Hata kama wanakula rushwa lakini SIO Sawa Kwa Sababu Kuna mawaziri na wakubwa wengi wanaiba mabilioni ya pesa ambazo ni Kodi za watu lakini Bado wanapewa kinwamgongo kikubwa. Hivyo Haki ya MTU isiingiliane na mitizamo ya watu.