y-n
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 2,389
- 2,510
Moja ya mchezo wenye changamoto nyingi sana hasa katika mchezo wa Soka ni mchezo wa "WATANI WA JADI" yaani Simba Vs Yanga.
Ni mchezo ambao unabeba hisia nyingi sana kwa wanamichezo kuanzia washabiki,wachezaji,makocha na wadau wote wa timu husika na timu mbalimbali shiriki.
Katika mchezo kuna matukio mengi sana ambayo machache yanaweza yakaonwa na mwamuzi na kuchukuliwa hatua na mengine mengi sana mwamuzi anaweza asiyaone na yakaonwa na watazamaji wengine hasa wa kwenye TV,hii ni kutokana na picha za marudio (Reply) zinazooneshwa.
Katika mchezo wa leo wa tarehe 29/04/2018 (Jumapili) ambapo timu ya Simba SC imeibuka na ushindi kuna matendo mengi sana yaliyotokea.
Moja ya kile kilichotokea ambacho kimenishawishi niandike haya ni mchezo/kitendo ambacho sio cha kiungwana kabisa (sio cha kimichezo) kilichofanywa na beki wa Yanga Kelvin Yondani kwa kumtemea mate mchezaji wa timu ya Simba.
Kiukweli ni moja ya kitu ambacho sio cha kiungwana kabisa kufanywa na mchezaji huyu hasa ukizingatia sifa ambayo Yondani amejijengea katika soka la Tanzania na hata nje ya nchi.
Ni kitendo ambacho labda mwamuzi hakukiona kabisa labda maana attention ya mpira ilikuwa ipo sehemu tofauti na kitendo hicho kilipotokea.
Ni wakati sasa wachezaji wazingatie michezo iliyo sahihi ili kufanya soka uwe mchezo wa kuburudisha kwa watazamaji wake.
Sheria ichukue mkondo wake dhidi ya vitendo kama hivi ambavyo si vya kiungwana vinavyotokea michezoni,TFF,inapaswa ichukue hatua kali sana ili iwe funzo kwa Yondani na wengine wote wenye tabia za aina hii.
Mwana_michezo