Kuhusu kitendo alichokifanya Kelvin Yondani dhidi ya Asante Kwasi

Kuhusu kitendo alichokifanya Kelvin Yondani dhidi ya Asante Kwasi

Amini hujui usemacho
Haya taja mwenye nidhamu utuambie tumfananishe na mpira wa asia au America
Unafananisha mpira wa Ulaya na Tanzania waendelee kuwa na nidhamu mbovu wataona watafika wapi?

Yupo wapi Juma Nyosso? Nidhamu ni kila kitu kiukweli kanishangaza sana na ninashangaa nikiona mtu anasupport kitu alichokifanya kisa tu anachezea team anayoshabikia.
 
1.Yeye ndiye mtu mzee sana kupita wote katika mchezo wa leo na yawezekana kwa wachezaji wote Tanzania

2.Alitakiwa awe ndio kiongozi wa busara na kwarekebisha wadogo zake wanapofanya kosa

3. Najua kwa nidhamu ile mbovu hatarajii chochote kwenye maendeleo yake ya kisoka ukijumlisha na umri wake

4. Amefanja jambo ambalo sii baya tu kwa clabu yake lakini hata kidiplomasia sii zuri kwa dharai ile aliyoionyesha kwa mchezaji wa TAIFA la kigeni ambaye hakumkosea chochote na hata baada ya kitendo kile yule mchezaji hakumjibu kwa ubaya zaidi alikwenda kumstaki kwa refa.

5. Haya mambo ni ya kizamani sana ambapo sikutarajia nilichokiona leo kwa karnr hii ambayo soka limeshaa toka kwenye uhasama na kubaki ni taaluma inayoongozwa na " FAIR PLAY" concept

6. Huyu mchezaji afutwe kabisa kwenye suala la uchezaji akafanye kazi nyingine hata za kusukuma toroli maana kwa kitendo kile anaonekana hana proffession nyingine zaidi ya mpira ambao sasa unaisha kutokana na umri ndio maana anafanya vitu vya ajabu
 
Hivi utafananisha mpira wa ulaya na tanzania? Mfano ronaldo akikosea unataka na mchezaji wa tanzania akosee?

Endeleeni kuwatia ubovu wachezaji wenu watazeekea Simba na Yanga.

Usiku mwema.
we unataka wazeekee wapi mbna Dinho alikuwa fear na anazeekea Mexico[emoji1] [emoji1]

Au Ulay hawazeeki??

Harry Kane hana kombe hata la Mmbu wa malaria, n anazeekea Tottenham we huwazi Yondan ana makombe Mengi kama Ramos.
 
Moja ya mchezo wenye changamoto nyingi sana hasa katika mchezo wa Soka ni mchezo wa "WATANI WA JADI" yaani Simba Vs Yanga.
Ni mchezo ambao unabeba hisia nyingi sana kwa wanamichezo kuanzia washabiki,wachezaji,makocha na wadau wote wa timu husika na timu mbalimbali shiriki.
Katika mchezo kuna matukio mengi sana ambayo machache yanaweza yakaonwa na mwamuzi na kuchukuliwa hatua na mengine mengi sana mwamuzi anaweza asiyaone na yakaonwa na watazamaji wengine hasa wa kwenye TV,hii ni kutokana na picha za marudio (Reply) zinazooneshwa.
Katika mchezo wa leo wa tarehe 29/04/2018 (Jumapili) ambapo timu ya Simba SC imeibuka na ushindi kuna matendo mengi sana yaliyotokea.
Moja ya kile kilichotokea ambacho kimenishawishi niandike haya ni mchezo/kitendo ambacho sio cha kiungwana kabisa (sio cha kimichezo) kilichofanywa na beki wa Yanga Kelvin Yondani kwa kumtemea mate mchezaji wa timu ya Simba.
Kiukweli ni moja ya kitu ambacho sio cha kiungwana kabisa kufanywa na mchezaji huyu hasa ukizingatia sifa ambayo Yondani amejijengea katika soka la Tanzania na hata nje ya nchi.
Ni kitendo ambacho labda mwamuzi hakukiona kabisa labda maana attention ya mpira ilikuwa ipo sehemu tofauti na kitendo hicho kilipotokea.
Ni wakati sasa wachezaji wazingatie michezo iliyo sahihi ili kufanya soka uwe mchezo wa kuburudisha kwa watazamaji wake.
Sheria ichukue mkondo wake dhidi ya vitendo kama hivi ambavyo si vya kiungwana vinavyotokea michezoni,TFF,inapaswa ichukue hatua kali sana ili iwe funzo kwa Yondani na wengine wote wenye tabia za aina hii.


Mwana_michezo


Njoooooo na wewee akutemeee
 
hayo ndiyo mapungufu, kwani wewe hujawahi kufanya ukorofi uwanjani??? Yaani mimi nilikuwa nawapiga hadi ngumi mtu akija kunikaba
Unachotetea ni nini sasa? Au ndo mlimwanbie afanye hivyo?
Sasa kama mmewatuma shauri yenu ndo mana wachezaji wenu wako kwenye hati hati ya kupewa adhabu kutkna na vitendo mnavyowafundisha visivyo na nidhamu! Chirwa na huyo Yondani
 
Kheri lawama kuliko fedhea

Safi sana Yondani tena ungemzaba kibao kabisa
 
Unachotetea ni nini sasa? Au ndo mlimwanbie afanye hivyo?
Sasa kama mmewatuma shauri yenu ndo mana wachezaji wenu wako kwenye hati hati ya kupewa adhabu kutkna na vitendo mnavyowafundisha visivyo na nidhamu! Chirwa na huyo Yondani
Yaani we unataka Yondani apewe adhabu mi sitaki sasa
 
Mleta mada ni mpumbavu na mpuuzi. Unajua sababu za Yondani kufanya vile au unakurupuka tu uonekane na wewe mchambuzi?
Hii inanikumbusha Zidane alimpiga kichwa jamaa lkn alipotoa utetezi wake ulikuwa na mashiko,usikurupuke kutoa hukum utakuwa mpumbavu
 
Back
Top Bottom