Kuhusu kitendo alichokifanya Kelvin Yondani dhidi ya Asante Kwasi

y-n

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
2,389
Reaction score
2,510
Moja ya mchezo wenye changamoto nyingi sana hasa katika mchezo wa Soka ni mchezo wa "WATANI WA JADI" yaani Simba Vs Yanga.

Ni mchezo ambao unabeba hisia nyingi sana kwa wanamichezo kuanzia washabiki,wachezaji,makocha na wadau wote wa timu husika na timu mbalimbali shiriki.
Katika mchezo kuna matukio mengi sana ambayo machache yanaweza yakaonwa na mwamuzi na kuchukuliwa hatua na mengine mengi sana mwamuzi anaweza asiyaone na yakaonwa na watazamaji wengine hasa wa kwenye TV,hii ni kutokana na picha za marudio (Reply) zinazooneshwa.

Katika mchezo wa leo wa tarehe 29/04/2018 (Jumapili) ambapo timu ya Simba SC imeibuka na ushindi kuna matendo mengi sana yaliyotokea.

Moja ya kile kilichotokea ambacho kimenishawishi niandike haya ni mchezo/kitendo ambacho sio cha kiungwana kabisa (sio cha kimichezo) kilichofanywa na beki wa Yanga Kelvin Yondani kwa kumtemea mate mchezaji wa timu ya Simba.

Kiukweli ni moja ya kitu ambacho sio cha kiungwana kabisa kufanywa na mchezaji huyu hasa ukizingatia sifa ambayo Yondani amejijengea katika soka la Tanzania na hata nje ya nchi.

Ni kitendo ambacho labda mwamuzi hakukiona kabisa labda maana attention ya mpira ilikuwa ipo sehemu tofauti na kitendo hicho kilipotokea.

Ni wakati sasa wachezaji wazingatie michezo iliyo sahihi ili kufanya soka uwe mchezo wa kuburudisha kwa watazamaji wake.

Sheria ichukue mkondo wake dhidi ya vitendo kama hivi ambavyo si vya kiungwana vinavyotokea michezoni,TFF,inapaswa ichukue hatua kali sana ili iwe funzo kwa Yondani na wengine wote wenye tabia za aina hii.

Mwana_michezo
 
khata ulaya matendo hayo hutokeo suarezi, costa, balotel wamekuwa na utovu wa nidhamu

Yondani yuko vizuri, alichezewa vibaya mara 2-3 ila akadhibiti hasira zake naona mwisho alishindwa akamtemea mate.
.mie nilijua atamkata na vibao kabisa
 
Ongeeni yooooote. tz hakuna beki bora kama Yondani, Ushahidi wote mnao. Huyu jamaa mpira anaujua Mengine ni mapungufu tu kila mtu na yake. Hata Ronaldo ni bora ila anaongoza kujiangusha Dunia nzima.
Ni mchezaji mzuri sana hasa katika nafasi yake ya ulinzi,hoja hapa ni kitendo ambacho sio cha kiungwana alichokionesha
 
Hoja iliopo hajaji uwezo wake uwanjani, ila ni kitendo cha kumtemea mate, mchezaji mwenzie.
hayo ndiyo mapungufu, kwani wewe hujawahi kufanya ukorofi uwanjani??? Yaani mimi nilikuwa nawapiga hadi ngumi mtu akija kunikaba
 
Ongeeni yooooote. tz hakuna beki bora kama Yondani, Ushahidi wote mnao. Huyu jamaa mpira anaujua Mengine ni mapungufu tu kila mtu na yake. Hata Ronaldo ni bora ila anaongoza kujiangusha Dunia nzima.
Msiwaharibu wachezaji wenu nidhamu ni kitu muhimu sana, mechi ilikua inaruka live hivi hata kama kuna team ilikua inamfuatilia unadhani itaendelea naye?

Wajifunze kwa Samatta na Ulimwengu huwezi kuona wanafanya vitu vya kijinga kama hivyo.
 
Ulimwengu na Nidhamu yake ana mafanikio gani??

Ubabe kwa beki unasaidia sana Mcheki mtu kama Ramos
 
khata ulaya matendo hayo hutokeo suarezi, costa, balotel wamekuwa na utovu wa nidhamu

Yondani yuko vizuri, alichezewa vibaya mara 2-3 ila akadhibiti hasira zake naona mwisho alishindwa akamtemea mate.
.mie nilijua atamkata na vibao kabisa
Unafananisha mpira wa Ulaya na Tanzania waendelee kuwa na nidhamu mbovu wataona watafika wapi?

Yupo wapi Juma Nyosso? Nidhamu ni kila kitu kiukweli kanishangaza sana na ninashangaa nikiona mtu anasupport kitu alichokifanya kisa tu anachezea team anayoshabikia.
 
Ongeeni yooooote. tz hakuna beki bora kama Yondani, Ushahidi wote mnao. Huyu jamaa mpira anaujua Mengine ni mapungufu tu kila mtu na yake. Hata Ronaldo ni bora ila anaongoza kujiangusha Dunia nzima.
Coton
 
khata ulaya matendo hayo hutokeo suarezi, costa, balotel wamekuwa na utovu wa nidhamu

Yondani yuko vizuri, alichezewa vibaya mara 2-3 ila akadhibiti hasira zake naona mwisho alishindwa akamtemea mate.
.mie nilijua atamkata na vibao kabisa
mi hilo tukio nilienda Mechi ikiwa iko mbali sana, Yondani hakoseagi ndio maana katoka hana kadi hata moja. Hii inadhihirisha Ana nidhamu ya hali ya juu sana.

Yanga wakimuuza au kumtema wasitegemee kupata mwingine maana Hamna beki tena wa kiwango kile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…