Kuhusu kitendo alichokifanya Kelvin Yondani dhidi ya Asante Kwasi

Ongeeni yooooote. tz hakuna beki bora kama Yondani, Ushahidi wote mnao. Huyu jamaa mpira anaujua Mengine ni mapungufu tu kila mtu na yake. Hata Ronaldo ni bora ila anaongoza kujiangusha Dunia nzima.
Sasa mambo ya kutema mate ana mimba? angesema watu wamletee ndimu na maembe mabichi
 
[emoji106]
 
Ukiangalia vizuri ile clip utaona dhahiri kabisa kwasi ndiyo aliyeanzisha tafran, kwa kuanza kumbughidhi kipa wa yanga pasipo sababu na ndiyo maana hata alipokimbilia kwa refa alipuuzwa!
Kuanzisha au Kutokuazisha tafrani hakujustify ‘upuuzi’ na ‘umbwiga’ alioufanya Kelvin. Hili linatakiwa likemewe na wapenda michezo wote.
 
Kuanzisha au Kutokuazisha tafrani hakujustify ‘upuuzi’ na ‘umbwiga’ alioufanya Kelvin. Hili linatakiwa likemewe na wapenda michezo wote.
Michezo napenda na sikemei hili we ombea tu mwenzio afungiwe badala uwaze yako, wapenda michezo wa leo bhana[emoji12] [emoji12] [emoji12]
 
Yondani namheshimu sana kwa kiwango chake, ila kitendo alichokifanya sio cha kimpira, naomba apewe adhabu kali ili iwe funzo kwake nakwa wengine wenye fikra kama zake, nakumbuka adhabu aliyopewa Nyosso baada ya kumshika makalio John Bocco.
 
khata ulaya matendo hayo hutokeo suarezi, costa, balotel wamekuwa na utovu wa nidhamu

Yondani yuko vizuri, alichezewa vibaya mara 2-3 ila akadhibiti hasira zake naona mwisho alishindwa akamtemea mate.
.mie nilijua atamkata na vibao kabisa

HATA ULAYA WANAUME WANAOLEWA . WE UPO TAYARI KUOLEWA? KAMA ULAYA WANAFANYA USHENZI SI LAZIMA NA HUKU WATU WAFANYE... UTAMADUNI WETU AFRIKA NI KUHESHIMIANA NA MPIRA NI STAREHE,NI FURAHA N.K SASA ALIFAIDIKA NA NIN? ZAIDI AMEDHARAULIKA MWENZIE HAKUMTUKANA HAKUMPIGA ANASEMA AMEMWACHIA MUNGU TU.YEYE ALIENDA KUCHEZA MPIRA... tuwe waungwana.... Nmeandk kwa sauti kubwa sababu tukitafuta justification tunakosea sana. Amekosea
 
mpira ni starehe ulaya mkuu sisi tunapoteza muda lini mpira umeanza kuwa starehe kwetu wakati umejaa ushirikina na upuuzi na mfanano wake.

kama mtuhumiwa kaamua kumuachia Mungu basi nasi tumuachie pia
 
Nimeona habari nyingi mitandaoni kuwa beki kisiki wa yanga na timu ya taifa ya tanzania bara (Kilimanjaro stars) na pia beki wa timu ya taifa (taifa stars) kelvin yondani alimtemea mate kwa makusudi beki wa simba asante kwasi.Kama tukio hilo ni la kweli basi yondani na klabu ya yanga kwa ujumla kwa pamoja wanapaswa kumuomba radhi raia huyo wa ghana ili kuepuka kitakachoitwa ubaguzi wa kitaifa iwapo suala hilo litapelekwa caf.Bado sioni sababu ya msingi ya yondani kumfanyia hvyo huyo mghana ilhali aliyefunga goli la simba ni mtanzania na aliyepiga faul iliyozaa goli ni mtanzania.Kama yondani alikuwa na hasira ya kufungwa basi ni bora hayo mate angewatemea kichuya au nyoni na sio huyo raia wa kigeni.Kitendo alichofanya huyu ndugu yetu mtanzania nahisi huenda kikafanya watanzania kuonekana sio waungwana kwa wageni haswa iwapo kama kwasi atahisi kafanyiwa hvyo kwakuwa yeye na wakuja
 
lini watanzania tumeanza kuwa waungwana sisi ni wanafiki.

yaani unaona ni halali kutemewa mate Kichuya ama Nyoni kisa ni watanzania, ila kwa m Ghana hapana.
 
Aisee, mimi Naomba radhi kwa niaba ya jamii ya Yanga.. Mpira ni fair play.
Napinga kama matukio mengne ya akina Zidane, Suarrez, Ballotel, John Terry, Nyoso nk
 
Kitendo hicho ni cha kibaguzi fifa hawataki kusikia utapigwa faini mchezaji na klabu yako na kusimamishwa kwa muda hapa sijajua tff wanasemaje yangu macho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…