Kuhusu kukamatwa kwa Tundu Lissu na leo John Heche

Kuhusu kukamatwa kwa Tundu Lissu na leo John Heche

Mushkov

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2024
Posts
667
Reaction score
1,403
Nilichojifunza mimi ni kwamba, kuna mkakati maalumu wa kujaribu kuwanyamazisha viongozi wa CHADEMA. Inawezekana wamepanga kuwakamata viongozi wote wa ngazi ya juu wakiwa na lengo la kupisha kwanza uchaguzi au kudhoofisha upinzani.

Nilichojifunza cha pekee ni kwamba, Watanzania bado hatujitambui. Sisi tunaopiganiwa hatuoni thamani ya wanaotupigania. Lissu alichukuliwa na polisi mbele ya umati wa watu lakini hakuna kilichotokea.

Leo Heche amechukuliwa mbele ya umati wa watu lakini Watanzania hawana hata shida, wapo comfortable. Wanafanya hivi kwa sababu wameshasoma Watanzania kwamba bado wapo usingizini. Kwa hali, wanaweza wakawakamata hata viongozi wote wa upinzani Nchi nzima na hali ikawa kama ilivyo sasa.

Ushauri wangu ni kwamba:-

1. Viongozi wetu wasikate tamaa.

2. Ikiwezekana kwa sasa tutumie njia nyingine mbadala ya mapambano dhidi ya dhuluma katika Nchi hii. Yaani, tusitumie mikutano tena, bali tutumie vitendo zaidi tena bila kelele zozote. Nasisitiza, viongozi wetu kama watatoka wataachiliwa, basi waje na mbinu na mikakati mipya ya kuendeleza mapambano ya kutafuta HAKI katika Nchi hii.
 
Back
Top Bottom