Pre GE2025 Kuhusu kupokea fedha za Abdul, kutoka kwa Lissu kuna ukweli kidogo na uongo mwingi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
kuna kusema ukweli na kuropoka ukweli.

ila lisu ni mropokaji tena muongo
 
Aya ya pili kutoka mwisho ndio tatizo kwa watanzania walio wengi.
Na imekuwa ndio norm na inakuwa vigumu sana kuwaelewesha watanzania kwamba fadhila ili mambo yaende nje ya utaratibu ni rushwa.
 
kuna kusema ukweli na kuropoka ukweli.

ila lisu ni mropokaji tena muongo
Weka mfano mmoja hapa, ikiwezekana kwa ushahidi wa audio au video, tuuchambue kwa kina, kimantiki, kwa kupima neno kwa neno, tujue ukweli uko wapi.
 
Aya ya pili kutoka mwisho ndio tatizo kwa watanzania walio wengi.
Na imekuwa ndio norm na inakuwa vigumu sana kuwaelewesha watanzania kwamba fadhila ili mambo yaende nje ya utaratibu ni rushwa.
Naam, kweli mkuu.

Watanzania wengi washazoea hii rushwa ya fadhila mpaka hawaioni kama rushwa.

Wamekuwa ni kama samaki aliyezaliwa na kuishi kwenye maji maisha yake yote, hata hajui kwamba anaishi katika maji, kwa sababu hajui maisha nje ya maji!

Nilitegemea mtu kama Lissu awe anatufundisha kitu tofauti, lakini utamaduni huu ni mgumu sana kuuvunja hata yeye kaingia kwenye mtego huo.
 
Reactions: Tui
Abdul mwenyewe si ngazi husika.

Abdul kushika nyaraka za Lissu tu ni favor, ni fadhila, bila kujali Abdul anazipeleka ngazi husika ama la.

Abdul anatumika kama mtoto wa rais kuweka pressure ili Tundu Lissu alipwe pesa zake. Abdul hahusiki na process hiyo, hiyo ni fadhila ya kisiasa kutumia jin ala mtoto wa rais na ofisi ya rais ili kumpa Tundu Lissu fadhila.

Tundu Lissu hakutakiwa hata kumpa Samia madai ya haki zake binafsi za mafao na kupewa pasipoti mpya, alikosea tangu alipompa madai hayo Samia Ubelgiji.

Pasipoti ikipotea, kuna mchakato wa kuomba mpya ubalozini. Mambo ya mafao yana mchakato wake serikalini. Michakato hii haimhusishi rais.

Lissu amejiingiza katika mtego wa kupewa fadhila na Samia katika sehemu ambayo Samia hahusiki.

Mchakato w akupata passport haupiti kwa Samia. Mchakato wa mbunge kulipwa pesa zake haupitii kwa Samia.

Lissu ametumia influence peddling kupata fadhila.

"In·flu·ence ped·dling

The use of position or political influence on someone's behalf in exchange for money or favors."

Hiki ndicho alichofanya Tundu Lissu.
 
Reactions: Tui
kupewa haki yako ni fadhila?
 
Hapo kuna mtego unaitwa Abdul tangu haya mambo yaanze hajawahi kuongea hata hayo mambo ya malipo ya Lisu hajaongea kwamba aliyapata kwa soft copy.Hapa ni mtu anatukana sufuria lillilompa chakula na kulitoboa kwa kutumia mtego wa Abdul.
 
kupewa haki yako ni fadhila?
Swali zuri, hapa naona kuna watu wengi hawaelewi.

Kupewa haki yako si fadhila.

Lakini, kumtumia mtoto wa rais ili uruke mstari halali wa kupata haki yako ni kupewa fadhila na huyo mtoto.

Umeelewa?

Yani inawezekana kuna dirisha la kupewa haki yako, kuna mstari wa watu 100 wamekutangulia kufika disrishani kupata haki zao.

Ukija wewe unajuana na mkurugenzi wa hiyo sehemu akakurusha huo mstari upate haki yako bila kufuata mstari, kukurusha huo mstari ni fadhila, hata kama unaruka mstari ili kupata haki yako.

Ushaelewa?
 
Hapo kuna mtego unaitwa Abdul tangu haya mambo yaanze hajawahi kuongea hata hayo mambo ya malipo ya Lisu hajaongea kwamba aliyapata kwa soft copy.Hapa ni mtu anatukana sufuria lillilompa chakula na kulitoboa kwa kutumia mtego wa Abdul.
Kanuni rahisi ni kwamba tuhuma zinatakiwa kujibiwa, zisipojibiwa zinachukuliwa kama kweli.

Kama Abdul kasingiziwa, akanushe tu tuhuma na kutupa upande wake.
 
Lisu hakumfuata Abduli. Abduli ndiye alienda kwa Lisu kumhonga, Lisu akamwambia sitaki pesa zako hizo, nataka pesa zangu halali. Nimeshafuata taratibu zote zaidi ya mara mbili bila mafanikio. Kamwambie mama yako anipe pesa zangu. Sitaki hizi zako CHAFU

hapo kuna kuomba fadhila hapo? kuna kuruka foleni hapo?

acha hizo diaspora

kule kwa shamgazi "kiranga" ni jembe lile la kulimia kwa mkono.
 
Nani kamfuata nani ni irrelevant, unaweza kumfuata Abdul kwake akakupa rushwa, mnaweza kukutana hotelini akakupa ruswa, anaweza kuja kwako akakupa rushwa.

Kwa hiyo habari ya nani kamfuata nani ni irrelevant.

Lissu angeweza kumwambia Abdul sitaki pesa zako ondoka kwangu.

Hakufanya hivyo.

Lissu alimtaka Abdul amfanyie fadhila ya kumsaidia kupata haki yake, fadhila ya kutumia jina la rais ili Lissu apate haki yake kirahisi.

Hii fadhila ni rushwa ya fadhila.

Hii rushwa ya kutumia influence yako ili kupata urahisi kinyume na mifumo rasmi iliyotumika hapa inaitwa "influence peddling".

in·flu·ence ped·dling

the use of position or political influence on someone's behalf in exchange for money or favors.

Jadili hoja, usimtukane mtoa hoja. Kumtukana mtoa moja ni dalili ya kukosa hoja.

Ni logical fallacy inaitwa ad hominem.
 
Lissu hakukataa hongo.

Alikataa hongo ya pesa akakubali hongo ya fadhila ya Abdul kumsaidia apate mafao yake.

Kwa maneno yake mwenyewe.

That was influence peddling.

Lissu should do better than that.
Mtu akiwa muongeaji sana kuna mahali anajikanyaga kwenye maelezo yake.
Lissu ameongea mengi kiasi cha kujiweka kwenye hatia ya yeye kutaka kupokea rushwa ya gharama za matibabu.
Ameruka moto akakanyaga maji ya moto.
Nikitoka nje ya mada kidogo, naona Mbowe imefika wakati anastahili kuachia mtu mwingine nafasi ya uongozi CDM.
 
Lissu kaongea sana mpaka kajikanganya kwenye maelezo yake.

Lakini kujikanganya kwenye mazungumzo mara nyingine kunaonesha mtu anasema ukweli. Ukiona mtu anatoa story imenyooka kila kitu, hapo inabidi upate shaka kujiuliza kama kuna vitu vinafichwa.

Mimi nimefurahia uwazi wake, Lissu hapa kasema kama mtoto ambaye hawezi kudanganya, anasema mambo mpaka yale yanayoweza kumuumiza yeye mwenyewe.

Ila pia, Tanzania tuna standards ndogo sana, pengine kwake yeye anaona hili si tatizo, na kama mwanasheria pengine anaangalia the legal standard, which is a very low standard kwa sababu kuna rushwa nyingine zipo kisheria kabisa na mtu mwenye moral compass anatakiwa kuzikataa.

Ndiyo maana CCM ilipotaka kuhalalisha takrima, kuna watu wengi walipinga wakisema wameipa rushwa chafu jina jipya tu.

Wanasheria wana tabia ya kusema mengi huku wakiamini kuwa hata wakibanwa wanaweza kujitetea kisheria.

Tatizo uongozi wa jamii si suala la kisheria tu, kuna mambo mpaka ya maadili pia.
 
m
mimi kimtazamo wangu kuhusu ombi la lisu kusaidiwa na abdul kupata stahiki zake si jambo baya ,maana kama tunavyojua abdul si mtu wa wizara husika inayoshughulikia maadai ya lisu ila ni mtu wa connection ambae ana influence kubwa kwa watu wa maamuzi hivyo aliamini kwa kupitia yeye basi jambo lake lingapata msukumo wa moja kwa moja kutoka kwa mama mtu na mama abdul akatoa comand kwa wahusika wafuate sheria inavyosema,kwa kutengua vikwazo vinavyominya stahiki za lisu kupatikana,kwa hisia zangu zinakuja kuwa abdul nae alitoa conditions za kufanikisha hilo,au kwa lugha nyingine quid pro quo ilihitajika au kula uliwe hapo ndipo lisu aliona huu mtego ,lisu aliona hawa watu wanataka kumziba mdomo ili siku nyingine asiweze tena kukemea rushwa akaona potelea pote sihitaji tena msaada wenu nendeni zenu.abdul kwa sasa ni kama dalali ukitaka jambo lako liwe la kisheria lisiwe la kisheria liende haraka basi muone hilo limeisha kama unavyojua system za kiafrika zpo kwa ajiri ya kuweka ugumu ili ufanikishe unachohitaji ,sio kama wenzetu system zpo kurahisisha maisha,.
 
Hiyo habari nzima ya kutumia connection ya Abdul kupata fadhila ili madai ya Lissu yapate msukumo ndiyo tatizo lilipo hapo.

Tundu Lissu kama msimamia haki alitakiwa kusimamia kupata haki yake bila kutegemea fadhila ya mtu.

Kutegemea fadhila ya Aabdul ni tatizo kwa sababu.

1. Kimsingi ni rushwa ya fadhila. Abdul alitaka kumpa Lissu rushwa ya pesa, Lissu akakataa rushwa ya pesa, akamtaka Abdul amfanyie fadhila kupata pesa zake, hii fadhila ni rushwa pia.

2. Tundu Lissu alipokataa rushwa ya pesa kimsingi alikataa kununuliwa kwa pesa ili asimsakame Samia. Kukataa pesa za Abdul halafu kukubali fadhila zake ni kukubali rushwa vile vile. Abdul akimpa pesa au fadhila bado anategemea Lissu asiendelee kumsema Mama yake Abdul rais Samia.

3. Rushwa ya fadhila inaondoa usawa. Kuna watu wengi sana wana tatizo kama la Lissu lakini hawajuani na Abdul wala Samia. Tundu Lissu akitumia nafasi yake ya kisiasa ya kujuana na Abdul na Samia kutatua tatizo lake, anakuwa kakwepa kutatua tatizo la kimfumo linalowaacha Watanzania wengi wenye tatizo kama lake ambao hawamjui Samia.

4. Tundu Lissu amekosa kuitumia nafasi hii muhimu kuifanya kama cause ya kulazimisha mifumo ifanye kazi vizuri zaidi kwa watu wengi zaidi. Amepewa nafasi ya kufanya kazi ngumu ya kuanzisha mabadiliko haya au kujinufaisha yeye mwenyewe kwa cheo chake na connections za kisiasa, kawasaliti Watanzania maelfu kwa maelfu wenye tatizo kama hili kwa kujipendelea yeye mwenyewe kupata mteremko kwa Abdul bila kushughulikia tatizo la kimfumo.

5. Noblesse oblige. Those who are given much, much shall be required from them. Tundu Lissu amepewa heshima kubwa, matumaini mengi na watanzania wengi. Standard ambayo tunapaswa kuwawekea viongozi wetu nayo inatakiw akuw akubwa.Tundu Lissu alitakiwa kuwa mfano kwa Watanzania wengi ambao hawajui influence peddling ni nini, alikuwa na nafasi ya kuwafundisha kukataa mfumo wa kupata haki kwa kujuana na kuonesha kuwa anaweza kung'ang'ania mfumo halali unaotakiwa kutumiwa mpaka apate halki yake, bila kutumia fadhila ya connections za Abdul na Samia.
 
Mtamaliza theories zote lakini ukweli hela za Abdul zimewaumbua Mbowe na genge lake la matapeli hapo Chadema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…