Desprospero
JF-Expert Member
- Feb 1, 2023
- 1,015
- 2,493
C&P from Face Book.
KUTEKWA, KUTESWA, KUUAWA KWA ALLY KIBAO, TUSAIDIANE KUTAFAKARI
Na Bollen Ngetti
SOMA lakini kwa tafakuri pana labda tukajua ukweli walau kidogo si wote katika giza hili lililofunika kutekwa, kuteswa na hatimaye kuuawa kikatili Mzee Ally Muhammed Kibao al-maarufu MeD.
Niharakishe kusema ukweli kwamba hakuna uhusiano mzuri baina na kati ya CCM na Chadema kimkakati, kisiasa na hata kimtazamo na kimaadili. Niharakishe pia kusema kama ilivyo kwa vyama vyote kongwe ni hayawani pekee anayeweza kutenganisha chama-tawala na dola. Kwamba dola inaishi kwa hisani ya chama-tawala na kwa mantiki hiyo dola ina wajibu mkubwa wa kukilinda chama kwa gharama yoyote.
Sasa twende. Siku za karibuni Jeshi la Polisi lilitoa taadhari kwa umma mpana kwamba lina taarifa za kijasusi zisizo na chembe ya shaka kwamba Chadema inapanga makundi ya vijana yapatayo 20 ambayo yatavamia vituo vya polisi jijini Dar es salaam kwa wakati mmoja.
Kwa mujibu wa Polisi intelijensia ilionesha kikao kilichokuja na uamuzi huo mgumu ulifanyika kupitia mtandao wa ZOOM. Hata hivyo Polisi haikusema lengo la kuvamia vituo hivyo ni nini hasa? Kuvichoma moto? Kuwapiga Polisi? Kuwafungulia huru maabusu? Kukwapua silaha? Kwenda kuvitumia wapi? Endelea kutafakari.
SASA tujiulize haya maswali ya msingi. Hakuna mtu wa kawaida mwenye uwezo wa kuvamia kituo cha polisi akijua fika ni eneo salama iliyosheheni silaha za kivita. Mtu huyo anaweza tu kama naye ana mafunzo mahsusi ya masuala hayo ama ni jambazi mzoefu. (Rejea kuvamiwa kwa kituo cha Polisi Stakishari Ukonga).
Tembea na neno "taarifa zisizo na SHAKA" kichwani.
Hii maana yake ni kwamba wavamizi watarajiwa wa vituo vya polisi kutoka Chadema wana uwezo, mafunzo, ujasiri juu ya maswala ya usalama na kwa mantiki hiyo wasingekwenda kujaribu bali kutekeleza. Swali lingine linanijia kichwani maana taarifa ya Polisi ina ukweli "usio na shaka". Kwamba vijana hawa wa Chadema wamepata mafunzo hayo wapi na lini? Maana si majambazi kwa mujibu wa Polisi.
Vyuo vya usalama nchini vinajulikana kuanzia Polisi, Magereza, TISS, JWTZ. Wao wamepata mafunzo wapi? Chadema ina chuo cha mafunzo ya silaha kiasi cha kuvamia vituo vya Polisi kulikosheheni bunduki za kila aina?
Kama hawa chuo kama hicho ndani au nje ya nchi, basi tujiulize kusumbua bongo zetu. Nani aliwapa mafunzo wakaiva na hivyo kuwa na uwezo, ujuzi na ujasiri wa kuvamia vituo vya polisi ? Kwani Red Brigade wanafunzwa kuvamia vituo vya Polisi? Usichoke kutafakari....
SASA, moja ya sifa tuliyoambiwa Marehemu Ally Kibao anayo ni kwamba ni Mwanajeshi mstaafu aliyefika katiko vyeo vya juu si kabisa. Kibao alikuwa ni Mjumbe wa Sekretariat ya Chadema lakini pia tunaambiwa kuwa ndiye alikuwa ni "strategist" wa chama na ndio hakufahamika sana majukwaani maana alikuwa "nyuma ya kamera ".
Sijui viapo vya JWTZ vinasemaje ila Kibao baada ya kustaafu alijiunga na CCM na kuwa Mwenezi Mkoa wa Tanga na baadaye kutimkia Chadema hadi alipotekwa, kuteswa., kuuawa na mwili wake kutupwa vichakani huko Ununio (Dar es salaam).
Swali fikirishi! Je, ni huyu (Kibao), strategist, JWTZ mstaafu ndiye aliwapika vijana wa kuvamia vituo vya Polisi? Je, uratibu huu ulikuwa ukiendelea na tuseme Polisi waliamua kujihami kabla ya uvamizi kwa usemi, "mpige mchungaji na kondoo wote watatawanyika"? Haya yote ni kuwaza maana ripoti ya uchunguzi juu ya waliomuua Kibao ni kina nani hasa licha ya alama zote kuonesha ni watu wenye kumiliki pingu ama wa ndani au nje ya nchi. Yote yawezekana.
Je, polisi iko katika operesheni maalum kuzuia wavamizi kabla ya kuvamiwa? Swali linalogonga vichwa ni kwamba kama taarifa za kijasusi zilionesha kuwa MeD ndiye alikuwa "chuo" cha kuwaandaa wavamizi ndiyo auawe badala ya kumfikisha kwenye vyombo vya sheria? Sina jibu....wauaji wana majibu.
Nawaacha na swali hili! Kwa tusiamini kuwa nyuma ya vitendo vya utekaji Chadema haiko nyuma yake kisiasa? Kwa nini hutaki kuamini na kwa nini uamini. Nawatakia tafakuri njema na jadidi. Alamsiki.
PIA SOMA
- TANZIA - Dar: Ally Mohamed Kibao, kiongozi wa chadema auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana