Kuhusu kuuawa Hayati Mzee Ali Kibao, Mwandishi nguli wa Habari za Uchunguzi Bollen Ngetti ameandika haya, inafikirisha!

Kuhusu kuuawa Hayati Mzee Ali Kibao, Mwandishi nguli wa Habari za Uchunguzi Bollen Ngetti ameandika haya, inafikirisha!

Nimeumia sana kwa hili lililompata Mzee Kibao (marehemu).
Nimelia sana sana.

Naomba niseme jambo moja, kama Mbowe aliyesemekana kupanga ugaidi alikamatwa na kuwekwa mahabusu na kushitakiwa, kwa nini mtu ambaye inasemekana (kama alivyoandika huyu Ngetti) kuwa ni "strategist" na mpikaji wa vijana wanaosemekana kuwa walikuwa wanaandaliwa kuvamia vituo vya polisi, asikamatwe na kuwekwa mahabusu na kisha kushitakiwa!!??

Hakuna sababu yoyote itakayohalalisha unyama aliofanyiwa marehemu Kibao.

Hakuna.
Hakuna.
Hakuna.
 
Mwandishi anajaribu kuonyesha CHADEMA ATI wanauwezo Mkubwa huku akidharau uwezo wa Vyombo vya Dola kwamba havijui, havina uwezo, havitambui wajibu wake n.k.

Mwandishi kadharau serikali kimantiki ingawaje Kwa umbo la nje ameonyesha kuitetea Kwa namna Moja ama ñyiñgine.

Mwandishi amejisahaulisha kuwa siô jukumu la CHADEMA, Kulinda raia WA nchi hii.
Mwenye jukumu Hilo ndîo anakuwa wakwanza kubeba lawama, fedheha Kwa kushindwa kutimiza wajibu
 
hakuna kitu nacheka kama
cdm wako nyuma ya haya, sasa hawa chadema wapewe nchi tu maana wanawezaje fanya vitendo kama hivi kwenye nchi yenye vyombo vya usalama na vinavyo lipwa kwa fedha za kodi na bado havifanyi kazi yake

acheni upumbavu kwamba serikali ichafuliwe kwa haya matukio na dola iko kimya

basi cdm ni dude kubwa sana
 
Wamekufikishaje hapo waandishi kamanda? Au unadhani kila mtu ataandika hadithi unazopenda wewe? Acha watu waandike fikra zao kwa uwazi kama huzikubali funga bakuli lako pita kule! Au unadhani kila mtu humu anadumisha fikra za mbowe?
huyo sio mwandishi. huyo ni spin doctor. Anamu-accuse Marehemu kwa kosa ambalo hata serikali yenyewe haijawahi kumuhisisha.. unajua implication zake kwa familia ya Marhum. huu ni upumbavu. Mzee wa watu hawezi kujitetea. kwanini asingesema yote haya alivyokuwa hai. Irresponsible 'journalism'
 
Kwahiyo huyo muandishi nguli yeye hakujiuliza kwanini rais alisema kutekwa ni drama, bunge kugoma kujadili huo utekaji, na mahakama kugoma kutoa amri ya kimahakama kuhusu watu kutekwa, ila yuko na hizo dhana za kuokoteza!

startergear naona unadhani bado watu wamelala, hivyo hii spinning ya huyo muhuni unategemea itatupoteza maboya.
Lengo la chadomo ni kutaka serkali iache ishu za msingi ibakie kujadili utekaji na watekaji ni wao , namshukuru Mh Rais Samia kugundua hilo na bunge kujitenga na ujinga huo

USSR
 
Lengo la chadomo ni kutaka serkali iache ishu za msingi ibakie kujadili utekaji na watekaji ni wao , namshukuru Mh Rais Samia kugundua hilo na bunge kujitenga na ujinga huo

USSR
Ujinga upo wapi hapo?....kwani utekaji na mauaji hayapo?
 
..naona kama muandishi Bollen Ngeti anajenga hoja ya kuhalalisha mauaji ya Mzee Ally Kibao.

..Huyu bwana hata kama aliwahi kuwa mwanajeshi, na alikuwa walipanga njama dhidi ya Polisi, bado hakustahili kuuwawa na kutobolewa macho.

..Na hapa sizungumzi juu juu tu. Tunaweza kurudia matukio ya ukamataji wa WAHAINI ya mwaka 1983.

..Yuko komando Captain Mussa Tamim aliuwawa wakati wa ukamataji. Tamim alikuwa askari, mtu wa Tanga, ambaye alituhumiwa kutoroka jeshini. Wengine wanadai hakutoroka alitumwa kwenda kumlinda Rais Yussuf Lule wa Uganda.

..Tamim aliuwawa na maofisa usalama waliotumwa kumkamata kwa tuhuma za kupanga njama kupindua serikali. Lakini uhalali wa kumuua ulitokana na ukweli kwamba Tamim alikataa kukamatwa, na aliwashambulia maofisa waliotumwa kumkamata.

..Tukirudi kwenye tukio la Ally Kibao, yeye hakugoma kukamatwa. Pia hakushambulia waliomkamata. Sasa imekuwaje akauwawa? Pia kwanini amwagiwe tindikali? Kwanini atobolewe macho?

..Nimewarudisha kwenye historia ili muelewe UJINGA wa baadhi ya waandishi watetezi wa CCM kama Bollen Ngeti.
Naamini hamjamsoma huyo mwandishi mpaka mwisho mkamuelewa, au kama mmemsoma, basi hisia za maumivu zimewasukuma kumshambulia kinyume na hoja zake alizoandika.

• Hivi mnaanzaje kumlaumu mtu ambaye anauliza, hata kama Marehemu Kibao alikuwa ns kosa, kwanini auwawe badala ya kupelekwa mahakamani?

• Mnamlaumu vipi mwandishi anayeuliza wapi Chadema wana chuo cha mafunzo ya kijedhi kama walivyo polisi CCP, TISS, ns JWTZ?

Wengi wenu mmekurupuka kumshambulia mwandishi, mnajihami kuogopa spinning mkidhani kila kinachoandikwa ni mchezo.

Nakuona umezungumzia haki za marehemu, wakati Bollen nae amezungumzia haki hizo alipouliza kwanini hakupelekwa mahakamani badala yake wakamuua?!

Nyie hamjamsoma mkamuelewa, mmekutupuka kumshambulia tu!.
 
Naamini hamjamsoma huyo mwandishi mpaka mwisho mkamuelewa, au kama mmemsoma, basi hisia za maumivu zimewasukuma kumshambulia kinyume na hoja zake alizoandika.

• Hivi mnaanzaje kumlaumu mtu ambaye anauliza, hata kama Marehemu Kibao alikuwa ns kosa, kwanini auawe badala ya kupelekwa mahakamani?

• Mnamlaumu vipi mwandishi anayeuliza wapi Chafema
don't entertain this ndugu. Trying to build an argument by sounding clever and taking clever digs at the regimes in such serious times isnt the way to go. Mzee wa watu amefariki , na huyu mwandishi amejaribu kuunganisha dots ambazo ni very far fetched. wapi polisi walimuhusisha na ugaidi? Wakti yupo hai jina lake 99.9% of wabongo hawajawahi hata kulisikia kwenye siasa and there isnt any reason for him to tie his death with stupid conspiracies. anataka kuhalalisha alichofanyiwa au??
 
Naamini hamjamsoma huyo mwandishi mpaka mwisho mkamuelewa, au kama mmemsoma, basi hisia za maumivu zimewasukuma kumshambulia kinyume na hoja zake alizoandika.

• Hivi mnaanzaje kumlaumu mtu ambaye anauliza, hata kama Marehemu Kibao alikuwa ns kosa, kwanini auwawe badala ya kupelekwa mahakamani?

• Mnamlaumu vipi mwandishi anayeuliza wapi Chadema wana chuo cha mafunzo ya kijedhi kama walivyo polisi CCP, TISS, ns JWTZ?

Wengi wenu mmekurupuka kumshambulia mwandishi, mnajihami kuogopa spinning mkidhani kila kinachoandikwa ni mchezo, mnatakiwa kutuliza vichwa msome mkijiamini, kisha mchambue maandishi.
Mpumbafu, kauliza maswali ya kijinga
 
Back
Top Bottom