Kuhusu Luteni feki wa JWTZ: Jeshi liboreshe alama zake zinazoweza kufojiwa kirahisi

Bongo wapo watu wanajifanya kitengo, takukuru tra nk pia

Ova
 
Ndio maana nasema mifumo mibovu haitoshi mtu kusema tu mm ni captain kitambulisho kiko wapi?
Kwanza polisi atakijulia wapi kitambulisho cha Jeshi? Hata akipewa akione hawezi kujua kama ni chenyewe. Huyo aliyekutwa na uniform ya jeshi hawezi kuvaa uniform ya jeshi na kusogea maeneo ya karibu yenye wanajeshi.
 
Wanajeshi wenyewe ndio hawa wanywa visungura na na kuvuta makushabu, sasa hapo unategemea weledi wowote kweli?
 
Shida sio kuwa luteni kwa miaka 24. Kuna vijana wengi tu kwa sasa wana nyota mbili. Ninachojiuliza huyo Emmanuel alitoa wapi zile sare, badge pamoja na baadhi ya nyaraka za kambi aliyodai anatokea
Simply anawashkaji wengi wanajeshi.
 
Dogo either alipitia jkt au ni askari kweli wa kawaida au alishafukuzwa, mtu tu wa kawaida si rahis kuwa na access
 
Nakubaliana na wewe.
 
Naomba nikuulize maswali mawili mkuu
1.Ukiwa na mtu kama kanali na una age ya 26 elimu form 6 science, vip anaweza kukuingiza kihangaiko kweny kozi ya ajira??
2.Na ukiwa na age iyoiyo na elimu iyoiyo apo juu vipi mtu kama kanali anaweza kukuingiza kweny kibangala cha wale wa Bms?? Mwachiluwi
Sikuizi mwisho 28 😂
 
KUboresha mifumo na taratibu sahihi
 
Kuigiza uanajeshi mpaka mtu awe amepitia mafunzo ya kijeshi na kukosa ajira ama kufukuzwa ndiyo unaweza.

Kumtambua mtu kuwa huyu siyo askari hakuhitaji kitambulisho.

Kuna vipengele vidogo vidogo vingi sana ambavyo hutumika kumtambua askari halisi na feki.

Kwanza kabisa kumtambua ni kutokana na desturi ama tamaduni za kijeshi pamoja na alama za vyeo: ukiona mkubwa wa cheo anaanza kumsalimia mdogo wa cheo, tayari mtego unaanza kutikisika huo.

Huyo wa Bariadi alitaka kupatia umri na cheo, maana kuna umri wa vyeo hivyo.
Miaka 24 alitakiwa awe Private ama officer 2lt.

Ukiona mbabu kavaa gwanda, ana cheo cha Pte, Cpl, 2Lt, Lt, Capt, simama umhoji kikosi anakotokea kabla mtego haujafyatuka kunasa.

'Jambo afande' ama kiitikio 'afande' hutumika kwa mdogo pekee kumsalimia ama kumuitikia superial wake, kinyume na hapo wacha mtego unase kabisa.

Tukija kwenye mavazi ya fatique(mnaita kombati), mavazi hayo yana matoleo ya kila wakati na mashono yanatofautiana.

Mtu kama alihifadhi gwanda la mwaka 2000, akilivaa leo, lazima aangaliwe kwa jicho la kwanini na wivu mkubwa, akamatwe na ahojiwe.

Ukiona askari kavaa kijeshi, halafu katamani ndizi, akanunua na kuanza kula huku akitembea, muite na umuulize kikosi cha karibu kinaitwaje, akikujibu, muulize Kombania gani uone atavyoanza kujikanyaga?

Ninasema kwamba askari ama officer halisi wa jeshi haghushiki na wala hahitaji kutambuliwa kwa kitambulisho, anatambuliwa kwa kumtazama tu.
 
Ndio ila lazima umri upunguzwe hapoa
 
Ili kuendana na umri tajwa au wanaoutaka kwa wakati uho
Duuh kwahyo kipengele cha umri kinaweza kukutoa mchezoni hata kama upo na MTU mkubwa mfano kanali? maana kuanzia kanali hua wanapewa nafas za kupeleka watoto wao
 
Duuh kwahyo kipengele cha umri kinaweza kukutoa mchezoni hata kama upo na MTU mkubwa mfano kanali? maana kuanzia kanali hua wanapewa nafas za kupeleka watoto wao
Kaka mimi sijui
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…