Juzi hapa kakamatwa kijana aliejifanya kuwa ni officer wa jeshi la JWTZ umri maika 24 kuna vitu JWTZ wanatakiwa kubadilisha cha kwanza vitamburisho
Vitambulisho vinavyotumiwa na wanajeshi wa JWTZ bado ni vyepesi mtu kutengeneza waige kutoka usalama wa taifa kile kitambulisho chao mpaka ukitengeneze ni kasheshe sana tofauti na JWTZ ambavyo mtu anaweza enda stationary aka kitengeneza ndio maana wanaibuka vijana wengi wakijifanya ni askari wa JWTZ na kukamatwa
Kingine kitendo cha yule kijana kukamatwa na polisi kwangu naona kama dosari fulani polisi anakuwa wakwaza kupata taarifa uku IO wajeshi wapo ambao walitakiwa kumjua before ya polisi kumjua, hii nitofauti na usalama mtu akijifanya usalama wa taifa kabla ajakamatwa na polisi wao wanakuwa wakwanza kumjua mara nyingi wao ndio wanamjua na wanamshuguhulikia kimya kimya akitoka salama hawezi simulia kilicho mkuta
Bado najiuliza maswali mengi sana ila sipati majibu ila mimi naona shida kubwa ipo kwenye vitambulisho bado nalia hapo ndio naona source watengeneze vitambulisho ambavyo ni thabit na sio hivi ambavyo vimepitwa na wakati waige kama vya usalama
Pia Simiyu yupo mshauri wa jeshi la akiba pale mkoa na wapo wasaidizi wake pia ina maana hawakuwai kukutana na huyu kijana najua askar yoyote wakikutana kuna mambo mkiongea mtajua tu huyu askari miaka 24 anakuwa ltn kaajiliwa lini chuo kaenda lini kamaliza lini na TMA kamaliza lini mh
Muhimbili pia matapeli wanaingia pale kwasababu symbol zao ni nyepesi mfano ukiwa mfanya kazi wa pale ili aingie wordin ni lazima awe na koti jeupe kama hana kitambulisho sasa kwa mfumo uhu amuoni mianya ya kuingiza matapeli ipo wazi kabisa na mtu anaweza akaingia na akamchoma mgonjws sindano ya sumu na akatoka kwasababu symbol zao ni nyepesi sana
Kuigiza uanajeshi mpaka mtu awe amepitia mafunzo ya kijeshi na kukosa ajira ama kufukuzwa ndiyo unaweza.
Kumtambua mtu kuwa huyu siyo askari hakuhitaji kitambulisho.
Kuna vipengele vidogo vidogo vingi sana ambavyo hutumika kumtambua askari halisi na feki.
Kwanza kabisa kumtambua ni kutokana na desturi ama tamaduni za kijeshi pamoja na alama za vyeo: ukiona mkubwa wa cheo anaanza kumsalimia mdogo wa cheo, tayari mtego unaanza kutikisika huo.
Huyo wa Bariadi alitaka kupatia umri na cheo, maana kuna umri wa vyeo hivyo.
Miaka 24 alitakiwa awe Private ama officer 2lt.
Ukiona mbabu kavaa gwanda, ana cheo cha Pte, Cpl, 2Lt, Lt, Capt, simama umhoji kikosi anakotokea kabla mtego haujafyatuka kunasa.
'Jambo afande' ama kiitikio 'afande' hutumika kwa mdogo pekee kumsalimia ama kumuitikia superial wake, kinyume na hapo wacha mtego unase kabisa.
Tukija kwenye mavazi ya fatique(mnaita kombati), mavazi hayo yana matoleo ya kila wakati na mashono yanatofautiana.
Mtu kama alihifadhi gwanda la mwaka 2000, akilivaa leo, lazima aangaliwe kwa jicho la kwanini na wivu mkubwa, akamatwe na ahojiwe.
Ukiona askari kavaa kijeshi, halafu katamani ndizi, akanunua na kuanza kula huku akitembea, muite na umuulize kikosi cha karibu kinaitwaje, akikujibu, muulize Kombania gani uone atavyoanza kujikanyaga?
Ninasema kwamba askari ama officer halisi wa jeshi haghushiki na wala hahitaji kutambuliwa kwa kitambulisho, anatambuliwa kwa kumtazama tu.