Kuhusu Luteni feki wa JWTZ: Jeshi liboreshe alama zake zinazoweza kufojiwa kirahisi

Kuhusu Luteni feki wa JWTZ: Jeshi liboreshe alama zake zinazoweza kufojiwa kirahisi

Halafu hujui hata unachokizungumzia hapa.
Kwa mujibu wa TPDF kijana mwenye elimu ya kidato cha sita anakuwa na sifa ya kupewa mafunzo ya uafisa. Halafu sasa hivi kuna vijana wengi tu wanamaliza form six na miaka 18. Kwahiyo akijiunga na jeshi na kupewa kozi ya miaka 3 ya military science au ile kozi ya mwaka mmoja tayari anakuwa lieutenant.
Hao usalama mnawatukuza bure tu.
Bure kabisa.
Mikataba mingapi serikali imeingia hasara ya mabilioni huku hao usalama wapo tu wanapigwa na viyoyozi.
Kuna jambo la muhimu kuliko uchumi wa nchi?
Uchumi wa nchi ukitetereka na nchi inatetereka, hakuna bunduki au askari anayeweza kumdhibiti mtu ambaye kula yake ya shiida . Sema tu Watanzania wajinga fulani.
TISS nitawakubali mpaka nione wameweza kuzuia ulaghai kwenye rasilimali za nchi.
Sasa hivi mkoa mmoja tu ukienda unakuta migodi zaidi ya 20 wachina wanachimba madini.
Imputs za maana hakuna
Tena kama usalama wapo serious walitakiwa ku deal na mwigulu zamani, sema nini unakuta mwigulu nae ana watoto wake au ndugu zake usalama sasa hapooooo.......basi ngoja niachie hapa
 
Tena kama usalama wapo serious walitakiwa ku deal na mwigulu zamani, sema nini unakuta mwigulu nae ana watoto wake au ndugu zake usalama sasa hapooooo.......basi ngoja niachie hapa
Shida hawa watu wanadanganywa na wanasiasa usalam ulete fyoko fyoko wanachukuliwa poa tu nishawai kukutana nao kwenye msiba wa mkubwa mmoja siku ya maziko alfajir walitimua watu wote hakuna cha polisi wala nan kauli yao ni moja tupisheni tufanye kazi yetu sasa na wote walikaa pembeni
 
Polisi ndo jukumu lao kukamata wahalifu wanaofanya kosa la jinai, hata kama wangemkamata Jwtz inatakiwa wampeleke polisi ili taratibu za kumfikisha mahakamani ziendelee, hao usalama unaosema wanamkamata mtu kimya kimya wanavunja sheria hawaruhusiwi kufanya ukamataji kama kweli wanafanya hivyo basi huo ni utekaji.

Maana hata hivyo kosa la kuvaa nguo la jeshi yoyote iwe jwtz, polisi au magereza bila ruhusa ya Rais adhabu yake ni faini elfu 50 au kifungo mwezi mmoja.
200
 
Juzi hapa kakamatwa kijana aliejifanya kuwa ni officer wa jeshi la JWTZ umri maika 24 kuna vitu JWTZ wanatakiwa kubadilisha cha kwanza vitamburisho

Vitambulisho vinavyotumiwa na wanajeshi wa JWTZ bado ni vyepesi mtu kutengeneza waige kutoka usalama wa taifa kile kitambulisho chao mpaka ukitengeneze ni kasheshe sana tofauti na JWTZ ambavyo mtu anaweza enda stationary aka kitengeneza ndio maana wanaibuka vijana wengi wakijifanya ni askari wa JWTZ na kukamatwa

Kingine kitendo cha yule kijana kukamatwa na polisi kwangu naona kama dosari fulani polisi anakuwa wakwaza kupata taarifa uku IO wajeshi wapo ambao walitakiwa kumjua before ya polisi kumjua, hii nitofauti na usalama mtu akijifanya usalama wa taifa kabla ajakamatwa na polisi wao wanakuwa wakwanza kumjua mara nyingi wao ndio wanamjua na wanamshuguhulikia kimya kimya akitoka salama hawezi simulia kilicho mkuta

Bado najiuliza maswali mengi sana ila sipati majibu ila mimi naona shida kubwa ipo kwenye vitambulisho bado nalia hapo ndio naona source watengeneze vitambulisho ambavyo ni thabit na sio hivi ambavyo vimepitwa na wakati waige kama vya usalama

Pia Simiyu yupo mshauri wa jeshi la akiba pale mkoa na wapo wasaidizi wake pia ina maana hawakuwai kukutana na huyu kijana najua askar yoyote wakikutana kuna mambo mkiongea mtajua tu huyu askari miaka 24 anakuwa ltn kaajiliwa lini chuo kaenda lini kamaliza lini na TMA kamaliza lini mh

Muhimbili pia matapeli wanaingia pale kwasababu symbol zao ni nyepesi mfano ukiwa mfanya kazi wa pale ili aingie wordin ni lazima awe na koti jeupe kama hana kitambulisho sasa kwa mfumo uhu amuoni mianya ya kuingiza matapeli ipo wazi kabisa na mtu anaweza akaingia na akamchoma mgonjws sindano ya sumu na akatoka kwasababu symbol zao ni nyepesi sana
Ilikuwa rahisi sana kukamata huyo kijana.
 
Kaka vijana sawa wapo ila umri unakataa ata kama umeingia chomboni ukiwa na elimu ya darasa la saba bado inagoma ata wale formsix wanaoenda kule kumbuka kuna miaka 3 ya kusoma military science bado umri unagoma lazima ukatae kwa miaka 24 pia kuna mwaka mmoja wa pale TMA bado

Kuhus nguo nahisi ni kutokana na kitambulisho uenda alienda kununua izo sare mgulani akaonyesha kitambulisho wakampa au alijitambulisha kwa njia ya simu kuwa p..,,,,,, wakamtambua kuwa ni afisa kumbe sio
Mkuu Watu kama wanakua wamekulia kwenye mifumo ya jeshi au walifukuzwa jeshi, kuna jirani yetu aliingia jeshi kabla kuingia jeshi alikua tapeli sasa baada kufukuzwa kazi ikabidi aendelee na kazi yake ya utapeli alikua anapita mpaka Lugalo na anajitambulusha yeye ni kapteni na anapita tu, kwa huyo kijana atakua kashapitia kwenye jeshi kwahiyo anajua mambo yao, siyo rahisi kija wa mtaani tu aanze kuvaa nguo za JWTZ. Ni sawa na mimi sijui mambo ya U Daktar na sijawahi kufanya kazi hospotali leo hii niende hospital nikajifanye Daktar hii itakua ngumu
 
Kumbe Mwachi Na Wewe Ni Arooo? Ushawahi Kukiona Kitambulisho Cha Usalama Sio?Kilimdondoka Afisa Usalama Ukamuokotea Ukampa Braza Usalama Au Vp? Basi Sawa!
 
Ndio maana nasema mifumo mibovu haitoshi mtu kusema tu mm ni captain kitambulisho kiko wapi?
 
Kumbe Mwachi Na Wewe Ni Arooo? Ushawahi Kukiona Kitambulisho Cha Usalama Sio?Kilimdondoka Afisa Usalama Ukamuokotea Ukampa Braza Usalama Au Vp? Basi Sawa!
Hapana ni raia mwema af hivyo vitambulisho kuviona ni kawaida tu inategemeana na marafiki zako au watu wako wanaokuzunguka
 
Back
Top Bottom